Rais Kikwete kutohutubia taifa mwisho wa mwezi Mei

Bado anaomboleza


Walinzi wake wasio onekana wamemkimbia baada ya mmiliki wake kuondoka, hilo moja!
Pili, kwani zile speech za kwenye semina elekezi alikuwa anahutubia Taifa? Huu sasa usanii.
Tatu naona ameishiwa hoja anasubiri kituko kingine kitokee ndo apate point za kuzungumza!
 
I really hate this oxymoronic "Directorate of Presidential Communications" what the heck is that? Rais akiwasiliana na mke wake hawa kurugenzi wanasimamia? Hivi kuna ugumu gani kuita Idara ya Mawasiliano Ikulu - Statehouse Department of Communication? Na kama wanaandika taarifa yao kwa Kiswahili kwanini wasitumiea letterhead ya Kiswahili vile vile?
 
Hivi great thinking ni kutukana? Huhitaji kufikri ili kutukana leteni hoja hata Kama ni ya kupinga. Aidha upinzani siyo kupinga kila kitu.
 
Aibu aibu!! Kwa ofisi kubwa kama ikulu, mahali patakatifu (kama baba wa taifa alivyozoea kupaita) kufanya makosa....."letter head" ni ya kiingereza...wakati barua ni ya "kiswahili"

hiyo ni aibu "salva" jamani...mnafanya rais wetu (handsome boy) aonekane "bogus"
 
JK-Mei.jpg
Hivi mei mosi ilikuwa tarehe ngapi?
 
mbona kuna matukio yaliyotokea baada ya mei mosi ambayo alitakiwa kuyatolea msimamo, mfano mauaji ya nyamongo, kifo cha shehe yahaya, ajali za barabarani, kumbukumbu ya mv bukoba nk
 
Nashukuru amegundua wengi wetu tunamsikiliza kama comedian asiye na dhamira wala lengo la hotuba zenyewe kwa watanzania na tanzania. Wanaomtayarishia pia wako out of touch na reality ya watanzania na tanzania.

Si ajabu Ikulu ni wadeni wa TBC. Asitishe kabisa hotuba za kipuuzi. Ebu tujiulize kama kuna hotuba iliyoleta tija.

Anaogopa kugusia maswala lakujivua magamba,mauaji ya Tarime na vitendo vya utumiaji nguvu kwa vyombo vya dola dhidi ya raia,matatizo ya umeme,ugumu wa maisha.Kero ambazo zinaongoza katika chat na CCM,JK na serekali yake "HAINA MAJIBU KWA KERO HIZI"ambazo ni jinamizi kwa chama tawala.Kuandaa hotuba bila kuzitaja kelo hizi haiwezekani.Hivyo ameamua kukwepa kuzungumzia mambo hayo kwa mtindo huo.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
I really hate this oxymoronic "Directorate of Presidential Communications" what the heck is that? Rais akiwasiliana na mke wake hawa kurugenzi wanasimamia? Hivi kuna ugumu gani kuita Idara ya Mawasiliano Ikulu - Statehouse Department of Communication? Na kama wanaandika taarifa yao kwa Kiswahili kwanini wasitumiea letterhead ya Kiswahili vile vile?

Mwanakijiji umefanya nichanganyikiwe kidogo; maana kumbukumbu zangu zinanikumbusha kuwa kuna wakati wanajiita Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu! kama nitakuwa nimekumbuka vyema basi yawezekana Salva amepitiwa katika kutengeneza neno la kiingereza "Directorate of Presidential Communication" au la like la kiswahili ndilo uwa linakosewa!

hii system ya Mafisadi na Mafya wa unga inachanganya sana zamani kulikuwa na Msaidizi wa Rais Hotuba! ambaye alikuwa mtumishi wa Ikulu, sasa sijui ndio nafasi iliyokuja kuitwa Directiorate of Presidential communications!?

Ila mambo aliyofanya Kikwete yamedhiirisha kuwa Tanzania haina ulinzi wowote na mtu akiingia madaraka anaweza kufanya lolote ambalo kichwa chake kitamtuma na bado dola ikamlinda na kumpigia salute siku zikasonga mbele.
 
I really hate this oxymoronic "Directorate of Presidential Communications" what the heck is that? Rais akiwasiliana na mke wake hawa kurugenzi wanasimamia? Hivi kuna ugumu gani kuita Idara ya Mawasiliano Ikulu - Statehouse Department of Communication? Na kama wanaandika taarifa yao kwa Kiswahili kwanini wasitumiea letterhead ya Kiswahili vile vile?

Tangu uzaliwe kuna kitu kuhusu JK umewahi kupenda? Nadhani unajua huwezi hata kutingisha upepo coward.
 
RAIS KIKWETE HATAHUTUBIA TAIFA MWEZI HUU, SABABU NI KWAMBA MAMBO MENGI AMEKWISHAYAONGEA KWA WANANCHI IKIWA PAMOJA NA HOTUBA YA MEI MOSI.

SOURCE: TBC1 Habari ya saa2 usiku

Ieleweke kwamba: Rais Kikwete hatahutubia Taifa mwezi huu, sababu kukwepa kuzungumzia mauaji mengi yaliyofanya na serikali dhidi wananchi hasa kule Tarime. Amechagua lawama badala ya kufedheheka.
 
Kazi kweli kweli....
Nilishasahau kama jana ilikuwa siku ya hotuba ya "mkuu"
Miongoni mwa hoja wajumbe waliokuwa wana-challenge sana huu utaratibu
wa kuhutubia kila mwisho wa mwezi ilikuwa ni hichi kinachoelezwa leo na "Kuregenzi ya Ikulu"..
Hamna sababu ya Rais kujibana eti mwisho wa mwezi lazima nipige stori na watu wangu...... kama hauna stori?? Ndio matokeo yake!
Kwa kiasi kikubwa watu wakiunganisha mtiririko wa matukio wanazidi kumuona rais wao kaishiwa, na hii ni mbaya sana kwa imani ya watu kwa rais wao.
Poor Jeykey!
 
Mambo yake anayoyazungumza siku ya kawaida sana labda atafute mengine ingawa najua ni mtihani kwake. Kiufupi hana jipya zaidi ya kulialia. Ingepeneza heading ingekuwa Rais kutolialia mwezi huu maana mlinzi wake ameondoka anaweza akaanguka.
 
Mhhh ni kweli mheshimiwa Rais hana kitu cha kuzungumza? Nini kimetokea tena? Yaani ya baada ya mei mosi hakuna lililotokea kubwa linalohitaji tamko? Basi atuambie hata semina elekezi japo haikuwa na bajeti iligharimu kiasi gani na nyamongo na rada basi
 
Atakae sikiliza hizo pumba atoe summary na mimi nasubiri atasema anakwenda Omar for good na sisi tufanye uchaguzi wa haki na amani yetu. This will be great day for Tanzanians.

"Warning:Lost man turn your tv off"
 
Je,atahutubia bunge la bajeti 2011/12?....kama hapana,lini atazungumzia mafanikio(?)/matatizo ya mwaka wa fedha wa 2010/11?...lazima atupe mustakabali wa mwaka wa fedha,pia azungumzie ripoti ya PCCB,Nishati na mwelekeo wake,Chakula na bidhaa muhimu kama mafuta,ajali za barabarani,mfumo wa elimu(matokeo ya mitihani na migogoro ya vyuo vikuu),mwelekeo wa taifa kuhusu katiba mpya,ufanisi wa kambi ya upinzani bungeni,ufanisi wa CCM bungeni,ripoti ya matembezi yake wizara mbalimbali,maoni yake na msimamo wa Tanzania kuhusu Afrika ya kaskazini na mashariki ya kati,michezo i.e simba/taifa stars/U21 ETC......Tunataka kujua msimamo wake na serikali kwa ujumla kabla hatujaanza kuipitia bajeti.
 
Maskini JK, hajui hata madhumuni ya Hotuba za mwisho wa mwezi kwa wananchi. Mbona Mzee Mkapa alieanzisha utaratibu huo hakuwahi kuishiwa cha kusema hata pale alipokuwa amebanwa na majukumu ya kimataifa?

Aache kuigaiga mambo ambayo hana ubavu wa kuyaendeleza....!!!!
 
Back
Top Bottom