Rais Kikwete na mazungumzo na ujumbe wa CHADEMA

Chadema are not safe from ill-will tactics of Magamba to make sure that the political opposition is crippled at all cost. They have successfully managed to silent CUF's activism buy merely engaging them into Zanzibar's government hierarchy and now Chadema seems to descend into the same trap. I advise Magwanda to be exta careful with CCM's double-dealing nature who might take an advantage of this meeting to entice Magwanda into accepting a coalition deal.
Mwita 25 ushauri wako ni mzuri sana na imani yangu CDM ni chama cha watu na si mafisadi na kinawasikiliza wananchi wake ambao ndiyo mtaji wao.
Pia nikutoe hofu CDM hawawezi kuanguka katika mtego mwepesi kama huo.
 
Wamekubaliana nini mkuu?

Wamekubaliana haya/hivi:
Serikali imepokea mapendekezo hayo, ilieleza taarifa ya Ikulu. Hata hivyo, pande zote mbili zimekubaliana kukutana tena leo asubuhi ili kuipa nafasi Serikali iweze kutafakari mapendekezo hayo.

Kwa mujibu wa Ikulu, lakini pande hizo mbili zimekubaliana kuwa Katiba ya sasa ni Katiba nzuri iliyolilea Taifa kwa miaka 50 iliyopita kwa sababu ni Katiba ya sasa iliyoliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na amani, utulivu na kupata maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepata mpaka sasa.

"Pia pande zote mbili zimekubaliana kuhusu umuhimu wa kutunga Katiba mpya kama Mheshimiwa Rais Kikwete alivyoliahidi taifa wakati wa salamu zake za Mwaka Mpya Desemba 31, mwaka jana, 2010, Katiba ambayo italiongoza Taifa la Tanzania kwa miaka mingine 50 ijayo," ilieleza taarifa hiyo.

Katika mazungumzo hayo, Rais aliwahakikishia wajumbe hao wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwa ni dhamira yake na ya Serikali yake kuhakikisha kuwa Tanzania inapata Katiba mpya.

Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa.

Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia misingi ya mambo mengine muhimu kwa Taifa la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa misingi ya udini na ukabila ama kutugawa kwa misingi ya maeneo.
 
Mwita 25 ushauri wako ni mzuri sana na imani yangu CDM ni chama cha watu na si mafisadi na kinawasikiliza wananchi wake ambao ndiyo mtaji wao.
Pia nikutoe hofu CDM hawawezi kuanguka katika mtego mwepesi kama huo.

Yote yanawezekana, ingawa la wao kuanguka litakua gumu kidogo kwani tayari wameshaonesha kule Arusha. Ninachokiona kwa CDM, wanataka siku wakiwasha moto basi wawe na kinga kwamba tulimshauri Rais lakini hakutusikia, wananchi wameamua kudai uhuru wao.

Nina imani kubwa kuwa CCM+KIKWETE, hawatajitahiri wao wenyewe, ila wananchi ndio watakaowatahiri. Tukiwaachia kazi ya kujitahiri, tusitegemee suala hilo kutokea. wanachokihitaji ni kuendelea kujenga mtandao wa kulindana, wanakula halafu no action na wana uhakika na kinga yao.

Ikumbukwe tu kuwa, kulikuwa na jitihada za kumfikisha Mkapa kwa madhambi mengi aliyoyafanya, lakini JK akasema, mwacheni mzee apumzike, mbon kawafanyia mengi mazuri? Kinga hii ndiyo kikwete anaihitaji kwani naye kama mkapa ana madhambio mengi aliyowafanyia watanzania.

kupatikana kwa katiba ya watanzania, kutahatarisha usalama wake, familia yake na mali walizomiliki hasa kwa kipindi cha urais wao
 
Katika mkutano kati ya Rais Kikwete aliyeambatana na Maafisa wengine wa Ikulu pamoja na Wawakilishi wa CHADEMA walioongozwa na Mh Mbowe,ajenda kuu ilikuwa ni Katiba.Wawakilishi wa CHADEMA walipewa nafasi ya kuwasilisha maoni yao mbele ya Rais yahusuyo Katiba.Pamoja na kuwepo kwa makubaliano juu ya mambo mbalimbali ambayo kimsingi si ajenda iliyowapeleka CHADEMA Ikulu,sintofahamu ilijikita juu ya suala la endapo Rais ausaini Muswada wa Tume ya Katiba au la.CHADEMA walionyesha dhahiri jinsi wasivyokubaliana na kusainiwa kwa Muswada huo uliopitishwa na Bunge 'kiholela'.Rais na Maafisa wake wa Ikulu walijitahidi bila mafanikio kuutetea na kuusifu Muswada huo.Si kweli kwamba kulifikiwa makubaliano.Baada ya sauti kuanza kupazwa kwa jazba,Rais Kikwete aliahirisha Kikao hicho hadi leo.Baadaye nitatoa taarifa kamili nikipata nafasi.Kikao kimeshaanza...........muda kidogo!
 
binafsi nafarijika kuona viongozi wetu wakuu wanakaa pamoja na kukubaliana mambo ya msingi likiwemo la kutambua maendeleo ambayo nchi yetu imefikia miaka 50 tangu tumepata uhuru.
 
