Rais Kikwete kukacha uzinduzi wa chanjo Arusha?

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,921
31,161
Wakuu leo tarehe 12 / 11 / 2011 Rais wa JMT Mheshimiwa J Kikwete anatarajiwa kuzindua chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano.Chanjo hiyo itahusisha magonjwa ya Polio,Surua,Vitamini A na dawa za minyoo.

Taarifa za kiintelijensia toka chanzo muhimu zinasema uenda Mheshimiwa Rais Kikwete atashindwa kuzindua kampeni hizo kwasababu za kiusalama mkoa Arusha.Taarifa nyingine za uhakika kuna mpango wa kile chama cha magwanda kuvuruga zoezi zima la uzinduzi kwa kubeba mabango yenye nia ya kumdhalilisha mkuu wa Kaaya eg:Mfungulie mbunge wetu,Ondoka na meya wako wa kuchonga na nk.
 
Raisi anapoanza kuogopa maeneo yake ya utawala kwa kuhofia defamation (hakuna cha mabango ya magwanda wala intelijensia hapo)..... no one can predict tomorrow
 
Ngongo,
Kwa taarifa nilizozipata hata mimi ni kwamba Kikwete ameingia mitini. Na sababu pekee ni woga. Anaogopa wananchi maana sio wapiga kura wake. Aliteuliwa na Usalama wa taifa na kutangazwa na Nec bila ridhaa ya wananchi. Na wakazi wa Arusha wanalijua hilo na wanalipinga kwa nguvu zote. Polisi ndio wanaomsaidia tu, otherwise angekuwa msoga anacheza draft.

Na kwa taarifa hizo hizo za kiintelijensia, hakuna kiongozi wa juu wa chama wala serikali mwenye udhubutu wa kutia mguu Arusha. Wataishia hukohuko. Kama unabisha muulize Nape ni kwanini aliishia stendi ya Moshi? Jibu ni lilelile, woga!

Kiongozi anapokosa ridhaa ya wananchi, anakosa confidence ya kusimama mbele yao na kuishia kutoa amri na maelekezo kutoka ikulu. Mimi naamini siku polisi wakichoka, tutaikomboa nchi kwa staili ya Misri!
 
Kuh Lema Bash:Wana Arusha tukumbusheni party ya kumpokea mpiganaji Lema mahali na muda. Viva Lema illustrious son of TZ.
 
Kulikuwa na thread inazungumzia kutokuja kwa JK hapa A-town. Vizuri kuanza kuwa mwoga wa kufika maeneo ambayo unajua kabisa hawakuungi mkono katika yako uongozi wako.
 
mkuu hata kabla polisi hawajachoka,uwezekano wa kuikomboa nchi kama misri na kwingineko upo,maana hali ya nchi imekuwa tete na ccm na mafisadi wao wanalijua hilo,tunaendelea kujiandaa kwa kuunganisha nguvu ya umma kwa kuelimisha elimu ya uraia na kwa wananchi kutambua haki zao na kisha kuzidai.
 
wewe umeishiwa hoja kama usalama wa taifa wako binafsi wamekudanganya hivyo unajidanganya. chadema wamedhibitiwa Arusha kiasi kwamba kulala uwanjani kwa siku sabu walizotangaza awali walishindwa unashangaza sana na habari za njozi
 
Kama ni kweli rais anaogopa kwenda Arusha sababu ya CHADEMA basi hali si shwari.
 
kama kikwete hatakwenda Arusha basi atakuwa na ratiba ingine Arusha ni tulivu kwa sisi tuliopo Arusha chadema wamedhibitiwa hata mbowe alikosa watu wa kumshangilia alipojisalimisha na kuachia. Polisi wanafanya kazi yao vema kwa watu wanaotaka kuvuruga Arusha yetu kwa sababu za kisiasa
 
aje A town kufanya nin kwn haogop leo hii anakuja iringa anaziara iringa vijijin ningependa kinuke ka mbeya nako tuone akifika atasema nini
 
sidhani kama JK anaweza kuogopa mabango ya kumdhalilisha basi atakuwa sio mwanasiasa aliyekomaa. mabongo ni ujumbe wa wananchi kwa rais wao hawezi kuogopa. mabango yanatumika sana katika nchi za magharibi ni jambo la kawiaida ila jamaa anataka tu kulikuza
 
Wakuu leo tarehe 12 / 11 / 2011 Rais wa JMT Mheshimiwa J Kikwete anatarajiwa kuzindua chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano.Chanjo hiyo itahusisha magonjwa ya Polio,Surua,Vitamini A na dawa za minyoo.

Taarifa za kiintelijensia toka chanzo muhimu zinasema uenda Mheshimiwa Rais Kikwete atashindwa kuzindua kampeni hizo kwasababu za kiusalama mkoa Arusha.Taarifa nyingine za uhakika kuna mpango wa kile chama cha magwanda kuvuruga zoezi zima la uzinduzi kwa kubeba mabango yenye nia ya kumdhalilisha mkuu wa Kaaya eg:Mfungulie mbunge wetu,Ondoka na meya wako wa kuchonga na nk.

anakwenda Mbeya
 
pale Arusha vyombo vya usalama viliwadhibiti chadema hata wakati Rais hayupo Arusha ndio unathubutu kutudanganya kwamba vyombo hivyo hivyo vitashindwa kuwadhibiti wakati Rais yupo Arusha wakati kwa uhakika ulinzi ndio utakuwa mkali maradufu.... huo ni uongo
 
Kuingia kwake miti tulilijadili tangu jana hapa.....Anabahati kachomoa na kuhusiana na ujumbe kama ulivyoainisha hao juu ni kweli.............
 
pale Arusha vyombo vya usalama viliwadhibiti chadema hata wakati Rais hayupo Arusha ndio unathubutu kutudanganya kwamba vyombo hivyo hivyo vitashindwa kuwadhibiti wakati Rais yupo Arusha wakati kwa uhakika ulinzi ndio utakuwa mkali maradufu.... huo ni uongo
Tuambie kwanini hajaja kama alivyo ahidi mpaka jana saa tano...
 
Back
Top Bottom