Rais Kikwete kukacha uzinduzi wa chanjo Arusha?

Wakuu leo tarehe 12 / 11 / 2011 Rais wa JMT Mheshimiwa J Kikwete anatarajiwa kuzindua chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano.Chanjo hiyo itahusisha magonjwa ya Polio,Surua,Vitamini A na dawa za minyoo.

Taarifa za kiintelijensia toka chanzo muhimu zinasema uenda Mheshimiwa Rais Kikwete atashindwa kuzindua kampeni hizo kwasababu za kiusalama mkoa Arusha.Taarifa nyingine za uhakika kuna mpango wa kile chama cha magwanda kuvuruga zoezi zima la uzinduzi kwa kubeba mabango yenye nia ya kumdhalilisha mkuu wa Kaaya eg:Mfungulie mbunge wetu,Ondoka na meya wako wa kuchonga na nk.

wewe unahamisha kutoka kichwani mwako unachokifikiria na kukifanya kuwa mawazo ya wengine? Rais Kikwete anapendwa na watanzania siyo kama unavyofikiria wewe.
 
wewe umeishiwa hoja kama usalama wa taifa wako binafsi wamekudanganya hivyo unajidanganya. chadema wamedhibitiwa Arusha kiasi kwamba kulala uwanjani kwa siku sabu walizotangaza awali walishindwa unashangaza sana na habari za njozi

Mkuu,
Jambo usilolijua ni bora ukakaa kimya!
Nimepita uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta hapa Arusha sasahivi na niliingia uwanjani. Ni aibu tupu. Uzinduzi unaoitwa wa kitaifa hauna watu wanaofika 500 na 80% ni watoto wa sekondari ambao hata chanjo yenyewe haiwahusu!? Sijui tbc1 wataonesha nini! Niaibu sana maana licha ya magari ya matangazo kutangaza kwamba JK ndiye angekuwa mgeni rasmi lakini hali ndio hiyo..
Amka mkuu, tz hii sio ile ya mwaka jana na mwaka juzi!
 
Wamkaribishe Rais wetu tuliyempigia kura Dr Slaa, ambaye kiravu alimchakuchulia kura akishirikiana na system.
 
Ni aibu kwa rais kutokwenda Arusha kisa tu wananchi wananchi watampokea na mabango ya kashfa.
 
Wakuu leo tarehe 12 / 11 / 2011 Rais wa JMT Mheshimiwa J Kikwete anatarajiwa kuzindua chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano.Chanjo hiyo itahusisha magonjwa ya Polio,Surua,Vitamini A na dawa za minyoo.

Taarifa za kiintelijensia toka chanzo muhimu zinasema uenda Mheshimiwa Rais Kikwete atashindwa kuzindua kampeni hizo kwasababu za kiusalama mkoa Arusha.Taarifa nyingine za uhakika kuna mpango wa kile chama cha magwanda kuvuruga zoezi zima la uzinduzi kwa kubeba mabango yenye nia ya kumdhalilisha mkuu wa Kaaya eg:Mfungulie mbunge wetu,Ondoka na meya wako wa kuchonga na nk.

Jambo Mkuu, Si rahisi kama unavyodhani aisee......"Raisi wa Nchi"???
 
Jiandaeni kwa kumficha, maana sasa hata mkisema ni cdm hakuna anayewaelewa na uzushi wenu!
 
Mkuu taarifa za kiintelijensia anakwenda Iringa.mbeya akafanye nini nasikia wanataka mkoa wao uhamishiwe Zambia.

hahahaha kikwe te anakazi ya kuwaunganisha watanzania sasa na huko mbeya sijui kuna lema..
 
Wabara,

Usipate taabu kubisha jambo usilolijua.Mkutano yote ya kimataifa tuliyozoea kuona ikifanyika Arusha siku hizi haifanyiki imefika mahali hata mikutano ya EAC inapelekwa Dar usisahau Arusha ni makao makuu ya EAC.

Mkuu wangu mimi si mshabiki wa CDM kama unavyofikiria wakikosea jambo nawatwanga bila kificho tafuta mabandiko yangu yamkini utajua unabishana na mtu wa namna gani.

pale Arusha vyombo vya usalama viliwadhibiti chadema hata wakati Rais hayupo Arusha ndio unathubutu kutudanganya kwamba vyombo hivyo hivyo vitashindwa kuwadhibiti wakati Rais yupo Arusha wakati kwa uhakika ulinzi ndio utakuwa mkali maradufu.... huo ni uongo
 
wewe unahamisha kutoka kichwani mwako unachokifikiria na kukifanya kuwa mawazo ya wengine? Rais Kikwete anapendwa na watanzania siyo kama unavyofikiria wewe.

anapendwa labda wale wanae mnunulia suti na watu wa pwani..
 
Mkuu wangu Hauxtable.

Kikwete haipendi Arusha fuatilia hotuba yake ya Dodoma utajua jinsi alivyoizungumzia.Ipo thread hapo nadhani ilianzishwa na Philemoni itafute utapata mambo mengi angekuwa na uwezo angehamishia makao makuu ya EAC Bagamoyo.

Jambo Mkuu, Si rahisi kama unavyodhani aisee......"Raisi wa Nchi"???
 
Mkuu wangu Hauxtable.

Kikwete haipendi Arusha fuatilia hotuba yake ya Dodoma utajua jinsi alivyoizungumzia.Ipo thread hapo nadhani ilianzishwa na Philemoni itafute utapata mambo mengi angekuwa na uwezo angehamishia makao makuu ya EAC Bagamoyo.

haipendi arusha hata sisi hatumpendi ahamishie kila kitu pwani kama anajeuri..
 
Nimebahatika kusoma Memo ya mkurugenzi wa TANAPA ikiwahimiza wafanyakazi kuhudhuria uzinduzi wa chanjo kwa wafanyakazi wote bila kukosa,Mamlaka ya maji safi Arusha mambo ni kulazimishana hakuna hiyari.Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wamesombwa kwa fujo nakuna na wengine wanatia huruma njaa na kiu ya maji zimewakamata kisawa sawa.

Dr Bilali kakimbilia Kibo palace kupata msosi wanafunzi wanateseka,namshukuru Mungu mwanangu hasomi hizi shule za kina Kayumba.
 
Back
Top Bottom