Rais Kikwete kuzungumza na wazee wa CCM Dar leo jioni!

Status
Not open for further replies.
Hivi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wazee wa Dar ni kamati ipi?
Unajua mimi mwenyewe najifahamu nikikutana na mtu ambae najua kwamba kiingereza kwake hakipandi, naongea kwa comfo na kuchepea kote siwezi kukuona. Lakina akiwa ni mtu ambae nafahamu kinapanda hata kile changu cha kuchapia kinapotea. Hii haina tofauti na Jk. Ana kawaida ya kuwakimbia kwa kuyakwepa makundi ya wenye akili na kutafuta makundi ambayo hata kutofautisha mkono wao wa kushoto kutoka kwa wa kulia hawajui. Anatamani na kufurahia kushangiliwa na washabik,. hataki ku-crack na kuyajadili masuala magumu katika uhalisia wake.
Dawa ya maleria ni kunywa dozi yake yote japo ni chungu na sii kurahisisha kwa kukata kichwa cha mgonjwa. Hope thati raisi kesho ataongea kama rais wa nchi na sii kama mshabiki wa chama chake kwa ushabiki atakaoshabikiwa na makada. MUNGU IBARIKI TANZANIA!!
.
 
Wazee wa DSM msije mkadanganywa kwa ubwabwa mkasahau mateso ya wanenu kujifunguklia chini, wajukuu zenu kukosa dawa mahospitali, watoto wenu madakktari kuonwa hawana maana na kisha mkashangilia mkidhani ni sikukuuu. Kumbukeni muendapo pale na kutosema ya kweli naamini kuna siku mtakumbuka hiyo nafasi pale mtakapougua na wanenu kuwapeleka muhimbili maana hawana pesa ya private hospital. Ukitaka kuwa maskini kuwa mchoyo, maana sijaona mjukuu wa mangungo aliyerithi mabiliono ya babu yake wakati wa ukoloni. maana mjinga akiingia mkenge ni kumpiga tu na kumpotezea maana ni mjinga.
 
...hotuba ya JK?,huyo m.k.w.e.l.e simwisho wa mwezi wa pili aliuza sura kwenye tv?,sasa nini tena?,anataka kutwambia nini tena?...tumechoka kusikiliza hizo pumba zake,hizo porojo na hadithi zake za abunuasi akamwadithie Mwaanaasha!...
 
Mimi ninge msahauri wangu mpendwa Kikwete. Aaache saiongee chocchote, alichopanga kuongea amwambie Pinda akiseme.
Kwasababu ninavyomjua raisi wangu huyu lazima tu kuna mahali atakosea......tena pakubwa tu... na itazidi kuwafanya watanzania wazidi kuuona udhaifu wa raisi wetu.
 
wanaomkejeli kikwete ni wale loosers ambao wana gubu mioyoni mwao,kwao hakuna jema hata moja
 
..JK mambo yameanza kumfika shingoni kesho atatafuta huruma za wazee kwa kuongea nao jijini DSM saa kumi jioni.Bila shaka hawa watakuwa wazee wa CCM tu.Tutakumbuka kuwa JK alifanya hivi wakati mgomo wa walimu chini ya TUCTA ulipotangazwa..na hapa ndipo ile kauli ya akili ya mbayuwayu changanya na ya kwako ndipo alipoitoa.Mgoja tuone..tutegemee hotuba yenye kujaa hoja zenye kutaka huruma za wazee dhidi ya matatizo mengi yanayoisumbua hii nchi kwasasa.

SOURCE:CHANNEL TEN

hii tabia ya mkuu wa nchi kutatua matatizo ya taifa kwa kuutubia wazee wa ccm sijapata ona hii ni special tanzania.
Mytake.
Tulitarajia angekaa na wahusika watafute muhafaka yeye anakwenda kuhutubia wazee ambao hawatakuwa na mchango wowotezaidi ya kupiga makofia,pilau na nauli.
 
JK kama ataongea kesho na wana ccm wazee namshauri atumie busara na kimya chake kiwe na mshindo mkuu,asije akabwabwaja upuuzi mbele ya madaktari kwani atatia petroli kwenye moto wa gesi na italeta balaa.
 
hii tabia ya mkuu wa nchi kutatua matatizo ya taifa kwa kuutubia wazee wa ccm sijapata ona hii ni special tanzania.
Mytake.
Tulitarajia angekaa na wahusika watafute muhafaka yeye anakwenda kuhutubia wazee ambao hawatakuwa na mchango wowotezaidi ya kupiga makofia,pilau na nauli.
watendaji wake ndio wamekaa na kuongea na madaktari...watu wenye mtindio wa ubongo kama wewe ndio hamtaona wala kujua umuhimu wa rais kuzungumza na taifa kupitia wazee
 
Mkuu Companero, kwani mimi Salva mpaka nijue?. Au na wewe unadhania na mimi ni mtu wa sehemu?. Mimi ni mwananchi tuu kama wewe, naisubiri hotuba hiyo ili niongeze katika mazuri ya JK au mabaya!.

Kaisoma tena posti yako. Imetumia maneno yanayoonesha unajua nini kitakachojiri kesho. Umesema hivi: "Yaani watakiona kisa cha mtema kuni, kilichomnyoa kanga manyoya!". Sasa si uongezee tu katika hayo mazuri/mabaya?
 
