Rais Kikwete chukua hatua haraka, wahusika wa ghasia wafilisiwe mali zao

proisra

JF-Expert Member
Jun 14, 2012
213
158
Tanzaniatokea uhuru haijawahi kushuhudia uvunjifu mkubwa wa amani na uchochezi wa marakwa mara kama awamu hii ya Rais JakayaKikwete. tunakiri hili kwani kwa umri wa baadhi yetu, marais wote wa taifahili tumewashuhudia, kwa awamu zote (Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete). Ila hadisasa J.K kaweka historia ya kufumbia macho maovu yanayotendeka chini ya utawalawake. Zanzibar,sehemu ya Jamhuri ya Muungano, kila siku ngoma za kuuvunja muungano zinapigwana kuchezwa. Makanisa lukuki yamechomwa moto Zanzibar, chini ya utawala huu huuwa J.Kikwete… Hakuna hatua za maana zimechukuliwa. Tanganyika(upande wa Bara), mauaji ya wananchi wasio na hatia kukabiliana na mikutano ya vyamavya upinzani yamefanyika na yanaendelea, Damu zao zinalia ardhini. Nahatutoshangaa hata ndani ya mwezi/mwaka huu tukashuhudia mauaji mengine ya raia...Hakuna hatua za maana zitachukuliwa vile vile. Misikiti inayohubiri chukiimeongezeka, kila upande, tukiwa majumbani tunahubiriwa chuki kupitia spika zahii misikiti. Isitoshe, Radio Imann yamjini Morogoro na magazeti ya Al-nooryanapandikiza chuki za udini kila wakati. Hakuna hatua za maana zimechukuliwa. Mtuanashindwa kutofautisha mahubiri ya chuki yanayotolewa kwa watoto wa Kipalestinadhidi ya Israeli na mahubiri ya kiislamu ya chuki dhidi ya Wakristo hapa Tanzania…Mbagala makanisa zaidi ya matatu yamechomwa moto juzi Ijumaa 12/10/2012. Je,isingekuwepo CHUKI, makanisayangechomwa moto? Hapana. Waislamu wangekuwa wanahubiriwa UPENDO kwa jiraani zao, haya yote yangetokea? Hapana. Je, hatua zamaana zimechukuliwa? Hapana. Pale ManzeseBakhresa (Dar es Salaam), mahubiri ya kudhalilisha dini zingine (na hasaUkristo) yanaendelea. Hakuna hatua za maana zimechukuliwa. Yamkini vipo vikundi vya wakristo vinafanya mambo haya haya ya Manzese Bakhresa (ingawasina data) lakini pia hakuna hatua za maana zimechukuliwa. KuwaRais na kuingia Ikulu siyo mwisho wakufikiri, kusikia wala kuona. Na wala siyo mwanzo wa kula bata tu na kusahauwajibu wako kikatiba kwa jamii iliyokupatia hiyo nafasi. Rais J. Kikwete usijisahau.kumbuka kuwa hata neno moja tu unalotamka kinywani mwako litaleta athari zipikwa jamii tofauti yenye uelewa tofauti, itikadi tofauti, na imani tofauti (a complex society). RaisJ. Kikwete, hatudhani kama umeshindwa hii kazi ya kutawala. Yamkini umesahau kidogowajibu wako kikatiba. Biblia inasema hivi (Ifa sentence against an evil work is not executed speedily, therefore the heartof the sons of men is fully set in them to do evil…Endapo hukumu kwa watendamaovu haitolewi haraka, mioyo ya wanadamu hujaa mipango ya kutenda maovu…(Mhubiri 8:11). Sisisiyo wasemaji wa Jumuiya za Wakristo wanaokandamizwa kwa sasa chini ya utawalawako. Tusingependa ushauri wetu kwako utafsiriwe na wapenda UDINI kama sehemuya uchochezi. Ila tunakushauri, UCHUKUE HATUA ZA MAANA HARAKA, kabla mioyo yahawa wanadamu haijapanga maovu. Kumbuka nenp la Mhubiri 8:11 hapo juu ni la Mungu, na neno la Mungu kuna wakatilitatimia. Hatua za kamata kamata ulizochukua siyo mwaraobaini. Utakamata wangapi,endapo kila kona ya Tanzania vikundi vya uchochezi vimezagaa. Je, makanisayaliyochomwa moto yatajengwa lini na nani? Magari yaliyovunjwa je, ni nani atayakarabati? Tunashauri iwepo sheria ambayo,wahusika wa ghasia Tanzania (wawe Waislamu, Wakristo, Polisi au Vyama vyaSiasa) wafilisiwe mali zao zote ili kufidia hasara ya uovu wanaosababisha. Tunajuahili litakuwa suluhisho la kudumu (Sustainable soltuion), kuliko kuweka watundani, huku vidonda vya uovu wao vikiwa havitibiwi haraka. Rais J.K,ukishauriwa, haijalishi ushauri mzuri kama huu umetolewa na nani, fanyia kaziushauri huo. Usivute muda ili kusubiri utoke madarakani 2015 ili atakayekurithiIkulu ndiye apambane na mizigo hii iliyo chini yako leo. Kila mtu na kila raisatabeba mzigo wake mwenyewe. Kikwete, chukua hatua za haraka sasa.
====ChristiansUnited For Israel (C.U.F.I), Tanzania Chapter====
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom