Rais Kikwete mgeni rasmi Tamasha la Pasaka

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Rais Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 24 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mshama Promotions, Alex Msama aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Rais amethibitisha kubariki tamasha hilo.
Napenda kuwaambia kwamba Rais wetu mpendwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amethibitisha kuwa mgeni rasmi katika tamasha letu mwaka huu.
Amekubali kushirikiana na Wakristo wote kusherehekea Sikukuu ya Pasaka Diamond Jubilee, alisema Msama aliyeambatana na mshauri wa kamati ya maandalizi, Askofu Rashid Matigisa, Askofu Philemon. Wainjilisti John Benjamin na Elia Mashaka pamoj na Shemasi Benjamin.
Mshama alisema kwa niaba ya Kamati namshukuru Rais kwa kukubali mualiko wa kuhudhulia Tamasha hilo, wasanii mbalimbali wa muziki wa injili wamethibitisha kushiriki ni pamoja na Rose Muhando. Anastazia kutoka kenya.
Mwananchi march 14, 2011
 
Ngeshangaa kama tamasha lingekuwa ni la imani hafu wamualike huyo mtu. Watu wanajiandaa kusherehekea pasaka bila kujua kuwa kwaresma ni muhimu!
 
Kuwepo kwa JK ni kwa sababu Frola Mbasha naye yumo, hilo tamasha tayari limegeuzwa mradi wa mkulu kujisafisha baada ya kueneza udini
 
binafsi sina muda wa kupoteza, tayari tamasha limetekwa na kuwa la kisiasa.
 
mimi nahisi washauri wa rais kila kukicha wao ni kutafuta matamasha kama haya na kubembeleza waandaaji ili wamualike mkuu wa nchi kama njia ya kujisafisha..tatizo lipo kwa haya waandaaji ...kwanini wasiweke wanasiasa nje ya mambo ya Dini.....?
 
MODS please pelekeni hii habari kwenye jukwaa la celebreties, hapa ni jukwaa la siasa, hii habari hatuhiitaji hapa.
 
mzee wa viburudisho............anataka kwenda kuwaona kina rose mhando na flora mbasha wakimkatia viuno.

rais wenu jamani kwa masihara!! simuwezi!

anatamani kuwa mswati.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 24 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mshama Promotions, Alex Msama aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Rais amethibitisha kubariki tamasha hilo.
Napenda kuwaambia kwamba Rais wetu mpendwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amethibitisha kuwa mgeni rasmi katika tamasha letu mwaka huu.
Amekubali kushirikiana na Wakristo wote kusherehekea Sikukuu ya Pasaka Diamond Jubilee, alisema Msama aliyeambatana na mshauri wa kamati ya maandalizi, Askofu Rashid Matigisa, Askofu Philemon. Wainjilisti John Benjamin na Elia Mashaka pamoj na Shemasi Benjamin.
Mshama alisema kwa niaba ya Kamati namshukuru Rais kwa kukubali mualiko wa kuhudhulia Tamasha hilo, wasanii mbalimbali wa muziki wa injili wamethibitisha kushiriki ni pamoja na Rose Muhando. Anastazia kutoka kenya.
Mwananchi march 14, 2011

Ni vizuri unapotaja Maaskofu useme pia ni wa dehebu lipi. Kama vile tunavyosema Mchungaji Mstaafu wa KKKT Mwasapile...
 
Heko JK kwa kukubali kuwa mgeni rasmi Diamond. Naona unamjibu EL aliyekuwa pia mgeni rasmi juzi kati hapo hapo diamond kwenye shughuli ya dini vile. Lakini kwa siku hiyo EL hajaongea chochote kile cha kisiasa!
 
MODS please pelekeni hii habari kwenye jukwaa la celebreties, hapa ni jukwaa la siasa, hii habari hatuhiitaji hapa.

Mkuu naona hii Thread imekuwa Incese kwako, kuwa mvumilivu Tamasha la Pasaka nadhani ni sehemu ya ibada kwa Wakirto watakuepo Maaskofu na viongozi wa kisiasa. nakushangaa wewe unaona hapa sio sehemu yake sehemu yake ni jukwaa la Celebreties, kama habari uipendi sio lazima uchangie kaa pembeni waache wenzio wachangie
 
Sihitaji malumbano, nadhani unafahamu vyema maana ya platform, sasa ikiwa kila mtu atakuwa anapost thread yake kwenye jukwaa la siasa kutakuwa na maana gani ya kuwa na platform? au hii ni habari ya siasa? naomba unieleweshe wewe maana labda mimi sielewi.
 
mimi nahisi washauri wa rais kila kukicha wao ni kutafuta matamasha kama haya na kubembeleza waandaaji ili wamualike mkuu wa nchi kama njia ya kujisafisha..tatizo lipo kwa haya waandaaji ...kwanini wasiweke wanasiasa nje ya mambo ya Dini.....?

Vipi ikulu wameanzisha marketing department ya kuuza sura ya JK?
 
Back
Top Bottom