Rais Kikwete kuongoza maziko ya Regia Mtema!

Hivi kwa nini msiba wa familia ya Mzee Mtema lakini air time, credit mnampa Jk eti mara kahudhuria maombolezo, mara Jk ataongoza mazishi, yaani msiba wa familia wanasiasa wana run the show? Halafu watu mnampa pongezi rais kwa vitu vidogo kabisa kama kuhudhuria misiba? Kuhudhuria msiba ni kitu rahisi sana, na kwa majukukumu ya rais asipohudhuria wala hatutaanza kumhukumu hapa kama antisocial au vinginevyo. Tulishawahi kuwa na marais huko nyuma, lakini mi nashangaa rais wa mara hii pongezi zake ni kwenye kuhudhuria misiba..

Na kuna mwingine anasema damned if you do and damned if you don't. Hujaelewa bado. Ni kwamba anadamniwa kwa yale yaliyompeleka Ikulu. Si kwa kutohudhuria misiba. Ina maana rais atahudhuria misiba mingapi na kila siku watu wanakufa? Ni kweli huu ni msiba mzito wa kitaifa na Jk atafanya vizuri kuhudhuria, lakini si jambo la kipekee kuhudhuria kwake pale.
 
wana JF mnisamehe kama ninawatia uchungu kwani hata mimi nampenda sana Regia. Kwa nini aliendesha gari lisilokuwa equipped kwake? Mnisamehe kuingiza swali muhimu wengi hawataki kulisikia lakini wengi wao walipenda kumuona Regia mmbunge wa Kilombero. Alikosea kumuacha dreva kama nasi tunavyokosa kwenye mambo mengi ya mwili na roho. Tumuombee Regia lakini kama mkristu makini tuwaonye wabunge wote wasiendeshe kasi na tuombe wabunge wenye ulemavu wapewe magari maalum
 
Duh yaani watu wengine mmezidi unazi hadi mnaboa, hata kama mna tofauti zenu na Kikwete kumbukeni huu ni msiba ambao umewakumba Watanzania wote na si Chadema pekee. Sioni tatizo lolote kwa JK kushiriki.
 
So then whats your point "Hahudhurii kila msiba!"?
Hivi na wewe mbona utumii common sence zako? ni binadamu gani mwenye uwezo wa kuhudhuria kila msiba? unajuwa kwa siku moja Tanzania nzima kuna misiba mingapi? what is the meaning of Great Thinkers?
 
Wanabodi,
Tuendelee kupeana pole kwa msiba huu wa Regia, Rais Jakaya Kikwete, atawaongoza umma wa Watanzania katika maziko ya mpendwa na shujaa wetu Regia Mtema yatakayofanyika Ifakara siku ya Jumatano.

Kwa mujibu wa ratiba ya ziara ya rais Kikwete mkoani Morogoro, ratiba hiyo inaonyesha rais Kikwete atahudhuria maziko hayo siku ya Jumatano.

acha kupotosha umma, ataudhuria tu anayeongoza mazishi ni mwenyekiti wa chama chake!
 
Back
Top Bottom