Rais Kikwete kuhutubia wakazi wa Dar mchana huu Mchikichini, Ilala

Hotuba za nini saa hizi...atoe misaada inatosha...

Sio misaada. Ni jukumu la serikali kuwatunza na kuhakikisha raia wake wanakua salama. Hivyo hapa serikali inapaswa kutimiza majukumu yake tulioipa kwa kuichagua kwa kura.
 
Anna Tibaijuka alipotaka kuwaondoa watu wa mabondeni Zungu yule bunge wa Ilala alipiga kelele hadi bungeni na kumtishia mama kwamba atapambana naye hadi mwisho lakini hatumsikii akisema haya maafa.
 
Anna Tibaijuka alipotaka kuwaondoa watu wa mabondeni Zungu yule bunge wa Ilala alipiga kelele hadi bungeni na kumtishia mama kwamba atapambana naye hadi mwisho lakini hatumsikii akisema haya maafa.

Kama zungu alimtishia Tibaijuka naye akaufyata, hapo ni kusema aliyemteua Tibaijuka naye alikubali kutishwa na akatishika.

Kama asingetishika, angemuambia Tibaijuka aendelee na majukumu yake ilimradi anafuata sheria. Na huyu zungu ni mbunge wa ccm, inawezekana kweli mbunge anamzidi nguvu raisi ambaye ni mwenyekiti wake!?
 
Ni Rais asiyekuwa makini.
Kumbuka kulitokea wafanyakazi wa mgodi kuangukiwa na kifusi nchi Mexico,Rais wa nchi hile alijumuika na waokoaji muda wote pale kwenye mgodi.
Lakini Rais wetu hupo Ikulu nakunywa kahawa ,kasubi maji yamepungua heti anazunguka na helikopta.Katoa msaada gani kwa wananchi wake?
Jana alikuwa wapi?

Rais wetu apendi kupata shida wala karaha na watu wake ,Ongera Rais kwa hilo we kaa Ikulu
kwanini asiutubie Jangwani ?

Kwa jinsi inavyoonesha hata jangwani kwnye hupajui ww!!!
 
Kwanini iwe wrong move? Unaelewa maana ya kufarijiwa? Imagine ni wewe umepata tatizo...halfu RAIS wa nchi anakuja kukupa pole..utajisikiaje? Kuna faraja unayoweza kupata zaidi ya hiyo?

Mwanzo nilidhani ni wanawake tu ndio wanadanganywa kwa maneno, kumbe si hivyo bali ni kila mwenye akili za kike. Sasa wewe ndugu yangu, maneno yanawezaje kukupa faraja kwa nyumba yako ambayo imekwenda na maji?

Kumbe kushikwa mkono na Rais ni dili, mwee! Kweli udhaifu ugonjwa mbaya. Mimi binafsi sioni utukufu wowote ktk hilo kwa sbb HE IS NOT THAT MUCH SUCCESSFUL. Tena nikikumbuka kuwa juzi tu hapa katoka kuchagua Mabalozi kwa faida yake, hata hamu naye sina.

Wahi baba ukapate faraja. Wengine sisi pole na ngonjera tumezizoea kwa kuwa tunaambiwa kila siku na wake zetu tunaporudi kwenye mihangaiko yetu.
 
Hivi wale wazamiaji toka South Africa hawajaitwa kutoa msaada wa kuokoa safari hii?
 
Kikwete ndiye raisi wa nchi, ndiye serikali yake inakusanya kodi zetu, ndiye ameapa na anawajibika kikatiba na kisheria kusimamia na kulinda maisha ya watanzania, kwahiyo alitakiwa kuwa wa kwanza kufika maeneo yenye mafuriko kujionea hali halisi ili aweze kuchukua hatua stahiki.Ajabu ni kwamba alikuwa amejifungia magogoni huku na yeye akiungana nasi kutoa pole kupitia facebook, sasa sijui kama raisi anatambua kwamba hao wananchi waliokumbwa na mafuriko wana access na mtandao.

Kwa taarifa, mwenyekiti wa Bavicha bw. Heche alikuwepo kigogo akisaidiana na wananchi kuwapa msaada waathirika wa mafuriko na hakuitaji camera ili auze sura kama iddi azani mbunge mzima anashindwa kutoa msaada na kuishia kuitupia lawama serikali yake legelege, ili tu auze nyago kwenye tv!Sasa raisi anasubiri maji yamekwisha na wananchi wamejitolea usiku kucha na mchana kutwa ndipo leo anakumbuka kuzunguka na chopa, then anakwenda kuwahutubia mchikichini, hii ni aibu kwa kiongozi wa nchi kushindwa kutambua wajibu wake on the spot, hadi watu wapige kelele kwenye mitandao ndipo anakumbuka wajibu wake.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) ilitoa tahadhari mapema miezi zaidi ya minne iliyopita kwamba kutakuwa na mvua kubwa sana mwishoni mwa mwaka lakini serikali haikuchukua hatua yoyote ya kujiandaa kukabiliana na madhara ya mafuriko, sasa watu wamepoteza maisha ili wapate nafasi ya kujinufaisha,tunakumbuka walivyojinufaisha wakati wa milipuko ya mbagala na gongolamboto, ambapo hadi leo hii wananchi wale hawakulipwa stahili zao na wengine wanaishi nje hadi sasa kama wanyama.
 
Kwa ninavyomjua rais wetu kwa upendo, hawa woote waliokosa mahala pa kuishi atawapa post za ubalozi kama alivyofanya kwa wale waliokumbwa na janga la kukataliwa na wananchi kwenye uchaguzi. Wakifika huko wakajifyatulie mahekalu km alivyofanya Mh.Mahalu kule kwa 'Bele-sokoni'. Tumpongeze kwa hili la kuwajali wenye shida kwa kweli
 
Hivi wale wazamiaji toka South Africa hawajaitwa kutoa msaada wa kuokoa safari hii?

Now that you mention that kaneno wazamiaji, nimekumbuka kitu. Juzi juzi hapa kwenye taarifa ya habari tuliambiwa kuwa wazamiaji haramu kutoka Somalia wamekamatwa Arusha. Kwa nini serikali hii inakosa ubunifu wa kuwatumia kuzamia tunapopatwa na majanga badala yake tunaishia kuwafungulia mashtaka heroes hawa?

Ni suala la kuwa-dis'haramu na kuwatunza vyema for fyucha yuz. Wadau wa mikakati mnasemaje?
 
Back
Top Bottom