Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda

Status
Not open for further replies.
Simpendi Kikwete toka moyoni na chama chake, ila kwa hili sioni 7bu ya yeye kushauriwa kuomba msamaha. Kwa kawaida ushauri hutolewa katika hali ya take it or leave it. Alichotakiwa kufanya Kagame ni kuuchukua au kuuacha huo ushauri wa Kikwete na siyo kupiga kelele na vijembe visivyokuwa na maana hata kidogo.

"Kikwete asiombe radhi kwa kuwa hajakosea lolote!!!!!"
 
Ushauri wako haufai. Ikiwa Kagame hataki kushauriwa basi na aache kama ambavyo tunaukataa ushauri wako.
 
Tusi wewe? Au M23 ?
Suala ni kuwa realist, sio utusi. labda wewe ndi mtusi! Lakini pia kuwa mtusi, si ni binadamu wa kawaida tuu, huwapedi watusi? We are all Africans, unaweza ukawachukia kumbe na wewe babu zako walitoka hukohuko! Why can we proud of our Continent instead of creating this divisions and segregation?
 
KUNA msuguano wa waziwazi unaoendelea kati ya Tanzania na Rwanda kufuatia ushauri wa Rais Jakaya Kikwete kwa mwenzake Paul Kagame, kumtaka akae na kuzungumza na waasi wa FDLR.



Kwanza lazima nikiri kuwa ushauri huo wa Rais Kikwete ni mzuri kutokana na dhamira njema iliyobeba ushauri huo. Dhamira inayolenga kuyapatia ufumbuzi wa kudumu matatizo ya kiusalama yanayozikabili nchi za Rwanda, Uganda na DRC kwa miongo kadhaa sasa.


Hata hivyo, ushauri huu haukuwa sahihi na haukutolewa mahali sahihi. Haukuwa sahihi kwa sababu haukuzingatia ukweli na mtazamo wa Kigali juu ya kundi la waasi la FDLR.


Na George Maziku
0659985064

Huyu Mwandishi si mwelewi kabisa.
Hivi kuna tatizo gani kwenye Ushauri mpaka ilete hasira kama si ujinga.Si kama hutaki unaacha tatizo liko wapi? Eti Kagame aombwe radhi, kwa lipi ?

Watu wengine wanasahau kuwa matatizo ya Rwanda kwa sehemu kubwa yana mkono wa Kagame na M7 hivyo kwa wao kutoa nafasi ya Uhuru wa Kisiasa kwa wengine ni Dhambi ndiyo maana amehamaki baada ya kupewa Ushauri huo.
 
Ni ajabu mtu anashauri ndugu wapatane alafu anaonekana mbaya,Mh rais wetu ajafanya kosa kutoa ushauri huu,tanzania ni muhadhirika mkubwa wa hali iliyotokea Rwanda baada ya akina kagame kuitungua ndege ya rais,ktk mauaji ya kimbari tulipokea wakimbizi 800,000-1,000,000 adhari za kimazingira,kiusalama na kijamii mpaka leo wantanzania wa kigoma na kagera bado zinawakabili.Duniani njia ya maongezi ndio inazaa mapatano ya kweli dhidi ya maasimu mfano ujermani,msumbiji,angola,burundi nk labda rwanda mna ajenda yenu.Kagame naamini ajasahau mchango wa nyerere(tanzania)katika kuipigania amani ya kwao.SS unatishia vita ni uongo kagame sio chizi awezi kuwaza kupigana na tanzania.Heko rais wangu ulitoa ushauri sehemu sahihi na wakati sahihi
 
George, nashindwa kuamini kwamba JK aliongea hilo jambo mbele ya Mkutano ule kabla ya kuongea na P Kagame faragha. Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba JK na Mamlaka za Tanzania walishaongea sana faraghani na mamlaka za Rwanda kuhusu hilo na mamlaka za Rwanda zikakataa pendekezo hilo huko huko faraghani ndio maana JK kaamua kulibwaga pendekezo hilo mkutanoni.

JK na mamlaka za TZ hawawezi kukosa ustaarabu kama huu. Haiwezekani. Dhahabu na Urani za DRC ni tamu sana kwa Kagame!
Usiconclude hivyo, kuna watu huwaga wanasema harafu ndio wanaanza kupima hoja kama ni ya kuboa, tabia yao utakuta anasema then anatoa ulimi kuwa kakosea, huenda .....!!!
 
Kikwete ni rais wetu, ni kweli hajafanya kosa lakini hebu tujiulize asingetoa huu ushauri malumbano haya yangekuwepo? kwani alilazimishwa kutoa ushauri? na nani alimtuma kutoa ushauri wakati wenyewe wamesema hawautaki? mkijibu hayo maswali mtajua mchokozi ni yupi, sometimes tuwe wakweli.



Kenge mkubwa, hujui madhara tunayoyapata kutokana na hali Ilivyo huko CONGO DRC, kwa nini tulipigana NAMIBIA, ANGORA, MSUMBIJI NA NCHI NYINGINE BARANI AFRICA? KAGAME amekuwa akiua watu bila huruma, soma post za reat thinkers kabla ya kumwaga povu humu jamvini.
 
Acha kukurupuka wewe,mujda huo ungeutumia kwenda kwenu Singida ukaleta mafuta ya alzeti uwauzie watu kuliko kuandika matapishi.Wewe unajua unachokiongea ama unaropoka tu, nani ni muuaji kati ya RPF na Interahamwe? Interahamwe ndiyo ilikuwa imeshikilia serikali na sasa wamevamiwa na waasi ulitegemea wakae kimya na hasa baada ya rais wao na Mkuu wa majeshi kutunguliwa na RPF kwenye ndege.Haya soma mwenyewe ndiyo utajua kati ya Interahamwe na RPF nani ametekeleza maauaji ya halaikiView attachment 105123Hungry for Truth, Peace and Justice: Testimony of Abdul Ruzibiza about how mistakes by both the Rwandan Government and the RPF led to the Rwandan genocide of 1994
 
I'm sorry to say, asiyewafahamu vizuri Wanyaranda ndiye atakaye weza kununua hili bandiko na kufanya kama mleta bandiko anavyopenda.

Wanyarwanda ni vinyonga na kwa ukinyonga wao, kwa sasa wameishaifanya EAC kuwa talking shop.

Siwezi kushangaa kama mleta mada atakuwa ni wale wale au ameishawezeshwa ili kupata nguvu za spinning kwenye international politics.

Relax, mbona mnatumia nguvu nyingi kujibu sentesi moja ya Rais Kikwete, au ndiyo yale yale ya guilty conscience kuwasumbua.

Ng'wamapalala, with due diligence naomba nitofautiane na wewe katika hili maana conclusion yako is short of both political and spiritual diplomacy. Nitajikita katika spiritual diplomacy ambayo naamini na wewe unayo to some extent as not long time back you stated to have been altar boy. Even though you were at tender age but catechism teaches us to reconcile, confess and self negation. So as ex- altar you should know that sincere penance is complete when you apologise sincerely even to those who have trespassed or done wrong to you.To put myself in the shoes of many, Kagame has done wrong to President Kikwete in all the remarks uttered following Kikwete's advice. However, as a spirit of tolerance and forgiveness Kikwete's apology to Kagame can add value. It's hard for normal human being to do but as a matter of fact, that's how spiritually we are supposed to die a little for a better world. Nawasilisha
 
Kikwete ni rais wetu, ni kweli hajafanya kosa lakini hebu tujiulize asingetoa huu ushauri malumbano haya yangekuwepo? kwani alilazimishwa kutoa ushauri? na nani alimtuma kutoa ushauri wakati wenyewe wamesema hawautaki? mkijibu hayo maswali mtajua mchokozi ni yupi, sometimes tuwe wakweli.

Mkuu Feedback wala huna sababu ya kukubaliana na wengi wakati unaelewa siyo kweli. Kikwete alitoa ushauri wa kipuuzi,ambao hakuwa na weledi wowote!

Watanzania wenzangu wanapaswa kutambua kwamba watu walioshiriki ktk mauaji ya kimbari wanaweza safishwa ktk mkondo wa sheria siyo mazungumzo ya amani!

Wayahudi hawakufanya mazungumzo ya amani na Wanazi, Yugoslavia ya zamani wahalifu wa mauaji ya kimbari bado wanasakwa,Cambodia wauaji wa mauaji ya kimbari bado wanasakwa,na imeanzishwa mahakama maalumu kuwahukumu.

Ktk ikiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanyika Afrika ni Rwanda na Siera Leone tu ambako ukiukaji wa haki za binadamu,UN imefungua mahakama maalumu kushughulikia makosa ya kivita. Kesi za watuhumiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita za Wakenya na mabwana wa vita wa DRC ni tofauti na hawa walioshiriki ktk mauaji ya kimbari.

