nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
- Monday, November 28, 2011, 6:28
- Habari kuu, Mtanzania
- Wakutana uso kwa uso Ikulu
- Mjadala mzito, waahirishwa mpaka leo
Kulwa Karedia na Maregesi Paul
"
Nilitamani sana kuwaeleza kilichojadiliwa, lakini nashindwa kuwaambia kwa sababu mazungumzo hayakumalizika, kwa hiyo tutatoa taarifa kamiliki baada ya mazungumzo kumalizika,"Kwa kifupi tu ni kwamba tulikutana na Rais, mawaziri na wasaidizi wake saa 9:30 mchana Ikulu mpaka saa 12 jioni, kikao kilipoahirishwa.
"Tumefanikiwa kumweleza Rais hoja zetu zote ambazo tulizokuwa nazo, miongoni mwa hoja hizo ni nini kilichosababisha wabunge wa Chadema kususia mjadala wa Katiba mpya katika kikao cha Bunge kilichomalizika wiki iliyopita,"Hoja nyingine tumemtaka Rais asisaini Muswada huo kabla ya Desemba Mosi kama alivyokuwa ameahidi wakati akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam,
"Tumeona kama akisaini Muswada huo, ni wazi utaligawa taifa kwa sababu kuna baadhi ya watu wanadai haukufuata taratibu zilizokuwa zinahitajika.
"Baada kutoa hoja zetu, tumemwachia Rais na wasaidizi wake, wakazijadili na tutapoonana kesho (leo), watatupa majibu na majadala utaendelea zaidi,"kilisema chanzo chetu.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mawaziri waliohudhuria ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wasira,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emannuel Nchimbi.
Kwa upande wa Chadema, waliongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Mbowe pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na ni Mbunge wa Hai.
Wengine ni Makamu Mwenyekiti Bara, Said Amour Arfi, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed, Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Mbali na hao, waliokuwapo Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambaye pia ni Katibu wa Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Halmashauri na Bunge, John Mrema na makada wa chama hicho, Profesa Abdallah Safari na Profesa Mwesiga Baregu.
Kikao hicho, kimefuatia ombi la Chadema kutaka kuonana na Rais Kikwete ili kumueleza kasoro zilizopo kwenye Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba, ambao yatari umepitishwa na Bunge na sasa unasubiri kusainiwa na Rais ili kuwa sheria.
Itakumbukwa wakati wa majadala wa Muswada huo, wabunge wa Chadema na wale wa Chama cha NCCR-Mageuzi, walisusia na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, kwa madai kuwa hawakutendewa haki.
Wakati huo huo, Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikisema Rais Jakaya Kikwete na ujumbe wa Serikali walikutana na ujumbe wa CHADEMA na kufanya mazungunzo Ikulu.
Taarifa hiyo ilisema kuwa, mazungumzo hayo yalifanyika katika mazingira ya urafiki na kwa ujumbe wa CHADEMA kuwasilisha mapendekezo kuhusu mchakato wa Katiba mpya ya Tanzania.
"Serikali imepokea mapendekezo hayo, hata hivyo, pande zote mbili zimekubaliana kukutana tena asubuhi ya kesho (leo), ili kuipa nafasi Serikali iweze kutafakari mapendekezo hayo.
"Lakini, pande hizo mbili zimekubaliana kuwa, Katiba ya sasa ni Katiba nzuri iliyolilea taifa kwa miaka 50 iliyopita kwa sababu ni Katiba ya sasa iliyoliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na amani, utulivu na kupata maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepata mpaka sasa.
"Pia pande zote mbili zimekubaliana kuhusu umuhimu wa kutunga Katiba mpya kama Rais Kikwete alivyoliahidi taifa wakati wa salamu zake za mwaka mpya Desemba 31, mwaka jana, Katiba ambayo italiongoza Taifa la Tanzania kwa miaka mingine 50 ijayo.
"Katika mazungumzo hayo, Rais aliwahakikishia wajumbe hao wa CHADEMA ambao waliongozwa na Mwenyekiti wao Mbowe kuwa ni dhamira yake na ya Serikali kuhakikisha Tanzania inapata Katiba mpya.
"Katika mkutano huo, pande zote mbili zimekubaliana kuwa, ni jambo muhimu sana kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa.
"Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa, mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia misingi ya mambo mengine muhimu kwa Taifa la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, kuligawa taifa kwa misingi ya udini na ukabila ama kutugawa kwa misingi ya maeneo," ilisema taarifa hiyo.