Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda

Status
Not open for further replies.
wewe unaona dhahabu za congo!!! kama JK ana uchungu na rasilimali za congo inakuwaje zetu ndo anagawa kawa pipi.. in short the man is real an intention seeker that only what i can see on him but even with his weakness never absolve Rwanda from all allegation from international community, the best thing is to handle everything in diplomatic way..
NO PRIOR DIPLOMACY then NO RESOLUTION DIPLOMACY hakuna cha kumwomba Kagame msamaha! kwani kwa ushauri wake mh. KIKWETE hakufanya kosa lolote na hata kama kwa ukarimu wake JK ataonelea bora kumwomba radhi dhalimu Kagame, namshauri asifanye hivo. Labda aombe mkuu wa wilaya ya KONDOA kwa niaba ya RAIS ingawa hana kosa kabisa RAIS WETU.
 
Huyu Marcopollo Wa tz Aombe Radhi Tu Wanyarwanda Kwa Kuingilia Mambo YasiyoMhusu, Akiendelea Kubisha, Kagame Mfanye Kama Juverinal Habyrimana..... Tungulia Mbali Huko Akafie Huko....shwain!
WANYARWANDA UTAWAJUA TU! YAAN WE KICHWA CHAKO HAKITOFAUTIANI KAGAME, AMBAYE ANAONA KUSHAURIWA NI DHAMBI!!!!!!! acha upungufu wa uyakinifu wewe. na huyo Kagame hawezi kupigana na TZ
 
Manyerere nakuheshimu sana. Hivi kweli hili ni la kitaifa au uchokozi wa waziwazi? Hivi JK amejifanya big brother na kutoatoa ushauri? Kagame ameutafsiri vingine, kwamba anajaribu kwaosha FDLR na kuwapa recognition. Manyerere ulikuwa na miaka mingapi 1994? Hawa jamaa walivyoua na kudhalilisha ubinadamu kwa hali ya juu? Jamani, tuache nationalism za kipuuzi, kwanini iwe Kikwete? Mbona Ban Ki Moon, Anan, mkongwe Museveni, Zuma, etc, hawajawahi kutoa ushauri kama huu?
Hata kama hammpendi Rais Kikwete, nasema kwa hili hana sababu ya kuomba radhi. Aombe ili iweje? JK watuachie sisi wenyewe tutofautiane naye huku, linapokuja suala la nchi, msimamo wetu ni mmoja-kuungana! Tusikubali kwa namna yoyote kuruhusu nguvu za nje kutuvuruga hata kama Rais wetu wengine humu ndani hawampendi.
 
Watanzania umaskini wetu umechangiwa na vitu vingi, kwanza serikali yetu inatoa huduma kwa raia wasio wake, tangu miaka ya 70 tanzania imekuwa ikiwapokea raia kutoka Rwanda na Burundi, kwa wale waliozaliwa juzi hawajui kama tuna makambi ya wakimbizi huko mishamo Rukwa na nk, hawa ni watutsi kutoka Rwanda. kwa wenyeji wa mikoa ya kanda ya magharibi na ziwa waulize wakwambie tumepoteza ndugu wangapi wasio na hatia kwa sababu ya siraha kutoka Rwanda na Burundi. Ni hekta ngapi za misitu zimeteketea kwa kuwahifadhi watu hawa? ni maliasili kiasi gani ikiwamo wanyama hasa tembo wameteketea kwa sababu tu ya upole wetu. Kagame anaua watu bila sababu angalia yule mama mpinzania wake kamfunga kwa sababu tu ana mawazo tofauti na ya kagame, Prop wetu wa mlimani aliuawa na kikundi cha majasusi wa kagame, why tuendelee kuona dhambi hii ikiendelea miaka na miaka? now no. ikiwezekana tumwondoe ili nchi rwanda iwe na amani ya kudumu, kwa sasa wana amani ya woga.

wewe uliyetoa mada hii siyo mtanzania laiti tungekujua tungeiamba serikali ifuatalie uraia wako. Rais wetu ataukanwe kama mtoto mdogo harafu tukapige magoti kuomba msamaha?

Kagame amekuwa akisisitiza mazungumzo ya amani kati ya Kabila huku nyuma anaingiza majeshi yake kuwapa support waasi wa m23.

Kagame ndiye aliyefanya mpango wa kumuua Rais wa DRC CONGO marehemu Laurent Kabila.

Ushauri kwa Rais wetu, aongewe ulinzi kwaani kauli ya kagame kuwa atamsubiri sehemu na atamuua siyo kauri ya kutazamwa kirahisi, tunatakiwa kufanya maamzi sahihi katika muda sahihi.

Mtoa mada: wale WAASI walioko congo siku wakikimbizwa huko watenda wapi kama siyo kukimbilia Tanzania na then kuwa majambazi kutuua kwa kusiriki ujambazi na kuteka magari?
 
NDEGE ILIYOTUNGULIWA NA KAGAME 1994.jpg

haya ni mabaki ya ndege iliyoangushwa na paul kagame na ndiyo chanzo cha mauaji ya haraiki ya rwanda

watanzania umaskini wetu umechangiwa na vitu vingi, kwanza serikali yetu inatoa huduma kwa raia wasio wake, tangu miaka ya 70 tanzania imekuwa ikiwapokea raia kutoka rwanda na burundi, kwa wale waliozaliwa juzi hawajui kama tuna makambi ya wakimbizi huko mishamo rukwa na nk, hawa ni watutsi kutoka rwanda. Kwa wenyeji wa mikoa ya kanda ya magharibi na ziwa waulize wakwambie tumepoteza ndugu wangapi wasio na hatia kwa sababu ya siraha kutoka rwanda na burundi. Ni hekta ngapi za misitu zimeteketea kwa kuwahifadhi watu hawa? Ni maliasili kiasi gani ikiwamo wanyama hasa tembo wameteketea kwa sababu tu ya upole wetu. Kagame anaua watu bila sababu angalia yule mama mpinzania wake kamfunga kwa sababu tu ana mawazo tofauti na ya kagame, prop wetu wa mlimani aliuawa na kikundi cha majasusi wa kagame, why tuendelee kuona dhambi hii ikiendelea miaka na miaka? Now no. Ikiwezekana tumwondoe ili nchi rwanda iwe na amani ya kudumu, kwa sasa wana amani ya woga.

Wewe uliyetoa mada hii siyo mtanzania laiti tungekujua tungeiamba serikali ifuatalie uraia wako. Rais wetu ataukanwe kama mtoto mdogo harafu tukapige magoti kuomba msamaha?

Kagame amekuwa akisisitiza mazungumzo ya amani kati ya kabila huku nyuma anaingiza majeshi yake kuwapa support waasi wa m23.

Kagame ndiye aliyefanya mpango wa kumuua rais wa drc congo marehemu laurent kabila.

Ushauri kwa rais wetu, aongewe ulinzi kwaani kauli ya kagame kuwa atamsubiri sehemu na atamuua siyo kauri ya kutazamwa kirahisi, tunatakiwa kufanya maamzi sahihi katika muda sahihi.

Mtoa mada: Wale waasi walioko congo siku wakikimbizwa huko watenda wapi kama siyo kukimbilia tanzania na then kuwa majambazi kutuua kwa kusiriki ujambazi na kuteka magari?
 
mi naomba upigwe ban kwa kututusi sisi watanzania wote maana unaona kama vile hatuna akili zilizoko sawa sawa...tumewapokea , sasa mnaaza kutuona wajinga...
 
Mchungaji punguza hasira ueleweke....

Mimi sioni tatizo la mleta mada, ushauri wa George na ule wa JK hauna tofauti kubwa, Kikwete anashauri Kagame akutane na waasi FDLR George naye anashauri Kikwete akutane na Kagame waombane msamaha yaishe kiutu uzima so what is the difference, kwanini ushauri wa mwingine uonekane mbaya?

