Rais Kikwete kutohutubia taifa mwisho wa mwezi Mei

Nahisi ameona hotuba yake angegusia na wale ndugu wa Tarime. ndio maana kaona mwezi upite huu. subirini ya mwezi huu juni:biggrin1:
 
duuh, kumbe Kikwete huwa anahutubia kila mwisho wa mwezi? Decoder yangu ya kichina nini? Mbona haijawahi kumuonyesha hata mwezi mmoja? I hope sija-miss kitu significant kwa ku-miss hotuba zake tangu awe Rahisi.
 
Salva,m-replace mkulu kwa kumpa air time babu wa Samunge! Then,tuhabarishe kwamba JK amepaliwa na kikombe cha babu so instead anaongea babu mwenyewe. Naamini atapata wasikilizaji mara 1,000,000 zaidi ya wangeomsikiliza JK.
 
Hana jipya, inaelekea hafikirii kufanya mengine mapya akili imesimama tangu MEI MOSI
 
kwa hiyo yaliyotokea tarime hayamuhusu??
rais kilaza kwa sasa anaogopa kivuli chake
 
JK-Mei.jpg

Rais muhuni huyu.
 
Anajua lazima angelazimika kusemea madongo ya CHADEMA kwa serikali yake, mauaji ya Tarime, hali ngumu ya maisha iliyo na majibu maana momba hajatoa pesa, magamba ya ccm yasiyobandukika ndani ya miezi mitatu, ........... sio kweli kwamba kayasema yote, kwani aliyasemea mambo ya Tarime hata kabla hayajatokea? Mei mosi alikuwa anaongea na wafanyakazi akazungumzia mishahara, kwani watanzania wote ni wafanyakazi za serikali? Sema anapata kigugumizi kuongelea mambo ambayo kwa kweli hana majibu na maswali yake.
 
Je,atahutubia bunge la bajeti 2011/12?....kama hapana,lini atazungumzia mafanikio(?)/matatizo ya mwaka wa fedha wa 2010/11?...lazima atupe mustakabali wa mwaka wa fedha,pia azungumzie ripoti ya PCCB,Nishati na mwelekeo wake,Chakula na bidhaa muhimu kama mafuta,ajali za barabarani,mfumo wa elimu(matokeo ya mitihani na migogoro ya vyuo vikuu),mwelekeo wa taifa kuhusu katiba mpya,ufanisi wa kambi ya upinzani bungeni,ufanisi wa CCM bungeni,ripoti ya matembezi yake wizara mbalimbali,maoni yake na msimamo wa Tanzania kuhusu Afrika ya kaskazini na mashariki ya kati,michezo i.e simba/taifa stars/U21 ETC......Tunataka kujua msimamo wake na serikali kwa ujumla kabla hatujaanza kuipitia bajeti.

Kijana wao Nape jana alidhubutu kutamka kuwa bajeti iliyoandaliwa itajibu kero zote, source TBC news jana usiku, inaweza kuwa sababu ya mkuu wa kaya kutozungumzia mambo ya bajeti? Ahadi zake zinatekelezeka? Huyo kaogopa hana cha kudanganya tena kwa hotuba zake.
 
Mheshimiwa Mtukufu Rais wa JMT, umetumia haki yako ya msingi. Unaweza kuongea au kutoongea. Ni vizuri umeamua kutoongea maana kuna vitu vingi watu wangependa kusikia msimamo wako kama vile:
  1. Malipo kutoka BAE
  2. Kwanini wahisani wamesusa kuchangia bajeti ya 2010/2011
  3. Mauaji na Unyanyasaji wa raia na polisi wako (Nyamongo na Tabora)
  4. Msimamo wako kuhusu Libya na NATO
  5. Ubadhirifu wa fedha za "Economic Recovery" walizopewa mabenki wakati hakuna hasara
  6. Hali ya miundo mbinu nchini
  7. Maendeleo ya utekeleza wa ahadi zako kwa wananchi wakati wa kampeni
  8. Manung'uniko ya watu wa Arusha kuwa unawakomoa na ndiyo maana mikutano unahamishia Dar.
  9. Ripoti ya Ufisadi iliyotolewa hivi karibuni
  10. Ugumu wa maisha uliyosababishwa kwa kupanda kwa gharama za vitu mbalimbali pamoja na huduma za jamii. (bei ya mafuta, gesi, umeme, nafaka, nk)
  11. n.k.
 
Nia aibu Rais wa nchi kukosa la kuongelea baada ya siku 30 kupita..ina maana hakuna baya au zuri serikali yake inalolifanya..?!
 
Mauaji ya polisi Nyamongo;Pamoja na kuvuja kwa taarifa kuwa watu wale walipigwa risasi kutoka nyuma wakikimbia ambayo ni kinyume cha sheria ( Force law) Rais hana cha kuwaambia watanzania. Huyu ndiye rais wetu. Kwangu mimi 2015 ni kama bado miaka 10.
 
Mambo ya kusema yapo mengi angeweza:
  1. Kuwapongeza Watanzania kwa uvumilivu wao yaani wameishi kwa utulivu na kwa kufuata sheria za nchi japo maisha ni magumu mnoo.
  2. Angeomba msamaha kwa shirika la serikali TANESCO kuwaletea wananchi umasikini mkubwa kwani wengi wamefunga shughuri zao baada ya kushindwa kufanya kazi kwa kukosa umeme saloon, viwanda na workshops ndogondogo za wajasiliamali.
  3. Angezungumzia japo kidogo kashifa inayovuma ya mgodi wa Barlick kule Mara
  4. Angefafanua kidogo ahadi aliyoitoa kwa wafanyakazi siku ya mei mosi kuwa ataongeza mshahara au la maana aliweka kauli yake kimafumbo na wafanyakazi wengi hawajaelewa kama kuna ongezeko la mshahara au la
  5. Kuna kupanda kwa bei ya mafuta hadi leo kuna sehemu mafuta ni Tsh 2300/= na inazidi kupanda mwisho wake nini juhudi gani zinafanywa na serikali kudhibiti bei maana inaweza kufika Tsh 5000/= lita kama hakuna juhudi za makusudi kudhibiti.
YAPO MENGI MENGINE WANA JF ONGEZEENI.

 
Is it true kwamba jicho la mbuni ni kubwa in size kuliko ubongo wake? Uko wapi ule msemo wa mbuni kufukia kichwa mchangani akifikiri amejikinga na dhahma kumbe mwili mzima nje nje!
 
Back
Top Bottom