Kikwete alipaswa kutambua kwamba ushauri wa kupata amani usiwakwaze watu. Ni lini hao waasi waliwahi omba msamaha kwa ukatili walifanya? Leo hii majirani zake Wazaramo wakiamua kuchinja Wakwere kqa mauaji ya kutaka kufuta kizazi chote cha Wakwere ataanzisha mazungumzo ya amani,tena watu ambao bado wanaamini kwamba Wakwere hawana haki ya kuishi?
 
umeongea kidiplomasia saana, mi naona kuna logic, ukimwambia mtu kitu asipopendezwa nacho, huna budi kumuomba ladhi, i can see the logic behind, manaake ninachoona ni mpambano usio na tija kwa pande zote mbili!

Hakuna la maana aliloandika hapo zaidi ya kutetea utusi. Kuna mahali ameandika kuwa watusi waliuliwa na intarahamwe (wahutu), mbona hazungumzii jinsi kagame alivyomuua rais Mhutu. Hivi ina maana mtusi akiuliwa ni unyama lakini akiuliwa mhutu siyo unyama kwa kuwa wao hawana nyama. Kasimba unasema mtu ukimpa ushauri kama hataki umuombe radhi, je wewe unaona ni sahihi kama hutaki ushauri njia sahihi ni kumtishia aliyekupa ushauri?
 
Mnaomkandia KAGAME, haya watoto wa shule za Msingi wanatumia LAPTOP 4G.. Uhuruto wanafuata nyie mliozaliwa after 1978 war between Tanzania and Uganda endeleeni kuwazia VITA:
 

Attachments

  • Kagame.jpg
    Kagame.jpg
    41.2 KB · Views: 102
Mimi naona Kagame na vibaraka wake ndio wanatakiwa kumuomba radhi Rais wetu kwa kumshambulia binafsi kwa kuwapa ushauri wa bure wa jinsi ya kumaliza mgogoro wao. Asituletee mambo ya kishirikina ya kuabudu mafuvu ya binadamu kwa kisingizio cha kumbukumbu za mauaji ya Kimbari.
 
Hamjui uchungu walionao wanyarwanda mpaka leo kwa kupoteza ndugu zao wengi kipindi kile ndio maana hatuwezi ona uzito wa jambo hili miyoyoni mwao.watafute njia ya kurudisha amani na kuwatuliza M23 ila kwa kutumia busara pasipo kuleta mgongano kama huu usije ukatuvuruga zaidi.
 
Khaa!!! wewe bure kabisa! amuombe msamaha kwa lipi? Kumpa ushauri? Ningekuwa JK kwanza ningeanza kumwambia aache kuwasaidia M23 kisha ndiyo akae na ndugu zake waongee wayamalize
 
Simpendi Dhaifu kwa sababu ni dhaifu na ANACHOSHA! (maoni ya Raia Mwema la leo)
Lakini kumuomba msamaha Kagame sikubali, huyu ni mal_ya wa wazungu amekuwa 'spoiled' yaani ashauriwe kiungwana namna ya kupata amani halafu atake kuanzisha vita nyingine na aliyemshauri?! ------- zake kabisa! Dhaifu hajakosea, hapa kapatia, asiombwe msamaha mal_ya mkubwa!
 
Simpendi Dhaifu kwa sababu ni dhaifu na ANACHOSHA! (maoni ya Raia Mwema la leo)
Lakini kumuomba msamaha Kagame sikubali, huyu ni mal_ya wa wazungu amekuwa 'spoiled' yaani ashauriwe kiungwana namna ya kupata amani halafu atake kuanzisha vita nyingine na aliyemshauri?! ------- zake kabisa! Dhaifu hajakosea, hapa kapatia, asiombwe msamaha mal_ya mkubwa!
 
Maziiku tayari Kagame amefanya uchokozi wa kutosha na Rais Kikwete Amekuwa mpole kupita kiasi. Wenyeji wa Kagera wanahujumiwa na Rpf sana. Wamejimilikisha kimabavu karibu pori lote linalounga wilaya ya Bk vijijini upande wa Izimbya kuelekea Burigi upande wa Muleba hadi Biharamulo kuzungukia Nyakahura hadi Ngara na kurudi Karagwe. 1. Wameyafanya mapori haya ya akiba mali yao wakihonga watendaji wa kata na madiwani katika vijiji vinavyozunguka mapori. Pesa ya kuhonga watendaji wa serkali wanaipata kwa kuteka na kuua raia na kuwanyang'anya mali zao. Sasa huyu Kagame ataendelea kutambanchini kwetu hadi lini? Hayo maendeleo unayodai yatafanyikia wapi? Bahati nzuri wananchi wa Rukoma- Izimbya juzi waliua askari 2 wa Rwanda waliokuwa na bunduki za kijeshi waliokuwa wamevamia mnada wa ng'ombe. Namuunga mkono rais Kikwete hawa watu warudishwe makwao kwa nguvu, na atakayeleta luneno anyolewe!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom