Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda

Status
Not open for further replies.
Amwite Kagame Dar anywe chai na mvinyo kwa lipi?Ninyi kwa misaada yoote tuliyowapa(kuwasomesha na kuwapa hifadhi) mmetushukuru lini?Huyo Museven amabaye ana mpa kichwa Kagame nae si "mtoto" wetu?Kasoma hapa,kakulia hapa bado tukamuweka madarakani leo yy na jamaa yake Kagame wanajaribu kuitenga TZ....Ninyi Wanyarwanda na watu wenye asili ya kwenu kama Museveni hamna shukrani hata kidogo na ni wabinafsi wakubwa!
 
Hakuna vita wala kuombana msamaha hapa. JK kashauri, PK kakataa. Sasa vita inakujaje hapo? Msamaha kwa kosa lipi?
 
Walio kosana ndio wanakaa meza moja na kupatana.Jk kumshauri Kagame kukaa meza moja na waasi haina maana kwamba Jk kamuona Kagame kuwa ni mharifu wala siyo kwamba waasi hawana makosa.Jk alitoa ushauri huo kwa sababu nayo ni njia moja wapo ya kupatikana kwa ufumbuzi na ule ulikuwa ni ushauri tu.Ambacho kilikuwa kinatakiwa kufanywa na Kagame ili kuwa ni kuukataa ushauri kwa sababu siyo lazima aukubali badala ya kujibu kwa kejeri kama vile.Unajuwa hawa wenzetu wa Rwanda wameshazoe vita kwa hiyo akiri zao na mawazo yao ni ya kivita vita tu sasa kama wanamuona hata yule anaye wapa ushauri wa kukaa meza moja na waasi ili kumaliza matatizo yao naye wanamuhesabu ni kama mharifu ninafuu tukazichapa tu kuliko kuomba msamaha.
 
wewe umetumwa nini? mbona hujamwambia kuwadi wako KAGAME awaombe radhi watanzania kwa matusi aliyotuporomoshea? Rais kikwete kosa lake ni kumwambia KAGAME azungumze na waasi? huyu kagame mbona amejaa damu za binadamu wasio na hatia ambao amewaua? JK alikuwa very specific kwa kagame. kwanza Tanzania hatuna chuki na wanyarwanda.
 
Jk anamapungufu yake ya ndani ya nyumba yake,lakini kwa hili hajaonesha mapungufu. Hakuna cha kuomba msamaha wala nini hapo.
 
Kwanza sioni ka Rwanda ati kivuli chake kinatutisha kiasi hicho labda kama wao wanataka kupatia umaarufu kwamba wana bifu na tz, lakini si saizi yetu ile ya bila kutafuna maneno, mbili mtu akikwambia kamalize ugomvi na jirani yako anakosa gani?Hakuna kutishiana nyau ati toka kwa mtu ambaye hata huo u jeda wake alifundishwa hapa home,Kislan kwetu atalia...hahahahah,so mtoa hoja kama ulidhan unawasilisha tatizo hakuna tatizo hapa...
 
George JK asipoomba msamaha nini madhara yake?
Kama madhara yake ni vita mi nasema na iwe hivyo. Hao wanyarwanda ndio wakuomba msamaha kwa tumewalea kwa zaidi ya miaka 20.

Tukianza vita na Rwanda kwanza tutafunga mipaka yote.Je wakimbizi wenu watakimbilia wapi congo kuna vita, Uganga kuna vita na Kone.

Wanyarwanda waombe radhi maana vita ikitokea hawana pa kwenda zaidi ya kusubiria kufa mmoja baada ya mwingine.
 
