Rais Kikwete kuzungumza na wazee wa CCM Dar leo jioni!

Status
Not open for further replies.
Hatuwezi fananisha walimu na madaktari.Walimu wakigoma athari zake zinaonekana baada ya mda mrefu lakn madokta wakigoma athari zake zinaonekana kwa muda mfupi tu.Unaweza kumlazimisha punda kwenda mtoni lakn huwezi mlazimisha kunywa maji.Tutagemee hali mbaya zaidi katika sekta ya afya
 
JK mtu wa ajabu, badala ya kukaa na kuzungumza na Drs yeye ameamua kwenda kusema na Wazee wa DSM kesho jioni.

Chanzo: NEWS Channel Ten
Mkuu, lazima kuongea na waliofanana na wewe!
Kama mweupe unaongea na weupe wenzako yakhe!
 
Jk akikaa kimya tunalalamika, akitaka kuongea tunalalamika, sijaona tatizo la kuzungumza na wazee kwa masuala nyeti ya taifa ni vema tuwe na subira atakapozungumza ndipo tujadili hotuba yake.
 

Yaani magamba wazee katika chama chake! Asichanganye wazee wote hapa Dar kuwa na mawazo kamo hao wazee wanaopioga makofi katika kila kitu -- na ndo maana wamelifikisha taifa lilipofika.

Wazee wenyewe wapo? Si wanaumwa presha na kisukari na ma dr wamegoma?
 
Jk akikaa kimya tunalalamika, akitaka kuongea tunalalamika, sijaona tatizo la kuzungumza na wazee kwa masuala nyeti ya taifa ni vema tuwe na subira atakapozungumza ndipo tujadili hotuba yake.

Mama Porojo, mambo sensitive ya taifa kwanini uongee na wazee? Mi nadhani kama issue ni ma dr akaongee nao wamgonge maswali yaishe mana PM kashindwa. Otherwise aongee na vyombo vya habari kama ni maswali wamwulize. Kwa hawa wazee tutegemee mipasho na vichekesho tuu
 
Nilidhania angeongea na madaktari,hasa baada ya Pinda kushindwa...oh,wazee wa Dsm!?it reminds me of ther infamous mbayuwayu speech!
 
wote hao kwenye red ni wajinga sana ndio wanaoleta maendeleo nyuma kama kweli madaktari ni waongo angeenda kuhutubia pale cpl aone moto wake
Mkuu wanaweza wakawa wajinga kweli sikatai
Lakini PM alicho zungumza na DRs ndio msimamo wa gvt akiwemo JK na sote tunajua ilivyoshindikana kupata suluhu.
Sasa watu wote tulikuwa tunapiga kelele Rais yupo kimya, kaamua kuongea kupitia wazee wa DSM imekuwa nongwa eti kwanini asihutubie cpl?
Kwani hii ni mara ya kwanza kwa marais kuongea na taifa kupitia wazee wa dsm? au unadhani pale anakwenda kujadiliana na mtu?
Taifa lilihitaji kusikia kutoka kwa rais, rais kaamua kuongea anapoongeleaga wewe huta unataka aende cpl
Sielewi kwanini hoja iwe wazee wa dsm na si ataliambia nini taifa kupitia hao wazee, maana inakuwa ni kana kwamba hao wazee ndio wameshikilia mustakabali wa sakata hili................

 
..JK mambo yameanza kumfika shingoni kesho atatafuta huruma za wazee kwa kuongea nao jijini DSM saa kumi jioni.Bila shaka hawa watakuwa wazee wa CCM tu.Tutakumbuka kuwa JK alifanya hivi wakati mgomo wa walimu chini ya TUCTA ulipotangazwa..na hapa ndipo ile kauli ya akili ya mbayuwayu changanya na ya kwako ndipo alipoitoa.Mgoja tuone..tutegemee hotuba yenye kujaa hoja zenye kutaka huruma za wazee dhidi ya matatizo mengi yanayoisumbua hii nchi kwasasa.

SOURCE:CHANNEL TEN

ndivyo alivyo itakuwa ni madongo na mishushuo kwa madaktari..
 
Mkuu Kiby Wazee wa Dsm si kamati yoyote isipokuwa inatakiwa ujue historia kidogo.
Nchi hii ilipopata uhuru wazee wengi waliofanikisha hilo zoezi walikuwa wakaazi wa hapa DSM na hata katika kuunda Serikali wengi walikosa sifa za kuongoza kwa elimu zao kuwa ndogo au kutokuwa nazo kabisa.
Nyerere kwa kutambua hilo akawa ana waenzi kwa kuwaita sehemu na ku address isuues mbali mbali za kitaifa kupitia kwao,
Utaratibu huu ukaendelea na kujenga mazoea na Mwinyi akaendelea nao kisha akaja Ben na sasa JK anaendelea nao
Cha umuhimu hapa ni kwamba Rais haongei na wazee wa DSM ili kupata huruma yao au anaongea nao eti kwakuwa upeo wao ni mdogo kuliko atakayoongea kama unavyodhani wewe, hivyo hata pata upinzani

Pale haendi kujadiliana na mtu, pale atasimama na kuongea yaliyomo moyoni mwake kama Rais akimaliza anasepa.

Madai kwamba wale wazee ni wa magamba yanaweza kuwa na ukweli kwasababu hapa DSM wazee wazawa karibu wote ni CCM damu,
wazee wakuja ni mara chache sana kwenda kwenye mambo kama haya na hawa wengi ni wastaafu waliochoshwa na CCM

Ki msingi hapa ni rais anataka kuongea na taifa kupitia wazee wa dsm na si anaongea na wazee wa dsm kwasababu hao wazee ndio watakao amua jambo fulani, NOPE.............

Kumbe ni kuaddress na si kuongea!

Je huyo muasisi wa huo utaratibu alikuwa anatumia huo utaratibu kwenye nyakati za wanataaluma kudai maslahi yao kama ilivyo sasa,au ilikuwaje...
 
Sio wana JF Wote wanapenda haya matusi, chonde bro, ukichukizwa basi jibu kwa kauli nzuri. mmeniharibia siku yangu leo.

Poa bro,umwambie na huyo mwanaharamu ajirekebishe kama ulivonambia mimi kistaarabu.ubarikiwe sana.
 
Kwakweli binafsi kuna kitu kikubwa sana kinanisumbua kuhusu huu u great thinker wetu humu JF, Haiwezekani watu wakawa wana comment vitu utadhani wamezaliwa jana. sredi nzima imejaa tuhuma dhidi ya wa zee..................
Sina tatizo na kudhani atakacho ongelea kesho, natatizwa na watu kutatizika kwa JK kuongea na wazee wa mkoa wa Dar es salaam.
Kanzia Nyerere hadi Ben wote walifanya hivyo, iweje iwe kituko kwa JK? kuongea na wazee ni namna tu ya kuongea na taifa kupitia wazee vinginevyo angejifungia nao sehemu.
Tusi watusi wazee wetu iwe ni wa CCM au la, hawana kosa lolote, kupitia kwao taifa litapata msimamo wa Rais that is all..........
Tumseme JK kama JK na Serikali yake na si kuwasema vibaya wazee wa watu as if wamefanya nini sijui

Tatizo watu waliingia na gia za ujana, kasi mpya, ari mpya, sasa uzee wa nini? Pili, walau kwa mikutano ya nyuma wazee ni kiduchu sana, wengi ni vijana (wazee?), Tatu, mikutano ya wazee imekuwa mipasho na madharau na hili sio jambo jema kwa jamii yetu! Nne,ukizozana na mfanyakazi wako ofisini huendi kuongelea na jirani, mtu mzima unakaa chini na kuyamaliza hasa pale inapotekea wewe ndio mshika mpini! Na mwisho, wazee wa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki nao wataalikwa au hawana nauli?
 
Kesho jioni JK anategemewa kuongea na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam..


source: Channel Ten

Ni wajinga pekee watakaomwamini na utumbo wake anaotaka kutoa badala ya kutafuta namna ya kutatua tatizo anaenda kuhutubia magamba wenzake waliochoka. Hao wazee hawawezi malori lakini, mtawaangusha, shauri yeni! Maana ccm haiwezi kushawishi watu kuhudhiroa mikutano yake ka,a haikawaleta na malori na kuwapa pilau
 
Kumbe ni kuaddress na si kuongea!

Je huyo muasisi wa huo utaratibu alikuwa anatumia huo utaratibu kwenye nyakati za wanataaluma kudai maslahi yao kama ilivyo sasa,au ilikuwaje...
Nyerere alifanya kama wanavyofanya akina JK, anasimama anongelea mambo ya kitaifa akimaliza anasepa. full stop, ni hotuba tu........
 
Jakaya anao uhuru wa kuongea na anayemtaka na kwa wakati anaoutaka. Kama amechagua kuongea na wazee wa Dsm huo ni uamuzi wake na hatuna budi kuuheshimu.

Na pia si vyema kuanza kutukana ama kutoa maneno ya kashfa kwa Mh raisi na wazee wa Dsm, kwani mpaka sasa hakuna anayejua Raisi atasema nini hapo kesho. Matusi si hulka ya watanzania, tumefundishwa kuheshimiana na kuishi pamoja kwa upendo.
 
wanaomkejeli kikwete ni wale loosers ambao wana gubu mioyoni mwao,kwao hakuna jema hata moja

ndio sababu ya kuwepo jukwaa hili huru unaweza kulitumia kuandika mema ya JK badala ya kutukana humsaidii nduguyo unamharibia.
 
..JK mambo yameanza kumfika shingoni kesho atatafuta huruma za wazee kwa kuongea nao jijini DSM saa kumi jioni.Bila shaka hawa watakuwa wazee wa CCM tu.Tutakumbuka kuwa JK alifanya hivi wakati mgomo wa walimu chini ya TUCTA ulipotangazwa..na hapa ndipo ile kauli ya akili ya mbayuwayu changanya na ya kwako ndipo alipoitoa.Mgoja tuone..tutegemee hotuba yenye kujaa hoja zenye kutaka huruma za wazee dhidi ya matatizo mengi yanayoisumbua hii nchi kwasasa.

SOURCE:CHANNEL TEN
Tutegemee uchafuzi zaidi wa hali ya hewa. Rais akae chini atafute ufumbuz wa matatizo yanayoikabili nchi na sio kutafuta huruma ya wazee. Anawaachia akina Pinda kufanya maamuzi mengi wkt nao uwezo wao wa kutatua matatizo ni mdogo cjui anategemea nini. Nionavyo mimi akina Pinda na wengineo ni kama wameamua kusabotage uongozi wa JK cjui kwanini JK hajiongezi na kungundua hili!!!
 
hizi choko choko na chuki zitaifikisha nchi pabaya,sasa libya imegawanyika na kenya wako the hegue.endeleeni na mjue dhambi hii itawatafuna mpaka makaburini

Jenga hoja Rais hawezi kupendwa na kila mtu hii haipo duniani kote. Rais yuko Ikulu kwa kodi za wote kwa nini asisemwe. Ni akili mgando kudhani wanaomkosoa Rais wana chuki naye mwambie atoke ikulu kama ni Rais wako peke yako.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom