Rais Kikwete kuzungumza na wazee wa CCM Dar leo jioni!

Status
Not open for further replies.
Kesho ni siku ya hotuba kama ile ya mbayuwayu!. Madokta ambao hawatarejea kazini baada ya hotuba ya kesho, chamoto watakiona!. Yaani watakiona kisa cha mtema kuni, kilichomnyoa kanga manyoya!.

Naisubiri kesho kwa hamu kumsikiliza rais wetu JK ambae ili nijue nitaongeza post kwenye thread ya mazuri yake au mabaya yake!.

Pasco kuna post nimeona kua ulidisco sheria u.d.s.m kama ni wewe kweli,basi sipati shida ku support hiyo post!lazima utambue tofauti ya taaluma ya ma dr na taaluma nyingine!chemsha akili mkuu labda unaweza kufanikiwa ku graduate na bachelor of law,mifano ya mbayuwayu watolee walimu na wengine sio doctors
 
Mimi nabashiri kuwa kesho ataonesha ujeuri wa kikwere usiokuwa na maana na kama hana busara za kuzaliwa atatoa maamuzi ambayo atakuwa ameyatoa kwa kufikiri kwa kutumia MOYO wake na si akili zake; matokeo yake ni kuliangamiza Taifa!!
 
Je, hiyo ni hotuba ya mwezi au ya wiki? maana hujinasibu kuhutubia taifa kwa mwezi ingawa siyo consistance!! mwenzake Mkapa alkiwa anatoa hotuba zake hadi akiwa kitandani nje ya nchi!! wakati mwingine anakatisha ziara ili kutoa monthly speech!! Rafiki yangu JK anatoa hotuba kwa kuvizia!! Lol!!
 
Hivi hao wazee ndo wanaongoza nchi? Mana kila kitu kikimuwia vigumu anakimbilia kwa hao wazee.


Hao wazee si ndio wanaponea kwenye hospitali za taifa? Madaktari wekeni camera zenu vizuri mnase sura za wazee uchwara wakija muhimbili muwape maji badala ya panadol!
 
kesho mimi napaka gundi usoni na poda kichwani na kwenye kope,nakula uzi wa kijani na mkongojo then safari kwa ukumbi najua buku teni haitanipiga chenga.hivi kikao kinafanyika wapi vil?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kama ana nia kweli ya kuzungumza na Wazee, kwanini asiwachukue wale Wazee wa iliyokua jumuia ya East Africa wanaodai mafao yao Zaidi ya miaka 30 sasa!!!
Wale watamfaa sana!!!
 
kesho saa ngapi?
Jamani viongozi wetu waache kufanya vitu kwa mazoea.

Nyerere wakati wa uongozi wake alikua anakutana na hawa wazee wa DSM na kwingineko coz most of them ndo wlikua freedom fighters na suppoers wake kwenye harakati za uhuru. Sasa naona haka kautamaduni kanaendelea mpaka sasahv kwa lengo la kukwepa vijana na watu wa makamo wataoweza kuwachallenge kwenye hizo meeting.

Jamani wazee wanaohudhuria hii mikutani yake wamechoka vibaya sana wanachohitaji ni kupata hako ka seating allowance na kipiga makofi ya kutosha. Kwann viongozi wetu hasa huyu wa sasa ni waoga sana wa kutoa mihadhara ya namna hii vyuo vikuu...?

Hili tukio ningependa lifanyike sehemu kama chuo kikuu cha DSM ili tujue mbivu na mbichi za speech yake
 
magwanda wanapokuwa hawajui nini kinaendelea wana haha!
 
mbayuwayu speech.........kesho analitibua
Kesho JK, atakapokuwa akishangiliwa na watu ambao siyo lazima wawe Wazee, wakiwa wamevalia mashati na fulana za rangi ya kijani na njano.

...atawajaza watu chuki dhidi ya ma-dr, kuwa wamekuwa wanalipwa mshahara kuliko watumishi wengine wa serikali lakini hawaridhiki...kuna wanasiasa(chadema) wanachochea mgomo kwa maslahi ya kisiasa...wanaingilia mamlaka yake ya kikatiba ya kuteua watu anaoona wanafaa(haikubaliki)...

Chama cha kitaaluma cha ma-dr hakina mamlaka kisheria kuitisha mgomo kwani trade unions hazikuhusishawa... hawakutoa notisi ya siku 90 kwa mujibu wa sheria...KISHA atafoka.."hii haikubaliki hata kidogo" atawataka wale md-dr wasiokubaliana na mgomo waendelee na kazi ...wale viongozi wa mgomo watafukuzwa kazi...DPP na DCI wataagizwa
kuchukua hatua...

Watakaoendelea na mgomo watafutiwa leseni hawataweza kufanya kazi hiyo popote duniani.... kisha atashangiliwa sana na "wazee" watakaokuwepo ukumbini...

"CHANGANYA NA ZA KWAKO!!"
 
Sasa wazee watamsaidia ushauri gani kuhusu mgomo wa madaktari? Kweli Jk ameishiwa uwezo wa kufikiri
Another choice of wrong audience.
Ni bora angekaa kwenye TV tu ikulu akabwabwaja.
 
Kama ndio hivyo tunategemea kuona JK anawajbika kuwafukuza kazi hao mawaziri waliosababisha mgomo maana mpaka
sasa maafa yameanza kuonekana asije akaleta siasa kwa kufurahia kupigiwa makofi na hao wazee wake...
 
Acha wazee wapewe mia tano mia tano zao washangilie vizuri huku wakitoka tu gari lao likipata ajali watajua maana ya kushangilia
 
Kesho ni siku ya hotuba kama ile ya mbayuwayu!. Madokta ambao hawatarejea kazini baada ya hotuba ya kesho, chamoto watakiona!. Yaani watakiona kisa cha mtema kuni, kilichomnyoa kanga manyoya!.

Naisubiri kesho kwa hamu kumsikiliza rais wetu JK ambae ili nijue nitaongeza post kwenye thread ya mazuri yake au mabaya yake!.

Yule mganga wake wa kule kijijini kusikofikika kwa gari hasa kipindi cha mvua si alimwambia ukweli kuwa vijana hata wa CCM hawakumchagua kabisa, hivyo ili aweze kumaliza kipindi chake salama ahakikishe hakutani uso kwa uso na vijana, hivyo anachofanya ni kuwakwepa vijana.

Mpe salamu zangu kuwa akiwa anampelekea yule mganga wake ng'ombe anipitie na mie maana twatoka kijiji kimoja na mie sina usafiri mwenzie.
 
Kesho ni siku ya hotuba kama ile ya mbayuwayu!. Madokta ambao hawatarejea kazini baada ya hotuba ya kesho, chamoto watakiona!. Yaani watakiona kisa cha mtema kuni, kilichomnyoa kanga manyoya!.

Naisubiri kesho kwa hamu kumsikiliza rais wetu JK ambae ili nijue nitaongeza post kwenye thread ya mazuri yake au mabaya yake!.

wewe ni wale wale wenye mawazo mgando ya wazee wa kale wa ccm...alishindwa nini kuwapa chamoto walipogoma mara ya kwanza? akijifanya kuleta uswahili wake na vizee vyake vilivyochoka akili, ni yeye mwenyewe atakaye kiona cha moto...!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom