Rais Kikwete jivue aibu jee (TAKUKURU) ina kazi gani?

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482


Christopher Nyenyembe

UAMUZI wa Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuridhia ombi la Rais Jakaya Kikwete la kutaka kuwawajibisha na kuwafuta uwaziri, mawaziri wanaotuhumiwa ama kujilimbikizia mali za umma, kushindwa kusimamia vema wizara zao na kuliingizia taifa hasara ya mabilioni ya fedha, si wa kishujaa.
Nasema uamuzi uliofikiwa juzi na CC ya CCM haujalenga kutibu tatizo hilo mapema licha ya kuwepo kwa taarifa nyingi zilizokuwa zikitolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwa serikali inaelemewa na matumizi mabaya ya fedha za umma lakini alikuwa hasikilizwi.
Nasema hasikilizwi kwa kuwa hata wabunge bila kujali itikadi za vyama vyao walieleza wazi kiburi kilichokuwa kikionyeshwa na serikali pale inaposhindwa kuwachukulia hatua mapema wale wote waliotuhumiwa kwa ufujaji wa fedha za umma, wengi waliendelea kutamba kuwa hawawezi kuguswa.
Hakukuwa na njia rahisi ya kuwawajibisha haraka watendaji wa serikali ilhali kila kitu kiliwekwa wazi na CAG na zile kamati tatu za Bunge nazo zilipiga kelele na kutoa taarifa zinazoonyesha namna mabilioni ya fedha za umma zinavyotafunwa na wateule wachache walioaminiwa na rais lakini wameamua kumsaliti.
Rais Kikwete alisalitiwa muda mrefu na baadhi ya timu ya mawaziri, manaibu mawaziri, makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi na mameneja wa mashirika ya umma kwa kuwa walijua fika kuwa uteuzi waliopewa bure ni zawadi kubwa itakayowasaidia kuteketeza fedha za umma.
Kwa kuwa hayo yametokea na leo Kamati Kuu ya CCM imekubali mawaziri hawa washughulikiwe bado kuna jambo kubwa ambalo bila kuliweka sawa rais yeyote ajae ataendelea kuipata aibu hii kwa kuwa si jambo la kujivunia mkuu wa nchi anapoaibishwa na wateule wake wasiokuwa waadilifu na waaminifu.
Tatizo hapa ni nini, tatizo kubwa linatokana na madaraka makubwa aliyopewa rais kwa mujibu wa katiba yetu mbovu tuliyonayo, inamfanya rais awe na kundi kubwa la wateule katika maeneo mbalimbali bila kujua hulka zao kama hawa ni wezi, wala rushwa au mafisadi waliokubuhu.
Hilo ni tatizo kwa kuwa hakuna tathmini ya kutosha inayofanywa na timu inayomshauri rais ili kujua tabia na maadili bora ya mtu anayepaswa kuteuliwa kuwa waziri, naibu waziri, katibu mkuu, mkurugenzi wa shirika la umma na nyadhifa tele ambazo kimamlaka rais amebebeshwa zigo hilo.
Haiwezekani rais huyo huyo ndiye anayeteua mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na wilaya, makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa mashirika ya umma, mabalozi na wengine akawa na ufanisi mkubwa wa kuwajua kikamilifu wale anaowapa nyadhifa.
Kwa mfumo huo ndio maana unamnyima meno waziri mkuu kutoonekana mtendaji mkuu wa serikali, kiongozi huyo yupo tu na hawezi kumwajibisha mteule yeyote aliyepewa wadhifa huo na rais na hapo ndipo aibu hii inayoonekana leo inapoangukia miguuuni mwa rais mwenyewe.Ipo haja mfumo wa kuteua watendaji wa umma katika nyadhifa na madaraka yao uangaliwe upya, kweli wapo wanaostahili kweli kuteuliwa na rais kwa maana ni muhimu sana rais kuteua mawaziri anaoona wanafaa kuisaidia serikali yake na hao wakivurunda mwenye fimbo ya kuwachapa hapo hapo ni rais mwenyewe.
Kwa maana hiyo itakuwa rahisi mkuu wa nchi kuwa na kundi dogo la viongozi wa juu serikalini wanaounda baraza la mawaziri kuwa karibu na rais na rais huyo huyo itakuwa kazi rahisi kwake kuweza kujua tabia na utendaji kazi wenye tija unaofanywa na wasaidizi wake.
