Rais Kikwete ateua bodi mpya ya TANESCO

Ngali Ngali Ngali............................................!Inatosha bana![/COLOR]
Sawa inatosha lakini huo ndiyo ukweli. Kwa jinsi TANESCO inavyoendeshwa utafikiri haina bodi ya wakurugenzi. Kama inashindikana kubadilishana bodi za TBL na TANESCO, basi timu nzima ya nishati na madini ihamie viwanda na biashara na ile ya viwanda na biashara iende nishati na madini.
 
Du! Nahisi harufu mbaya! Tanesco watazidi kuwachumia wanasiasa mpaka lini? Kama kila rais anaweka boardmember watakao mpa ulaji? Toka enz za mkapa board ya tanesco imeonekana haina malengo mengine zaid ya kuchota pesa. Kwa taarifa tu mpaka sa tanesco inakadiriwa kukusanya 45bil per month, zote zinaishia kwenye matumbo ya mafisadi haswa kwenye malipo ya aina ya akina Jairo. Mkurugenz wa tanesco anatishwa kila kukicha!
 
Ingekuwa vyema angewapa Jeshi waendeshe TANESCO maana hawa ndugu zetu wa uraiani wameshindwa kabisa.

Nakubaliana nawe, wanajeshi hawewezi kua-afford kuwa lax katika kutekeleza kazi zao, wako makini sana. Lakini vile vile uraiani kuna baadhi ya wenzetu waliyo makini na wabunifu sana katika kazi zao na uendeshaji wa mambo, mimi binafsi huwa na admire mzalendo mwenzetu BAKHERESA sijuhi jina lake vizuri - we anagalia anavyo endesha kampuni zake ambazo ni nyingi tu zimetapakaa Africa Mashariki na Kati, sijawahi hata siku moja nikasikia wafanyakazi wake wamegoma au kampuni zenyeshewe zina mushkheri wa kutolewa kwenye vyombo vya habari; swali ni je huyu mzalendo anatumia mbinu gani kuendesha kampuni zake kiufanisi?

Mashirika yetu ya UMMA have a lot to learn from kutoka kwa mwenzetu huyu, Bakheresa ana talent za ajabu katika uendeshaji wa mambo, mimi kama ningekuwa na uwezo wa kumshauri JK basi ningemuomba awasiliane na Bakheresa na kumtehuwa kuwa Board Chairman wa TANESCO walao kwa muda wa miezi sita (afanye kazi sambaba na mwanajeshi huyo) , JK ampe Bakheresa a blank cheque ya kuhisuka upya TANESCO, atumie talent zake katika utehuzi wa wakurugenzi na watu muhimu wa kuendesha shirika hilo, asihingiliwe na wana siasa au mawaziri katika ufumuaji na usukaji upya wa TANESCO maanake watanzania tu mahili sana katika kuweka SPANA kwa mtu yeyote anayeonekana kumudu mambo kiufanisi watamuwekea fitina za kila aina hili ashindwe.

Nimuzungumzia kuwabadilisha wakurungezi kwa kuwa ndio huwa na kazi za kudumu siyo kama mawaziri ambao kazi zao ni za muda tu, mashirika ya UMMA yamekufa kutokana na wakurugenzi wao kufanya mambo kienyeji mno, kukaa kwao shirika moja kwa muda mrefu unawafanya kujisahau na kuwa wabishi na wasio kubari kubadilika - ni vigumu sana kubadilisha mind set za jamaa hawa - labda niwe muwazi hapa kwamba siyo kila mkurugenzi ni mzigo la hasha lakini wengi wao hawatufahi hata kidogo.

Miezi sita inatosha kwa Bakheresa kufanya mahajabu katika shirika la TANESCO - his actions speaks volume kwa mzalendo huyu, hilo likishindikana basi JK ampe January Makamba wizara ya nishati na madini, najuwa watu watahanza kuleta mambo ya udaku kuhusu January ambayo mengi ni huzushi mtupu, tuangalie hatua ambazo January amewahi kuzichukuwa na kuwa muwazi kuhusu madhala yanayo tokana ukosefu wa umeme wa kuaminika nchini alichukuwa RISK kubwa sana kuwabana wahusika na alikuwa anasema ukweli na aogopi mtu, katika uchunguzi wake ambao aliwahi kufanya na habari alizowahi kupata kutoka kwa wananchi kuhusu Shirika hili la TANESCO, naona atakuwa amepata treasure trove kubwa ya kuweza kuhisuka upya TANESCO kwa kuwa amekwisha juwa fika udhaifu huko wapi. JK asipate kigugumizi kwa kudhani kwamba labda akimutehuwa January watu watamlaumu, afumbe macho afanye kama dhamila yake itakavyo mtuma hasijali lawama cha muhimu afanye analo ona liko kwa best interest ya Taifa letu na uwezo huo JK anao SANA.
 
Hivi hii tabia ya kurundikia madaraka wastaafu itaisha lini? Mtu akistaafu ina maana anatakiwa kupumzika awaachie wengine ambao bado wako active waendeleze kusukuma gurudumu la maendeleo. Viongozi wetu hawawezi kuona watu wengine wenye uwezo wao huwaona wastaafu tu hasa wa jeshi.
 
Sasa huyo Ret. Gen. Mboma ndiye mwenyekiti wa board ya wakurugenzi wa TPDC ambayo pia ipo chini ya Wizara hiyo hiyo ya Nishati na Madini chini ya Ngereja.

Hilo Shirika mmoja tu anapata nalo taabu linamshinda, na sasa anapewa jingine TANESCO lenye matatizo lukuki!!!!

Nchi itafika kweli tunakotaka kwenda? Je, ni kweli watanzania Million 40 hatuna watu wengine wanaoweza kuwa wenyeviti wa hiyo board na waka perform vizuri badala ya kurundikiana vyeo mtu mmoja?[/QUOTE
 
Ingekuwa vyema angewapa Jeshi waendeshe TANESCO maana hawa ndugu zetu wa uraiani wameshindwa kabisa.
Hata hao raia wakipewa uhuru wa kuliendesha shirika kitaalamu, bila kuingiliwa na wanasiasa, wanaweza kulifanya liwe la mafanikio
 
Baruany Elijah A. T. Luhanga Huyo jamaa alikuwa CEO wa Tanesco from 1996 -2002 ? Karudi kufanya nini tena. hama kweli Bongo tambarare
 
Hongera M/kiti mteule. Uzoefu wako wa TPDC usaidie kuleta mabadiliko TANESCO. Ujasiri wa kuamua mambo ni muhimu kwenye shirika lenye ukiritimba kama TANESCO.
 
Kurudi kwake kutasaidia kurekebisha makosa aliyofanya akiwa madarakani na yale aliyoyaona akiwa nje. Sometimes uzoefu unahitajika katika mambo haya.
 
Baruany Elijah A. T. Luhanga Huyo jamaa alikuwa CEO wa Tanesco from 1996 -2002 ? Karudi kufanya nini tena. hama kweli Bongo tambarare

Kurudi kwake kutasaidia kurekebisha makosa aliyofanya akiwa madarakani na yale aliyoyaona akiwa nje. Sometimes uzoefu unahitajika katika mambo haya.
 
Kweli kabsa meku, maana wanyaji wa bia ni wengi kukukukukukukuliko wateja wa tanesco. Aika monoko.
No siyo jeshi, angechukuwa bodi ya TBL maana bia hazijawahi kuwa za mgao. Hii inaonyesha wapo kibiashara zaidi
 
Back
Top Bottom