Rais Kikwete na ziara ya kwanza Jijini Mwanza baada ya uchaguzi

Badala ya kutatua matatizo mbali mbali yanayowakabili Watanzania kutokana na kupanda sana kwa gharama za maisha bado anafanya kampeni tu na wakati uchaguzi umemalizika miezi saba tu iliyopita! Huu ni usanii wa hali ya juu!
 
Nadhani mtoa mada yuko sahihi ila wachangiaji tunataka kutoa maana kabisa ya fikira pefu za jukwaa hili. Mwanza ina matajiri na kiasi cha 10 m hakiwezi kuwalaghai watu wa Mwanza ili wampende Kikwete ila inabidi wajijue wazi kuwa wanataka nini ili wasonge mbele. Weje anatakiwa kujielewa kuwa aliungwa mkono ili afanye nini .... nadhani anafanya vyema so far!
 
JK is among the very very cheap minded poiticians this country have ever had..
 
tujiulize ccm walitumia sh ngapi mwaka 2010 katika uçhaguzi wa jimbo hilo? itakuwa hiyo milioni kumi? hana madhara ni gamba tu?
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Kwa hivyo Mwanza bila CDM milioni kumi zisingepatikana? Kumbe upinzani unalipa ehe? Majimbo mengine na yenyewe yajipange kwenda upinzani ili Mkuu JK aweze kuyajali japo kwa TZS 10,000,000 ... lol
 
Badala ya kutatua matatizo mbali mbali yanayowakabili Watanzania kutokana na kupanda sana kwa gharama za maisha bado anafanya kampeni tu na wakati uchaguzi umemalizika miezi saba tu iliyopita! Huu ni usanii wa hali ya juu!
kampeni wanafanya chadema sio kikwete, kwanza waambieni wabunge wenu wanao zunguka nchi nzima kufanya mikutano isio na maana..
 
Fikra za watu wa Mwanza zimebadilika sana na upeo wa ufahamu mabo umekuwa mkubwa mno wanahitaji kazi ya ziada kuwabadilisha watu na kuwarudisha mawazo ya zidumu fikra za CCM,Mwezi uliopita nimetembela maneo mbalimbali ya mko wa Mwanza ukiongea na watu wa wengi wa kawaida kabisa wanakwambia maisha yamekuwa magumu kwa sababu ya uongozi wa JK na CCM yake wamefanya mafuta kuwa bei ghali, umeme hakuna na bei za vitu hasa vyakula vimepanda sana
 
kampeni wanafanya chadema sio kikwete, kwanza waambieni wabunge wenu wanao zunguka nchi nzima kufanya mikutano isio na maana..

wewe ni mbuge wa jimbo gani....? au ni mpiga zumari
 
Safari ya Rais Kikwete Mkoani Mwanza ni dalili za kupima upepo wa kisiasa kutokana na wimbi la Chama pinzani cha Chadema kuteka Kanda ya Nyanza hivi karibuni.
  • Je atafikiwa kiwango wananchi waliohudhuria Chadema?
  • Je atasambaratisha ngome ya Chadema Mkoani Mwanza?
  • Kuchangia mfuko wa maendeleo jimboni kwa Wenje ni njia ya kujaribu kuwateka wananchi wa Mwanza?

Hebu tupe takwimu za Matokeo ya urais ya JK mkoani Mwanza dhidi ya wagombea wengine
 
Fikra za watu wa Mwanza zimebadilika sana na upeo wa ufahamu mabo umekuwa mkubwa mno wanahitaji kazi ya ziada kuwabadilisha watu na kuwarudisha mawazo ya zidumu fikra za CCM,Mwezi uliopita nimetembela maneo mbalimbali ya mko wa Mwanza ukiongea na watu wa wengi wa kawaida kabisa wanakwambia maisha yamekuwa magumu kwa sababu ya uongozi wa JK na CCM yake wamefanya mafuta kuwa bei ghali, umeme hakuna na bei za vitu hasa vyakula vimepanda sana

Ha ha ha aaaaa kama walipokea mwitikio wa cdm wa kupewa vitu bure unategemea nn zaidi ya maisha kuwa magumu ? waambie wafanye kazi bana sera ya cdm ya vitu vya bure haifanyi kazi dunia hii, Besigye alijaribu nae kuiiga amefanywa vibaya km slaa
 
jk mjanja kweli kweli katanguliza harambee kumbe yy mwenyewe anafuata nyuma , hahahaha

Hapo kwenye red. JK ana ujanja gani?? Angekuwa mjanja nchi ingekuwa na hali hii?? Angekuwa mjanja CCM ingekuwa inachungulia kaburi?? Hakuna kitu kichwani mwake
 
Back
Top Bottom