Rais Kikwete atembelea msikiti wa Sultani Qaboos Grand Oman

Nao huo si sehemu ya udini? Unatumiaje pesa za walipakodi kutembelea misikiti. E mungu tanzania ya leo udini,udini,udini utaangamiza taifa hili.
 
Mnh! huko farasi si jadi yao, labda watampandisha kwenye ngamia maana kuna wale walio mpandisha kwenye bembea. Xuma hebu nitafutie cacico anaweza kuleta mawazo mbadala ya namna ya kupunguza hizi safari maana kama ni kupiga picha tumeshapiga saaana tu! kuanzia zile za viongozi wenzetu mpaka zile za wachezaji na wasanii. Kama ni kupanda kwenye vyombo mbalimbali basi tumeshapanda sana tu! kuanzia gari, ndege, farasi na hata bembea! Kama ni zawadi tushapewa saaaana tu mpaka jezi! Sasa nini kimebaki jamani?

Hebu tusaidieni tupunguze hizi safari, tutulie nyumbani na kutatua matatizo yanayotukabili. Matatizo ambayo wengi wanayaona ni madogo lakini baada ya muda si mrefu tutakuja kujuta maana tutakosa pa kukimbilia! Leo kanisa moja linachomwa watu wanaona ni sawa tu. Linaongezeka la pili, la tatu na kuendelea bado inaonekana ni vurugu tu za vijana wasio na kazi. Watu wanauawa mikononi mwa vyombo vya dola vinaundwa vijitume na kutoa vijiripoti siku zinaenda. Sasa RPC anauawa na tena FFU bado tutaendelea kujivunia kuwa tuna nchi ya amani na utulivu! Aaaghrrrrrr!

Nimechoka mie bora nijiendee zangu Chit Chat au Jamii Photos nikapoteze mawazo!

Mbona safari bado we unafikiri tutweza bila mzee kuenda kupiga picha na kwa taarifa yako bado KUTELEZA KWENYE BARAFU!!!

Kwanza tulishaambiwa liwalo na liwe nini tunasubiri lakini????
 
Mbona safari bado we unafikiri tutweza bila mzee kuenda kupiga picha na kwa taarifa yako bado KUTELEZA KWENYE BARAFU!!!

Kwanza tulisha waambiwa liwalo na liwe nini tunasubiri lakini????

Kaka unazidi kuzika tumaini dogo lililobaki.
 
EMT sina uhakika kama Hayati Nyerere na Mkapa waliwahi kufanya ziara nje ya nchi kutembelea nyumba za ibada. Viongozi wetu inabidi wafike mahali watofautishe mambo ya binafsi (personal interest) na yale ya Taifa. Vipi Mh Kikwete ingetangazwa kamba yuko kwenye mapumziko binafsi huko Oman akafanya hayo yote bila kupewa "Public coverage"?
 
Last edited by a moderator:
1350503365044013000.jpg
1350503345024010900.jpg

Pichani Rais Kikwete akitembelea msikiti wa Sultani Qaboos Grand na pia akitia saini kwenye kitabu cha wageni.

Rais Kikwete ameendelea na ziara yake nchini Oman ambapo jana alitembelea msikiti wa Sultani Qaboos Grand ulioko Bausher, nchini Oman. Katika ziara hiyo, Rais Kikwete alipewa historia ya msikiti huo ambao unajumuisha chuo cha masomo ya Kiislamu, sehemu ya kufanyia mihadhara na sehemu nyinginezo.

Aidha Rais Kikwete alijionea mwenyewe usanifu wa jengo la msikiti wa Sultani Qaboos Grand uliojengwa kwa usanifu mzuri wa Kiarabu na Kiislamu.

Taarifa inaendelea kusema kuwa Rais Kikwete alijionea mwenyewe majukumu ya msikiti huo katika jamii na katika kufikisha ujumbe wa kuvumiliana kwa mujibu wa dini ya Kiislamu (President Kikwete familiarized himself with the role of the mosque in the society and in conveying the tolerant message of Islam).

Kabla hajamaliza ngwe yake atajenga msikiti kama huo huko nyumbani kwake Msoga/Chalinze.
 
Back
Top Bottom