Kuomba radhi kwa mtu mzima ni kuonyesha usitaarabu na ukomavu hata kama wewe ndiye uliyekosewa, radhi huepusha shari kinyume chake ni kujenga uhasama.
Feedback Hiyo mifano ni tofauti bwana,Kagame anauwa na kuiba mali za Wacongo.Kikwete kamshauri aongee na ndugu zake aliepigana nao yeye hataki kwa kuwa anataka wale jamaa wazidi kuwa kule Congo ili iwe ni chanzo cha kuendeleza fujo ili aendelee kupora na kuiba.Kikwete anapomuomba msamaha Kagame ina maana anabariki uporaji na mauaji ya Kagame????
 
Manyerere nakuheshimu sana. Hivi kweli hili ni la kitaifa au uchokozi wa waziwazi? Hivi JK amejifanya big brother na kutoatoa ushauri? Kagame ameutafsiri vingine, kwamba anajaribu kwaosha FDLR na kuwapa recognition. Manyerere ulikuwa na miaka mingapi 1994? Hawa jamaa walivyoua na kudhalilisha ubinadamu kwa hali ya juu? Jamani, tuache nationalism za kipuuzi, kwanini iwe Kikwete? Mbona Ban Ki Moon, Anan, mkongwe Museveni, Zuma, etc, hawajawahi kutoa ushauri kama huu?
Wewe Kalisa kaa kimya wewe Mauaji ya kimbari yalisababishwa na Kagame na jeshi la serikali lilikuwa linajihami.Kagame ndio chanzo ya yote.
 
...-Namshauri Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda, amuombe radhi Rais Kagame. Ampigie simu amwambie yaishe kwa kuwa hakukusudia kumuudhi wala kumkumbusha machungu ya unyama wa Interahamwe, amwalike Dar es Salaam wanywe chai na mnyinyo.-

... Nonsense!!-

Muheshimu Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania. Ukome kumlinganisha na Huyo MUHUNI na MUUAJI wa Rwanda!!

... Umenielelwa?!!!
 
"Rais Kagame na mamilioni ya wananchi wa Rwanda wa kabila la Watutsi na Wahutu wachache wenye msimamo wa wastani, ni waathirika wakubwa wa ukatili na unyama uliofanywa na FDLR, na bila shaka hawajasahau wala kusamehe.

Rais Kikwete alipaswa kuzingatia ukweli huu kabla ya kuamua kutoa ushauri wake. Kama angezingatia ukweli huu kabla, bila shaka asingethubutu kumshauri Rais Kagame kukaa meza moja na kundi ambalo halijawahi kuomba msamaha kwa Wanyarwanda wala kuonyesha kujutia uovu wao.

Halafu Rais Kikwete alikosea kutoa ushauri huo mbele ya mkutano ule. Hapakuwa mahali sahihi kwa jambo zito kama hilo. Angetafuta nafasi nyingine, na kwa maoni yangu angezungumza na marais wenzake kwa faragha, ama wote kwa pamoja au mmoja mmoja.

Angepata nafasi nzuri zaidi ya kufafanua dhamira ya ushauri wake, na pia angeweza kuona mwitikio wa Rais Kagame juu ya ushauri huo. Ninaamini msuguano wa sasa usingekuwepo kwa sababu wangejadiliana kwa kina na kuyamaliza mambo yote katika chumba kilichofungwa milango.

Sasa ushauri unataka kuzaa vita ya majirani wawili wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Bila shaka madhara yake ni makubwa. Mbali na kusababisha kuharibika kwa mahusiano kati ya nchi hizi, pia zitapoteza maisha ya watu wake na rasilimali, na hivyo kuteteresha uchumi wa kila moja.

