Kwenye blue: Ni maneno ya pande zote mbili au kuna mtu amelazimisha?Lakini pande hizo mbili zimekubaliana kuwa Katiba ya sasa ni Katiba nzuri iliyolilea Taifa kwa miaka 50 iliyopita kwa sababu ni Katiba ya sasa iliyoliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na amani, utulivu na kupata maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepata mpaka sasa.
Nahisi kama Rais au timu yake bado wanataka umma uamini kuwa wao (rais na ccm yake) ndio walitaka katiba mpya na sio 'shinikizo' toka upinzaniPia pande zote mbili zimekubaliana kuhusu umuhimu wa kutunga Katiba Mpya kama Mheshimiwa Rais Kikwete alivyoliahidi taifa wakati wa salamu zake za mwaka mpya Desemba 31, mwaka jana, 2010, Katiba ambayo italiongoza Taifa la Tanzania kwa miaka mingine 50 ijayo
Nimefurahi sana kuona hii movement.CCM na CDM vinaunganika pamoja kuitengeneza tanzania tuitakayo.
Mwanzoni hili waliliweza CUF na sasa naona CDM wameingia. Kwa mantiki hii upinzani Tanzania sasa basi.
Pasco unajua haya ni mazungumzo, CHADEMA hawajapeleka mapendekezo ili JK aamue, wamepeleka mapendekezo ili wajadiliane kupata muafaka.Hii ni muhimu sana, anatafakari walichopendekeza ili naye ashauriane na timu yake, kesho asubuhi awape Chadema maamuzi yake!.
mkuu, mimi naishangaa sana hii kurugenzi ya mawasiliano ikulu, press release gani hii sasa. wangenyamaza tu.Hii Press release imejaa propaganda
Mkuu kweli umesoma hii taarifa between lines. CDM wamekubali (kwa mujibu wa taarifa) kuwa atiba hii ya sasa imeleta maendeleo makubwa kwa nchi yetu pia kwamba ni nzuri. Halafu wanakubali kuwa katiba itakayotungwa itaiongoza Tanzania kwa miaka 50 ijayo; ikitokea watanzania wanataka kuibadili baada ya miaka kumi? Si vyema kusema kuwa katiba itaiongoza Tanzania kwa miaka 50 ijayo kwani huenda wengine wkaiona haifai baada ya miaka kumi! Tusubiri tuone.Wameanza kutunga makubaliano sioni mbele kuna nini. si amini Ujumbe wa CDM unaweza kukubali uzuri wa katiba hii ya mkoloni.
Msemaji mwingine wa Ikulu ...Hii ni muhimu sana, anatafakari walichopendekeza ili naye ashauriane na timu yake, kesho asubuhi awape Chadema maamuzi yake!.
Hawa viongozi wa CHADEMA wamenihuzunisha sana leo. Yaani wanapiga picha na Rais wasiyemtambua huku wanacheeeeeeka meno yote 32 nje. Hapo unategemea nini zaidi ya kushuhudia ndoa nyingine ya mke wa pili wa CCM mwaka 2015. Kweli siasa za Tz ni vichekesho tupu.
Inavyoelekea kuna wana CCM wengi ambao hawakupenda CDM walivyoenda ikulu, ndio maana wanajaribu kuifananisha na CUF ili CDM ikate tamaa. Kwenda ikulu si kujiunga na CCM, basi mabalozi wote wa nchi za nje wanaoenda ikulu wanaenda kujiunga na CCM ! CUF case yaoni tofauti na CDM, wao CUF wana Makamu wa Rais na mawaziri katika serikali ya CCM, sio simply kwenda ikulu!
Hii pia imenishangaza miye!Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia misingi ya mambo mengine muhimu kwa taifa la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa misingi ya udini na ukabila ama kutugawa kwa misingi ya maeneo.