Sijaelewa vizuri CHADEMA wameenda Ikulu kuzungumza na Mwenyekiti wa CCM au Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama ni Rais basi wanatakiwa watoe tamko la kumkubali kuwa alishinda katika uchaguzi wa Mwaka 2010.
Kwani walikataa kumtambua? Walisema hakushinda kwa wingi wa kura (kihalali!) na hivyo tume ya uchaguzi ilikosea kumtangaza kama mshindi! Kwa sheria na katiba ya sasa ya Tanzania tume ya uchaguzi ikishakutangaza....basi unakuwa rais....hakuna kuhoji!
 
I like technology.
Nasisitiza jamani kikao kisiwe cha mashindano na kila upande ujitahidi kudhibiti emotions.KWA KILA NAMNA ISIPOKUWA JAZBA RAIS AAMBIWE MAPUNGUFU YA MUSWADA HUO.
 
Whether Magwanda succeed with their plan to prevail upon JK to delay the signing of the disputed bill or not, we should bear in mind that CHADEMA's delegation does not reflect the general public sentiments. The common citizen, who is supposedly major stakeholder of the whole process, seems to have been left aside and his position subsequently being substituted by political and civil society groups. We as Tanzanians should therefore come forward separately, gather our opinions pertaining to how the mechanism of composition of new constitution must be, and set up a representative committee to carry our recommendations to JK for consideration.
 
kweli kazi ipo.mh rais atumie busara tu asiusign mswada,tusipoteze muda mwingi kwa mambo madogo kama hayo,haihitaji kuwa na degree kujua kama huo mswada ni mbovu au lah.
 
Sa ivi ikulu tunaingia kama cinemax, dah! raha sana. Kumbe hii sehemu hua ina ingilika bana.. Lakini Hivi huyu jamaa alivyoanza kufungulia milango sa hivi si watampiga stop wakubwa zake?
 
Whether Magwanda succeed with their plan to prevail upon JK to delay the signing of the disputed bill or not, we should bear in mind that CHADEMA's delegation does not reflect the general public sentiments. The common citizen, who is supposedly major stakeholder of the whole process, seems to have been left aside and his position subsequently being substituted by political and civil society groups. We as Tanzanians should therefore come forward separately, gather our opinions pertaining to how the mechanism of composition of new constitution must be, and set up a representative committee to carry our recommendations to JK for consideration.

Tupo level ya kitaifa, wewe endelea kujadili vyama ila kumbuka level ya uchama ni ndogo kuliko level ya utaifa.
Taifa kwanza chama baadae.
 
binafsi nafarijika kuona viongozi wetu wakuu wanakaa pamoja na kukubaliana mambo ya msingi likiwemo la kutambua maendeleo ambayo nchi yetu imefikia miaka 50 tangu tumepata uhuru.
 
Kabla ya majadiliano hayajaanza Chadema na CCM wanakunywa chai ya Ikulu, ili waanze mjadala
Cha ajabu ni nini? Hivi mnadhani vilivyopo Ikulu ni mali ya CCM hivyo aliye nje ya CCM anakula fadhili? Acha chai tuu hata kitanda anacholalia JK na mamaa pale ikulu ni mali ya watanzania wote. Amka wewe
 
Today i will sticky with you for a while, CHADEMA wamechagua kujidhalilisha, yote waliyokwisha sema kuhusu kikwete, wananchi kuwa mahakama ya mwisho na kutoka bungeni kaaa.

Leo hana hoja ya kusema wananchi ni mahakama ya mwisho wamekwenda kupiga magoti kwa KIKWETE, sidhani kama kikwete anaitaji support ya chadema kupitisha mswada huo ulishapita wasasa wanaongea naye nini? Kabla ya kutoka bungeni hawakujua kama kikwete ni raisi?

Mkuu naomba nitofautiane na wewe kidogo. Sidhani kama CDM walikwenda kumpigia magoti JK. Tumeshaambiwa walikuwa na mazungumzo na pande mbili zikakubaliana mambo kadhaa. Labda tuwape muda watuweke wazi ni mambo gani waliyozungumza na kukubaliana ndipo tuweze kusema kama CDM wameburuzwa ama la.
 
Back
Top Bottom