Ni imani yangu Watanzania wengi hawataki na hawawezi kuunga mkono uamuzi wa kuingia vitani na Rwanda. Watanzania hawapo tayari kwa vita vingine, baada ya vile vya Uganda vya mwaka 1978. Tunataka kujenga nchi yetu kiuchumi, kisiasa na kijamii kukimbizana na wakati kwa sababu tupo nyuma sana.

Namshauri Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda, amuombe radhi Rais Kagame. Ampigie simu amwambie yaishe kwa kuwa hakukusudia kumuudhi wala kumkumbusha machungu ya unyama wa Interahamwe, amwalike Dar es Salaam wanywe chai na mnyinyo."

!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Bw. Easyjet a.k.a Maziku,
Ushauri wako kwa Raisi Kikwete tumeusoma. Lakini ni ushauri tu ! Lakini kabla haujazingatiwa ingekuwa vizuri utusaidie kuweka mambo kadhaa muhimu wazi:
1. RPF chini ya Kagame walivyodungua ndege ya kiraia iliyokuwa imebeba maRais wa nchi huru mbili( hivi sasa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki) wakitokea Tanzania kuzungumzia amani na Rais Mwinyi -Rais Habyalimana wa Rwanda na Rais Ntaryamira wa Burundi, wafanyakazi wa ndege hiyo na kusababisha vifo vyao hudhani kwamba raia wa nchi hizo na Afrika kwa ujumla tulistahili kuombwa msamaha ?. Au magaidi hawaombi msamaha ?

2. Majeshi ya Rwanda hadi sana yamesababisha vifo na mateso makubwa nchini Congo, weka pembeni uporaji wa rasilimali na uharibifu wa maliasili-Lini waliwahi kuwaomba Wakongo msamaha? Idadi ya vifo vya Wakongo kutokana na vita ambavyo wapiganaji wakuu ni vikosi aidha vya serikali ya Rwanda, makundi ya waasi wa Rwanda na Uganda vimekadiriwa kufikia milioni tatu. Easy jet ungemshauri kwanza Kagame kuwaomba Wakongo radhi kabla ya kufikiria viginevyo.
3. Kwa miaka kadhaa nimekuwa nikisikia baadhi ya Great Thinkers wakihusisha kifo cha Prof Jwani Mwaikusa na Kigali. Huenda siku moja Rais Kagame ataulizwa kuhuzu jambo hili. Lakini kwa familia ya Prof Mwaikusa, Watanzania na hata Mungu wake angeomba msamaha.

4. Zaidi ya hapo, EasyJet ungemshauri Raisi Kagame kuendelea kuishukuru Tanzania, kama jirani mwema kwa kuwapa hifadhi Wanyarwanda kuepuka mauaji na vurugu kila inapobidi. Hakika hifadhi kwa maelfu ya wakimbizi husababisha athari za kiuchumi, kimazingira, kijamii , kiusalama na kisiasa.

5. Ukiangalia yote hayo hapo juu na kuwalinganisha Raisi Kikwete na Raisi Kagame, Rais Kikwete may be a 'Saint'. Kagame je ? Hili nawaachia Wakongo, Warundi, Watanzania, wanajamvi na Waganda mahali ambapo Kagame alipigana vita vya msituni Luwero Triangle, na kuacha marundo ya mafuvu, na baadaye kutumika kama Mkuu wa idara ya ujasusi jeshini.

Nchi kadhaa ikiwemo Marekani wameanza kujifunza kutomhandle Kagame using a kid's gloves. Wengine wameanza kupunguza misaada ili ajirekebishe na kutoa uhuru zaidi wa kidemokrasia katika nchi yake, pamoja na kuacha uvamizi wa nchi za watu bila kuzingatia sheria za kimataifa.

Wakuu naamini kwa yote hayo Riasi Kikwete hana sababu ya kuomba radhi ila kutompuuza huyu jirani kutokana na historia yake.
 
Watu wengine mnakera sana. Kikwete amefanya kosa gani? Yeye ametoa ushauri. Kama kagame hataki ushauri mwambie aachane nao.
 
Duh! Hii nayo inabidi iende kwenye list ya maajabu ya dunia. Kwa hiyo ukitaka kumshauri mtoto wako mbele ya wenzake aache kupigana na mtoto wa jirani utamwita faragha kwanza? Na mtoto wajirani nao vipi, au wao hawatahitaji faragha? Sasa huo si utakuwa mchezo wa kuigiza?

Ushauri wa JK ni ushauri wa UN, JK alijitolea kumfunga paka kengele. Ndio maana UN na USA wamekaa kimya huku wakimpongeza JK kwa chini chini. Na ndio maana Kagame hana amani!! Usiniulize source ya hili tafadhali, kama vipi ichukulie kama udaku tu.

Nimeipenda hii, 'Ushauri wa JK ni ushauri wa UN'. Ila nashawishika pia kwamba serikali ya TZ imefahamu toka siku nyingi kwamba msimamo wa Kagame ni kungángánia DRC ndio maana wametumia Mkutano huo kulipua suala hilo hadharani.
 
Nadhani wewe EasyFit ndo uliombe radhi jukwaa kwa kupost ujinga huu.
 
Last edited by a moderator:
Watu wengine mnakera sana. Kikwete amefanya kosa gani? Yeye ametoa ushauri. Kama kagame hataki ushauri mwambie aachane nao.
Kikwete ni rais wetu, ni kweli hajafanya kosa lakini hebu tujiulize asingetoa huu ushauri malumbano haya yangekuwepo? kwani alilazimishwa kutoa ushauri? na nani alimtuma kutoa ushauri wakati wenyewe wamesema hawautaki? mkijibu hayo maswali mtajua mchokozi ni yupi, sometimes tuwe wakweli.
 
George,
there is no way president Kikwete ataomba msamaha kwa ushauri aliotoa japo ulikuwepo mchemko wa kidiplomasia being EAC heads wail kuwa na more venue or platform for that, same way ambavyo PK atakaa kusubiri hilo la masamaha litokee na eti lisipotokea achukue bunduki kupigana. Wala hakuna sababu ya msingi kwetu Tanzania kupeleka askari wetu kupigana vita eti kwakuwa ushauri uliotolewa na raisi umepokelewa vibaya. Kinachoonekana hapa kuna zaidi ya ushauri na mapokeo ya ushauri. Wizara zote za kidiplomasia baina ya Tanzania na Rwanda zimeshindwa kuliweka swala hili pazuri na hata waziri wetu wa jumuia haliongelei na sasa eti vimekuwa vyombo vya ulinzi na usalama. Kwa upange wa Rwanda issue ya RDC in tata sioni jinsi gani wanaacha kutatua hilo na kuandaa majeshi kupigana na Tanzania. Mpaka hapo nadhani kuna sababu kuu ya vita zaidi ya Mashauri na mapokeo tuwekwe wazi. Nidhabi mbaya kushabikia ugomvi sisi sote ni ndugu.
 
Kikwete ni rais wetu, ni kweli hajafanya kosa lakini hebu tujiulize asingetoa huu ushauri malumbano haya yangekuwepo? kwani alilazimishwa kutoa ushauri? na nani alimtuma kutoa ushauri wakati wenyewe wamesema hawautaki? mkijibu hayo maswali mtajua mchokozi ni yupi, sometimes tuwe wakweli.

Sasa wewe unafurahia mambo yanayoendelea kule kongo?? Kwanini kikwete akae kimya wakati kuna binadamu wanateswa na huyo kagame kule kongo. Kuna msemo mmoja wa kiingereza unasema: evils triumphs when good people do nothing. Kwa hiyo kikwete aliongozwa na hii philosophy. Nyie wanyarwanda dawa yenu inachemka jikoni. Siku yenu inakuja. Tutawasambaratisha, tuwarudishe wahutu madarakani. Msituchezee.

 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom