Sasa nimepata picha. Zitto kabwe ni mshiriki mkubwa wa kikwete. Ni zitto aliyewakilisha mchango wa tsh 10mil kutoka kwa jk, ktk hafla ya kuchangia mfuko wa elimu, wenje akiwa muandaaji, kumbe mil 10 ilikuwa ni kisafisha njia? Jk, kwa nn amtume zitto wakat kandoro mwakilishi wake yupo? Naanza kushawishika na mawazo ya weng kuhusiana na zitto.
On the red - Spot on!
Si vizuri ku-generalise watu wa maeneo fulani lakini nashawishika kusema kwa siasa za Tanzania na hasa kwa vyama vya upinzani watu wa Kigoma wanaonekana kuwa vegeugeu - wanatoa picha ya kutoaminika. Dr.Kaborou (spelling), David Kafullila, na sasa Zitto. Pia tukumbuke baada ya uchaguzi Kikwete alisikika akilia na UDINI, Zitto naye anadakia akisema kuwa hata yeye anaamini kuna udini (including jimboni kwake).
Kwa wale waliokuwa wanasema huyu dogo karudi kwenye mstari think again. Hana jinsi, he has to do as they tell him maana alishapigwa bei a looooong time ago. Kwa kifupi Zitto yuko kwenye njia panda- sijui anapataje usingizi huyu mtoto. Kwa upande mmoja ni 'stakeholder' wa mmoja wa mapacha watatu, upande mwingine ni 'stakeholder' wa magogoni, wakati huo huo ni anajiona yeye ni mpambanaji ndani ya chadema (zitto vs mbowe vs uchagga vs udini!!!!) then anajitokeza kwa umma kama mmoja wa makamanda wa chadema!!! Mkorogo.