Dah! for sure Kagame nilikua namuona km role mode wangu! lakini kwa hili dah am sory kusema nimekushusha sana kwa kauli ulizozitoa hasa kwa Rais mwenye ushawishi mkubwa Afrika na nje ya bara! Hukutumia lugha za kiutu uzima achilia mbali za kiuongozi! Kagame usitafute matatizo ambayo huyawezi Tanzania ni baba yako kwa kila nyanja kupigana nae huwezi ila anaweza kukuadhibu kidogo tu! Kagame nakushauri uombe radhi kwa matamshi yako lasivyo utaiangamiza Rwanda! kumbuka umekalibishwa EAC
 
George, nashindwa kuamini kwamba JK aliongea hilo jambo mbele ya Mkutano ule kabla ya kuongea na P Kagame faragha. Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba JK na Mamlaka za Tanzania walishaongea sana faraghani na mamlaka za Rwanda kuhusu hilo na mamlaka za Rwanda zikakataa pendekezo hilo huko huko faraghani ndio maana JK kaamua kulibwaga pendekezo hilo mkutanoni.

JK na mamlaka za TZ hawawezi kukosa ustaarabu kama huu. Haiwezekani. Dhahabu na Urani za DRC ni tamu sana kwa Kagame!

Duh! Hii nayo inabidi iende kwenye list ya maajabu ya dunia. Kwa hiyo ukitaka kumshauri mtoto wako mbele ya wenzake aache kupigana na mtoto wa jirani utamwita faragha kwanza? Na mtoto wajirani nao vipi, au wao hawatahitaji faragha? Sasa huo si utakuwa mchezo wa kuigiza?

Ushauri wa JK ni ushauri wa UN, JK alijitolea kumfunga paka kengele. Ndio maana UN na USA wamekaa kimya huku wakimpongeza JK kwa chini chini. Na ndio maana Kagame hana amani!! Usiniulize source ya hili tafadhali, kama vipi ichukulie kama udaku tu.
 
Hata kama hammpendi Rais Kikwete, nasema kwa hili hana sababu ya kuomba radhi. Aombe ili iweje? JK watuachie sisi wenyewe tutofautiane naye huku, linapokuja suala la nchi, msimamo wetu ni mmoja-kuungana! Tusikubali kwa namna yoyote kuruhusu nguvu za nje kutuvuruga hata kama Rais wetu wengine humu ndani hawampendi.
Hamtaki diplomasia ichukue mkondo wake...kwa sababu mnayo malengo yenu ya kuanzisha vita na Rwanda....ikizingatiwa tunaelekea uchaguzi mkuu 2015.

Nchi inayosifiwa kwa amani...inapotokea mwandishi "maarufu" wa habari, amabaye amelelewa katika masuala diplomasia ya kulinda amani, akashadadia masuala ya vita ujue kuna namna
 
tumechoka mambo ya wanyarwanda. kuwapokea tuwapokee sisi, hifadhi tuwape sisi, elimu ya bure tuwape sisi, kisha tuwaombe msamaha!? majangaaaaaa, majangaaaaa kweli majangaaaaaa. :wave:KAMWE hatuwezi fanya ujinga hou. kagame na rwanda yake ni wadogo sana kwetu. kwa taarifa yake, UN imeruhusu vikosi vyake DRC kjihami na kupokonya waasi silaha. breki kigali twaja.........
 
Upo sahihi dhahabu hizo ndio zinazoa mtoa roho kam waliokufa wameshakufa wahutu ile ni inchi yao pia nilishani kama rais yy ndio alitakiwa kukomesha hili kwa faida ya vizazi vya mika mia ijayo.kuna kitu anakipata aombwe radhi kwa lipi baya waswahili wanasema JERI MWENZIE KUSUDI,UKISIKIA KICHEFU CHEFU TAPIKA SIO KULA NDIMU,kwani kagame alisemea chumbani huku milango ikiwa imefungwa?Jk ni wetu watuache tusigane nae wenyewe hapa ni utaifa.SINGI VITA WALA C PENDI kwakuwa mimi nitakuwa ni mmoja wa waathirika lakin Kagame kwa hili kateleza na cjui kwanini walimuingiza kwenye EA.???Rais Kikwete alimtaarifu Rais Museveni kile walichojadili baada ya yeye kuchelewa kufika. Alisema ni vema serikali za Rwanda na Uganda zikakaa na kuzungumza na makundi ya waasi wa nchi zao, na kulitolea mfano kundi la waasi wa Rwanda la FDLR.Inasemekana ushauri huo uliungwa mkono na Rais musevi,lakini ulipingwa vikali na Serikal ya Kigali.
Ina mana walishakaa chumbani kama ulivyotaka lakini yeye ndio kawa bedui wa kuyatoa NJE




George, nashindwa kuamini kwamba JK aliongea hilo jambo mbele ya Mkutano ule kabla ya kuongea na P Kagame faragha. Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba JK na Mamlaka za Tanzania walishaongea sana faraghani na mamlaka za Rwanda kuhusu hilo na mamlaka za Rwanda zikakataa pendekezo hilo huko huko faraghani ndio maana JK kaamua kulibwaga pendekezo hilo mkutanoni.

JK na mamlaka za TZ hawawezi kukosa ustaarabu kama huu. Haiwezekani. Dhahabu na Urani za DRC ni tamu sana kwa Kagame!
 
Binafsi huwa sipendi kuwakosoa wenzangu kwa majina makali kama mnafiki, mwongo nk. lakini kwa uzi huu bwn Easyfit unakaribisha moja kati ya sifa hizi zisizo nzuri bila kujali wewe ni Rwandiz au Mtz kama mimi. Hoja yako ya kuwa JK alikosea kutoa ushauri ule kwa Bwn Kagame si sahihi kwa kuwa mkutano ule ulikua kwa ajili ya kutafuta amani ya kongo na wahusika wote wanajua kuwa M23 inapewa support na Kagame kuleta instability ndani ya kongo, kwa msingi huo hakukua na sababu yoyote ya kuongea swala lile chumbani kwa maana hakuna siri inayofichwa hapo kagame ajue kuwa watu wamechoshwa na vita ya kongo isiyoisha, Pili hakuna usahihi katika hoja ya kukaaa faragha kwa kuwa suala la kongo lishaongelewa sana kwa levels mbalimbali , mbona Museven amekubali kistaarabu kwani kuna kipi cha ajabu kinachompa kagame credit zaidi ya museven ? ni vyema wenzetu raia wa Rwanda wapenda amani mkaliongelea hili japo najua huko kuna mkono wa chuma (kagame) ambao ni tishio kwa wapenda ukweli. Mwisho ni vyema Bwn Easyfit ukatumia hizo busara zako kuwaonea huruma wananchi wenzio wa Rwanda wanaokandamizwa na utawala uliopo Rwanda kwa sasa, ujue pia kuwa japo Tanzania hatupigii chapuo vita lakini ikibidi hatutarudi nyuma msijidanganye kuona tofauti zetu za kisiasa katika hili tutasimama pamoja.
 
Hamtaki diplomasia ichukue mkondo wake...kwa sababu mnayo malengo yenu ya kuanzisha vita na Rwanda....ikizingatiwa tunaelekea uchaguzi mkuu 2015.

Nchi inayosifiwa kwa amani...inapotokea mwandishi "maarufu" wa habari, amabaye amelelewa katika masuala diplomasia ya kulinda amani, akashadadia masuala ya vita ujue kuna namna

Ndugu yangu, kosa la Rais Kikwete ni lipi? Hivi kumwambia Rais Kagame azungumze na wabaya wake ili amani itamalaki Rwanda na ukanda huu wote ni kosa la kumshurutisha Rais wetu aombe raidhi? Aombe radhi kwa lipi?

Fikiria, ni kama wewe leo umwambie Rais Kikwete aketi na Chadema wamalize tofauti zao. Je, ni haki Rais Kikwete au Freeman Mbowe kuudhika? Je, watokee watu humu wakushurutishe uombe radhi kwa kauli yako, utakubali?

ndiyo maana nasema, Rais Kikwete ni rais wetu. Linapokuja suala la nchi na nchi, lazima tusimame upande wa Rais wetu hata kama wapo Watanzania wasiompenda. Suala la nchi lazima ushabiki wenu uwe mmoja. Hivi ninavyoandika majibu haya nasikiliza Redio DW ikitangaza kwamba Rais Obama kawatuma maseneta wawili, akiwamo John McCain (wote wa Republican) kwenda Misri kuhakikisha amani inarejea. Obama kafanya hivyo kwa manufaa ya Marekani. Linapokuja suala la nchi, Chadema, CCM, UDP, TLP na wasio na chama sote tunapaswa kuwa kitu kimoja. Rais wetu hawezi kutukanwa halafu tukashangilia. Tukishangilia, tutaonekana mazuzu mbele ya jumuiya ya kimataifa.
 
Wewe George Maziku una akili kweli? Umepewa sh.ngapi na Kagame uje uandike huu ujinga wako? Kwanza Kagame ndio chanzo cha yote kwa maana walipindua serikali halali.Wewe unafurahia ujambazi wa Kagame anaoufanya Congo kuiba mali na kuuwa? Usiisaliti nchi yako kwa ujinga mbwa wewe.Hata mimi ni chadema mkubwa ila siwezi kuwa mjinga kama wewe nikaisaliti nchi yangu.Matatizo ya ndani hayawezi kunifanya niisaliti Tanzania.Mimi ni mchungaji ila vita vikitokea na tukazidiwa niko tiari kuifia nchi kwa kwenda vitani.Yaani unaiuza nchi yako kwa kupewa pesa,wewe Yuda Iskariot mtoto wa malaya.KIKWETE JAPO SIPENDI UNAVYOENDESHA NCHI ILA SWALA LA KAGAME NIKO NA WEWE BEGA KWA BEGA.Hilo gazeti lilitoa maoni kama hayo lifungiwe.
 
Upo sahihi dhahabu hizo ndio zinazoa mtoa roho kam waliokufa wameshakufa wahutu ile ni inchi yao pia nilishani kama rais yy ndio alitakiwa kukomesha hili kwa faida ya vizazi vya mika mia ijayo.kuna kitu anakipata aombwe radhi kwa lipi baya waswahili wanasema JERI MWENZIE KUSUDI,UKISIKIA KICHEFU CHEFU TAPIKA SIO KULA NDIMU,kwani kagame alisemea chumbani huku milango ikiwa imefungwa?Jk ni wetu watuache tusigane nae wenyewe hapa ni utaifa.SINGI VITA WALA C PENDI kwakuwa mimi nitakuwa ni mmoja wa waathirika lakin Kagame kwa hili kateleza na cjui kwanini walimuingiza kwenye EA.???Rais Kikwete alimtaarifu Rais Museveni kile walichojadili baada ya yeye kuchelewa kufika. Alisema ni vema serikali za Rwanda na Uganda zikakaa na kuzungumza na makundi ya waasi wa nchi zao, na kulitolea mfano kundi la waasi wa Rwanda la FDLR.Inasemekana ushauri huo uliungwa mkono na Rais musevi,lakini ulipingwa vikali na Serikal ya Kigali.
Ina mana walishakaa chumbani kama ulivyotaka lakini yeye ndio kawa bedui wa kuyatoa NJE
Huyu George ni mjinga kupita kiasi ila naamini kapewa pesa aandike upuuzi huu.Anasaliti haki,anaunga mkono ujambazi na mauaji? Anasaliti nchi yake.
 
Liwalo na liwe, asithubutu kufanya upuuzi unaomshauri. Na hii oparehseni ya kuwarudisha wanyarwanda aifanye bila kuangalia nyani usoni. Tumeshachoka!
 
George Maziku ni dhaifu kuliko dhaifu original!!! Unafikiri akiomba radhi Kikwete itakuwa kaomba yeye binafsi au Tanzania ndio itakuwa imeomba radhi?

Ukwendeeee alaaaa!!!
 
hivi rwanda inaizidi kondoa kwa ukubwa?
hebu acheni kuwaogopa wanafanya mambo mengi sana tunawavumilia. tusikubali kila siku tuonekane wajinga bana tumechoka tumetumia raslimali zetu nyingi kwa ajili yoa kwa muda mrefu halafu tuendelee kuwanyenyekea kwa lipi zaidi?
kama biashara tunayoogopa kuikosa rwanda si ya maana sana kama ya kongo kama itakaa vizuri.
hivyo msiogope kivile kuwa vigari vyenu vya mizigo vitakosa safari na biashara
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom