Rais Kikwete kukutana na wabunge wa CCM leo hii

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
kuna tetesi kuwa rais kikwete atakutana na wabunge wa ccm leo hii kabla ya saa kumi na moja jioni.bado sijapata taarifa kwamba kikao hicho ni shinikizo la wabunge au la.najitahidi kutafuta info zaidi nikifanikiwa nitatoa updates.
 
ni sehemu ya kuweka mambo sawa,, urais ndy huo unapokutana na changamoto uoneshe ukomavu wako wa kukabiliana nazo
 
Ni sahihi anajaribu kuwarudisha wabunge wa ccm waliomeguka kutaka kuididimiza serikali yake; mtoto w mkulima yamemshinda
 
Badala akakutane na madr waliogoma kwanza yeye anaenda kuktana na wabunge....au kipaumbele chake ni kipi
 
Badala akakutane na madr waliogoma kwanza yeye anaenda kuktana na wabunge....au kipaumbele chake ni kipi

Hujuwi kuwa matatizo ya madaktari uchwara yanashughulikiwa na kamati ya bunge? magwanda wakiwemo.

Kama ni kweli akimaliza kukutana na wabunge wa CCM basi atakutana na wa magwanda, hapo ndipo Kikwete anapojuwa kuwapatia, juisi na kashata kidogo, kusuta kote hakuna. Kama watoto wadogo vile.
 
Ndio maana wabunge wa CCM leo walitangaziwa bungeni wasizime simu zao na wasiende mbali maana wanaweza wakahitajika wakati wowote.Tunasubiri kitakachojiri.
 
kikwete bado hajatambua kuwa yeye ndiye rais wa TZ anababaika sana hana maamumzi nchi ya wadanganyika imemshinda kuongoza hata akikutana na wabunge wake hana ubavu ninafikiri 2014 ndipo atatambua nafasi yake poleni watanzania nawahurumia sana
 
Hata bia zimepanda bei, nawashauri walevi wenzangu tugomee na sisi iwe "glass down"
 
Hujuwi kuwa matatizo ya madaktari uchwara yanashughulikiwa na kamati ya bunge? magwanda wakiwemo.

Kama ni kweli akimaliza kukutana na wabunge wa CCM basi atakutana na wa magwanda, hapo ndipo Kikwete anapojuwa kuwapatia, juisi na kashata kidogo, kusuta kote hakuna. Kama watoto wadogo vile.

Angalia maneno yako, ukiugua ujue pa kwenda Pambaf we.!!!
 
Back
Top Bottom