Nyadhifa nyingine kama nilivyozitaja ambazo lazima rais afanye uteuzi huko kote ni kumdhalilisha kiongozi mkuu wa nchi inapotokea watu wanatafuna fedha za umma bila kuchukuliwa hatua haraka kwa kuwa mlolongo wa upelekaji wa taarifa hadi zimfikie rais na ili aweze kuchukua maamuzi tayari jahazi litakuwa limezama.
Ipo haja na hilo naliweka mbele ili liweze kuenenda na mabadiliko mapya ya Katiba ya nchi, umefika wakati ambao lazima watumishi wa umma wanaopaswa kushika nyadhifa nyingine wanapaswa kuomba na kudhibitishwa na Bunge ili iwe rahisi kupitia bunge mtendaji mkuu wa shughuli za serikali bungeni ambaye ni waziri mkuu awe na meno.
Haiwezekani tuhuma za ubadhirifu zinamhusu mkurugenzi wa shirika la umma na tuhuma zake zote zimethibitishwa na tume za Bunge na taarifa ya CAG kuwa mkurugenzi huyo hawezi kuchukuliwa hatua eti kwa sababu ameteuliwa na rais, huko kote kunasababisha urasimu wa madaraka na ulezi wa vitendo vya ufisadi usioweza kuliendeleza taifa hili.
Si jambo rahisi kuwa rais awafahamu fika wateule wake wote, bali anachotakiwa ni kuwajua kwa undani wakuu wa idara nyeti za serikali ambao watakuwa wanamsaidia katika shughuli za kila siku.
Mamlaka ya uteuzi yanapokuwa makubwa nyuma yake kunakuwa na kundi kubwa la wateule ambao wanapoboronga hushindwa kuwajibishwa kikamilifu na huishia kutamba kuwa hawawezi kufanywa chochote kwa kuwa rais ndiye aliyewapa nyadhifa husika.
Haiwezekani waziri mwenye dhamana na wizara ashindwe kumwajibisha naibu wake, au katibu wa wizara pale inapogundulika kuwa kwa pamoja wamekula njama za kuiba fedha za umma, kila mmoja anatamba kuwa kawekwa kwenye nafasi hiyo na rais ambaye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho wa kujua hatma ya wateule wake.
Mfumo huu ndio unaogharimu maendeleo ya nchi, ndio unaochangia kutoa mwanya kwa viongozi wa umma kufanya watakavyo. Kuna kila sababu ya kuangalia madaraka makubwa aliyonayo rais ya kuteua watendaji wa umma kwa nafasi zao.
Ili mambo yaende sawa utumishi wa umma usiwe na matakwa ya mtu mmoja ndio maana dhana ya kuwajibishana na kuwajibika umekuwa mzigo mzito usioweza kubebeka kiasi cha kuifanya nchi ifikie hapa ilipo sasa.
Ili uwe kiongozi mzuri lazima ukubali kuwa bilionea kwa muda mfupi huku watu wengi masikini wakizidi kuwa wanyonge na wanajitahidi kuwanyenyekea wateule wa rais hata kama wakifukuzwa kazi wanarudi na mabilioni yao mitaani na kuanza kugawa fedha hizo bure bure kwa lengo la kujisafisha.
Hii ni aibu na kwa vyovyote rais anapaswa kujiepusha nayo, hawa wanaochafua upepo mbaya serikalini hawawakomoi watu masikini kwa kusababisha utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi ziwe tatizo, wanaichafua zaidi serikali inayoonekana kushindwa kufanya kazi iliyoaminiwa na wananchi.
Kwa kuwa tatizo ni mfumo wa uteuzi na mfumo wa kupeana madaraka kinachotakiwa kufanywa upande wa pili wa shilingi ni kumuondolea rais madaraka makubwa ya kuteua watendaji wa umma, awe na ukomo kwa baadhi ya nyadhifa za watendaji wa serikali ili iwe rahisi kwa mamlaka nyingine kuweza kuwawajibisha.
Ipo haja nafasi ya waziri mkuu wa nchi ikaangaliwa upya, haipendezi kiongozi huyo anapokosa meno hata ya kumuuma naibu waziri, anaposhindwa kumng’oa madarakani mkurugenzi wa shirika la umma na wengineo wanaobainishwa wazi bungeni na ndani ya taarifa za CAG kuwa ni wezi, mafisadi au wametumia vibaya madaraka yao wanaangaliwa tu bungeni eti lazima rais abariki, hilo ni tatizo.
Ili haya yanayotokea leo yaweze kumuepusha rais na aibu hii ipo haja ya msingi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ikawa na mahakama yake maalumu inayoshughulikia wala rushwa kama zilivyo mahakama za ardhi, mahakama za kazi (upatanishi na usuluhishi) na mahakama za biashara, hapo hakika rais hawezi kukumbwa na aibu hizi zinazofanywa na wateule wake.


h.sep3.gif

cnyenyembe@yahoo.com 0754 301864, 0715 301864

 
Mkuu, c TAKUKURU tu.. Kuna kitu inaitwa EWURA... Kaka sijaiona faida ya hiyo kitu.. Mwaibula alikua poa,wakamtimua sasa SUMATRA.. Hao ndio hovyo kabisa.. Shotly Huyu jamaa ni Hovyo hana sifa ya kuliongoza Taifa bali wizara tu niyo ulikua uwezo wake....
 
Mimi naungano mkono mkuu na wale wenye kusema kuwa baada ya kungolewa mawaziri waliokula mabilion ya pesa za umma waburuzwe mahakamani, hii itakuwa ndio funzo kwa wengine ,bila ya hivyo basi itakuwa hawa wamedokowa wengine watakula kwa madonge.


Itakuwa ule msema usemao chukuwa chako mapema kabla mambo hayaja haribika, maana hukumu itakuwa ukicha kuiba mabilion utangolewa kuendelea na mradi mwingine ,hii sio dawa na ugonjwa itakuwa bado hatuja utibu?.

Vyombo vya mahkama vipo na kufikishwa huko ndio kujikocha kwao na kuachana na maneno yakusema pembeni kuwa wako wasafi na hawana kosa kwa hio huko ndiko watakako jieleza na kusibidisha mazingira gani ya upoteaji wa mamilioni ya pesa za umma.

Hivi sasa watanzania tumechanganyikiwa kutokana na ukali wa maisha hii ile katika familia ukiomwa na homa tu tafrani hujuwi pesa utapata wapi, wachilia ukali wa maisha, huku wanatokea wajanja wanaiba mamilioni ya fedha sisi bado tunaona azabu ni kuwavua madaraka tu.

Hii sio dawa wengina wanaweza kuiba mabilioni kwa kipindi kifupi tu ili kujiimarisha na mapema kabla ya kutolewa ni kula kwa matonge, inasikitisha kuona mtu anaondoka na mamilioni bila sheria kumkusa , huku tanzania ikiambiwa ni moja kati ya nchi maskini na fukara watu wake.

Jee rasilimali zetu zinakwenda wapi? Jee kweli tanzania ni maskili? Inasemekana kuwa viongozi wa tanzania wana utajiri mkubwa na rasilimali kuliko viongozi wa ulaya , ambao viongozi wetu wanakwenda kuomba katika nchi zao.

Nilazima wawajibishwe ki mahakama wezi wa mali za umma.
 
Tz tuna nchi yenye rutuba,siasa mbovu na uongozi ovyo ndo maana kila kitu ni mshikeli.Kwa siasa bora hawamawazi wangeshajiuzuli siku nyingi kusubiri uchunguzi wa dola na kwa uongozi bora waliowateua wangeshawawajibisha siku n yingi.Ni ajabu waziri kafanya madudu halafu adai hajapata ripot? Hii ni aibu yetu watanzania,ni aibu ya polisi wanaohangaika kumkamata mwanasiasa i.e slaa huku wanaotuhumiwa kuhujmu uchumi wakitamba mitaani.:A S shade:
 
Back
Top Bottom