JK kama ataongea kesho na wana ccm wazee namshauri atumie busara na kimya chake kiwe na mshindo mkuu,asije akabwabwaja upuuzi mbele ya madaktari kwani atatia petroli kwenye moto wa gesi na italeta balaa.
Mi namshauri asitumie busara afuate maoni ya kina thatha na wenzake.......
 
Kesho ni siku ya hotuba kama ile ya mbayuwayu!. Madokta ambao hawatarejea kazini baada ya hotuba ya kesho, chamoto watakiona!. Yaani watakiona kisa cha mtema kuni, kilichomnyoa kanga manyoya!.

Naisubiri kesho kwa hamu kumsikiliza rais wetu JK ambae ili nijue nitaongeza post kwenye thread ya mazuri yake au mabaya yake!.

Yaani kama vile uko kwenye mind yangu..

Atachimba mkwara kwamba,ambaye hatafika kazini na kufanya kazi mujibu wa zamu yake atawajibishwa...
Na atasema serikali yoyote haishinikizwi na makundi ya watu wachache kutekeleza matakwa yao..
Na mwisho atasema wale watakaoendelea wataboreshewa maslahi yao,ila wavute subira..
Na wazee watapiga sana makofi!
 
Hivi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wazee wa Dar ni kamati ipi?
Unajua mimi mwenyewe najifahamu nikikutana na mtu ambae najua kwamba kiingereza kwake hakipandi, naongea kwa comfo na kuchepea kote siwezi kukuona. Lakina akiwa ni mtu ambae nafahamu kinapanda hata kile changu cha kuchapia kinapotea. Hii haina tofauti na Jk. Ana kawaida ya kuwakimbia kwa kuyakwepa makundi na kutafuta makundi ambayo hata kutofautisha mkono wao wa kushoto kutoka wa kulia hawajui. Anatamani na kufurahia kushangiliwa na washabik,. hataki ku-crack na kuyajadili masuala magumu katika uhalisia wake.
Dawa ya maleria ni kunywa dozi yake yote japo ni chungu na sii kurahisisha kwa kukata kichwa cha mgonjwa. Hope thati raisi kesho ataongea kama rais wa nchi na sii kama mshabiki wa chama chake kwa ushabiki atakaoshabikiwa na makada. MUNGU IBARIKI TANZANIA!!
.
Mkuu Kiby Wazee wa Dsm si kamati yoyote isipokuwa inatakiwa ujue historia kidogo.
Nchi hii ilipopata uhuru wazee wengi waliofanikisha hilo zoezi walikuwa wakaazi wa hapa DSM na hata katika kuunda Serikali wengi walikosa sifa za kuongoza kwa elimu zao kuwa ndogo au kutokuwa nazo kabisa.
Nyerere kwa kutambua hilo akawa ana waenzi kwa kuwaita sehemu na ku address isuues mbali mbali za kitaifa kupitia kwao,
Utaratibu huu ukaendelea na kujenga mazoea na Mwinyi akaendelea nao kisha akaja Ben na sasa JK anaendelea nao
Cha umuhimu hapa ni kwamba Rais haongei na wazee wa DSM ili kupata huruma yao au anaongea nao eti kwakuwa upeo wao ni mdogo kuliko atakayoongea kama unavyodhani wewe, hivyo hata pata upinzani

Pale haendi kujadiliana na mtu, pale atasimama na kuongea yaliyomo moyoni mwake kama Rais akimaliza anasepa.

Madai kwamba wale wazee ni wa magamba yanaweza kuwa na ukweli kwasababu hapa DSM wazee wazawa karibu wote ni CCM damu,
wazee wakuja ni mara chache sana kwenda kwenye mambo kama haya na hawa wengi ni wastaafu waliochoshwa na CCM

Ki msingi hapa ni rais anataka kuongea na taifa kupitia wazee wa dsm na si anaongea na wazee wa dsm kwasababu hao wazee ndio watakao amua jambo fulani, NOPE.............
 
Anajitakia mwenyewe kwani iweje matatizo ya watanzania akawaeleze wazee wa ccm?
au kwa kuwa huwa wanampigia makofi?


hajaanza yeye bali anaendeleza,ila kwa kuwa wewe na wenzako mna gubu mioyoni mwenu ndio mnaamua kuharisha hapa jukwaani
 
Kwakweli binafsi kuna kitu kikubwa sana kinanisumbua kuhusu huu u great thinker wetu humu JF, Haiwezekani watu wakawa wana comment vitu utadhani wamezaliwa jana. sredi nzima imejaa tuhuma dhidi ya wazee..................
Sina tatizo na kudhani atakacho ongelea kesho, natatizwa na watu kutatizika kwa
JK kuongea na wazee wa mkoa wa Dar es salaam.

Kanzia Nyerere hadi Ben wote walifanya hivyo, iweje iwe kituko kwa JK? kuongea na wazee ni namna tu ya kuongea na taifa kupitia wazee vinginevyo angejifungia nao sehemu.

Tusi watusi wazee wetu iwe ni wa CCM au la, hawana kosa lolote, kupitia kwao taifa litapata msimamo wa Rais that is all..........
Tumseme
JK kama JK na Serikali yake na si kuwasema vibaya wazee wa watu as if wamefanya nini sijui

wote hao kwenye red ni wajinga sana ndio wanaoleta maendeleo nyuma kama kweli madaktari ni waongo angeenda kuhutubia pale cpl aone moto wake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom