Rais Kikwete arejea ghafla ikulu ya Dar es salaam

Status
Not open for further replies.
Honestly, sioni haja ya kumsifia Rais kurudi huo ni wajibu wake akiwa kama Rais wa nchi.
Mungu awatie nguvu wafiwa, na i hope watu watawajibishwa kwa sababu hii ajali ni matunda ya uzembe, meli ya watu 645 inabebaje watu zaidi ya 800? kwani hamna sheria za kuzuia overloading na je hamna watu wanaosimamia haya mambo ya usafirishaji? for once, Tanzania isimamie uwajibikaji.
 
kwa kweli TZ ni aibu vpu. kuanzia mabasi ya mikoani bado yanajaza na trafick hawakohoi. akishasimamisha gari atapanda kukagua then atawaona waliosimama kwa macho yake, kifuatacho anashuka na kupewa buku mbili yake basi linaondoka. kwenye vidaladala ndiyo usiseme. mtu anakuwekea kwapa puani kwako. imagine. ilinibidi nisave hela ili kupata usafiri before nyumba kwa kuwa sipendi kusondekwa kama mihogo. hapa arusha watu wa daladala za kutoka njiro wana mtindo wa kukatisha route. wanaishia sabena na si stendi. watu wakiambiwa hapa ndo mwisho shukeni wala hawakatai. wanashuka. mimi nilikuwa nakatalia ndani ya gari hadi wananipeleka stand nikiwa peke yangu. japo kuna siku walitaka kunifanyia fujo lakini nikawazidi nguvu. point yangu ni kwamba, watz tumezidi upole au umbumbumbu. pia serikali imejaa wazembe wakubwa na wanatumia ujinga wetu kujinufaisha wao bimafsi. kwenye zike sled za wamarekanikuna m6ja kasema wananchi wanashinikiya wahurika kujiuzuru, mwingine kasema 3rd world kwa ninh janga likitokea wananchi ndo wanataka mhusika ajihuzuru, mwingine kasea inawezdkana walisema kabla na ilikuwa ndiyo mpango ila mhusika anaamua afanye kuchelewesha ili akusamye hela yake kwanza na ndo matokeo haya tunayoyaona. hapa jirani yetu kenya na uganda tu madaladala yote hayazhdishi abiria hapa ninh kinatushinda? sheria zipo na zipo wazi. na kama tusingelundhjana kwenye mabasi nauhakija mabasi yangezunguka kwa haraka zaidi na watu wasingdchelewa kama wanavyodhani. sheria zifuatwe na tusiwd wa kusubiri majanga ndiyo tume ziundwe. hazitusaidii tena kwani watu tushapoteza tayari..
 
This tragedy is a deja vu of the MV Bukoba,we didnt learn the lesson... watu wanajaza mizigo na abiria kupita kiasi na mamlaka husika hazichukui hatua stahili.. shame on this nation!!!
 
Waafrika kuthamini maisha yao ni jambo la mwisho na hasa Tanzania ndiyo kabisa .I always wonder kuona traffic njiani lakini mbele yao yapita lori au gari halina taa za nyuma .Daladala haina taa na kwa ndani juu kichwani ni mabati natupu .Hakuna hata taa za kuonyesh mtu anakata wapi .Maajabu ni kwamba kun basi la polisi Dar aina ya Layland nimeona haina handle ya kufungulia mlango wa dereva , baadhi ya daladala dereva anafunga mlango kwa mpira au kamba yet hakuna shida na watu hawa lalamiki .Speed za daladala na malori utashangaa na ajali zinatokea watu wanakufa yet hakuna serikali inasema lolote.
 
Kufuatia msiba ulio likumba taifa,yule bingwa wa safari duniani ndugu yetu kabisa JK imemubidi ageuke kutoka Nairobi!
Hivi kikwete muda wote yuko nje ya Tanzania?
Kila event inayotokea yuko ughaibuni.
CNN, BBC, Aljazeera wameirusha hewani ajali ya meli wangemtafuta huko America (sijui alikua anaenda kuzurura wapi) wamhoji...
 
Kurejea kwake hakuna maana yeyote, hivi hiyo mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu unafanya nini? makosa yale yale - mazingira yale yale yaliouwa mamia mwaka 96 tunayarudia tena.

Kuna haja ya kuwa na hii mamlaka ambayo haiwezi kusimamia hivi vyombo hasa vya majini kama vina viwango vinavyokidhi kusafiri majini na pia vinachukua idadi ya shehena inayotakiwa - hii pamoja na abiria.?

Na hili tutamsukumia mungu kama tulivyozoea -- yaani na TUME juu tumeiunda. Hivi ile riporti ya TUME YA MV Bukoba ipo wapi? je ilifanyiwa kazi? Ama kweli viva Tanzania.......

Sorry Umeme umekatika siwezi kuendelea kuandika, maji nayo tangu juzi hatuna huku mbezi juu.......Kuoga kwetu ni starehe.
 
<br />
<br />
Ameonesha moyo wa kujali na huruma kama kawaida yake. Sasa mbona magwanda wao wanaendelea na kampeni tu Igunga?

Hahahaaa, nyie Magamba mna akili kweli; Uzembe wenu kazini unasababisha ajali na asara kubwa, ajali zikitokea mnatangaza mapumziko!!!!!! Hayo mapumziko ni bora basi mngekuwa mnaenda kuwajibika eneo la tukio, siyo kulala wakati posho zinaingia\!!! Akili mbovu kweli!
 
AGIZO LA MUNGU KWA BINADAMU 'KUSHUKURU KWA KILA JAMBO':
KAMA SI MAREHEMU WETU WA AJALI YA PEMBA KUMGOMEA RAIS KIKWETE KWA SAFARI ZAIDI UGHAIBUNI, MAMILIONI HAYA YA GHARAMA WALIPAKODI TUNGEJIOKOLEA WAPI?????


Vipi sasa jamani inamaana baada ya Mhe Kikwete kulazimishwa na huu msiba wa kitaifa kule Pemba, vipi sasa walau balozi wetu huko nchini Marekani ataweza kupata fursa yake stahiki kuwakilisha serikali yetu kwenye hiyo minuso miwili ya PEACE CORPS na kule kwenye mkutano wa DICCOTA na kutuokolea walipa kodi gharama kubwa ya hela za usafiri, chakula, malazi, na posho kwa ujumbe wa zaidi ya watu 50 sio????????????

Ama kweli kila baya na afadhali yake; pengine ndio maana Mungu Muumba wetu ametuficha ujumbe mzito sana nyuma maneno 'SHUKURUNI KWA KILA JAMBO' eeeehhhh??????????

Hakika siku zote sie viumbe dhaifu hukumbuka tu na kukubali KUSHUKURU katika jema lakini baya linapotokea watu hatukawii kuanza ubishi ndani ya kughairi kwetu kwenye ukimya wa KUTOKUTEKELEZA agizo hilo la Mola wetu.

Ni vema waumini wa dini zote tukajifunza kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jambo, zuri au baya, kama maandiko yanavyotuagiza. Kwa mara nyingine, Marehemu zetu AJALI YA PEMBA pumzikeni kwa amani!!!!!!!!!
 
Duh Mbongo unapenda starehe kama mtu wa Burnei!! Siku tatu kulala tu na kuomboleza, hakuna kitu kama hiyo. Tuchape kazi kuwaenzi wenzetu

Mwita25 wakati mwingine wanifanya niwaze kama wewe ni great thinker au ni great stinker ?
 
Amerudi kama wajibu wake na tunashukuru kwa hilo. Na nyie wanaCDM sasa tafuteni kingine cha kupigia kampeni huko Igunga, si mlitegemea yeye kutokurudi ndio iwe dili huko.
 
Poleni wafiwa na tunawatakia uvumilivu mwema kwa wale wanaosubiri ndugu zao!

Vichekesho tupu hivi. Unajua ninapo sikia jina la kikwete napata aibu tupu.

Huyu ndio mzee wa majanga Tanzania. Kama janga la Gongo la Mboto, Mbagala, Umeme, Maji na Umaskini sijui huyu jamaa kazaliwa wapi? Maybe nisingehangaika ku-comment kwenye hii thread but I have things to say too.

Unakumbuka serikali ya mkapa wakati wa MV Bukoba na report kama ilitoka kwa wananchi, kuna yeyote yule alichukuliwa hatua? Ilikuwa kama ajali zingine za Tanzania na hii itapita kama wale wana-ccm wanavyotaka na hii si ya mwisho! Wananchi watapewa siku tatu za maombolezo ya titanic. It's all about leadership in Tanzania na hata kama watakuja wengine wakasema ni rushwa au ni uzembe but tutarudi palepale kwenye ofisi ya raisi na uongozi wake. I bet you kuna mtu ata-respond katika hii thread kusema 'kwani kikwete angefanyaje hapa na asingeweza physically kuzuia haya'
Leaders are required to protect their people na zaidi ni kuwa na uwezo wa ku-forecast the concerns and prepare the people. Kikwete anauwezo upi? Nothing nothing nothing ......
http://www.tzaffairs.org/1996/09/tanzanias-titanic-disaster-–-mv-bukoba/

Naona ni wajibu hao kwanza. Kiongozi wa nchi ananafasi kubwa ya kuangalia priorities na ku-safe guide inchi, hili ni jambo la kwanza. Pili kutokana na ajali nyingi kujirudia Tanzania, inaonyesha wazi hakuna wanajifunza kikubwa hakuna enforcement yeyote kuzuia wasimamizi au owners wa hizi biashara kama usafiri kutojaza wasafiri wengi ili kupata faida au laws zinazofuatwa. Ukifuatilia utakuta hakuna records za wasafiri na leo wana-destroy kila kitu ku-avoid ushahidi wakishirikiana na polisi. Loop holes zipo kila mahali Tanzania kuanzia mtoto anapozaliwa muhumbili mpaka huyo huyo mtoto akikuwa kuwa mtu mzima, tunapambana na uzembe na u-ccm kila mahali. Congrats kikwete kwa uongozi bora!

Nawatakia wanachama wa ccm furaha tele na uongozi bora wa kikwete! Kikwete na ccm mtasema nini this time? Tunajua ukweli hii ajali ni avoidable na haitakuwa accountable kwa mtu yeyote yule serikalini ikiwemo cuf.

Ndugu yangu Mtanzania,umenena vema,lakini jambo moja tunapaswa kulijua ni kuwa hizi ni kafara wanazozitosa.na shariti la kwanza kutowachukulia hatua wahusika,kwani wanakuwa wanajua wanachokifanya.jambo moja tu wahusika pelekeni salamu kwamba mwaka huu imekulaa kwao.
Mungu wa Israel hajalala usingizi,lazima zitapikwe kafara zote.
 
Amerudi kama wajibu wake na tunashukuru kwa hilo. Na nyie wanaCDM sasa tafuteni kingine cha kupigia kampeni huko Igunga, si mlitegemea yeye kutokurudi ndio iwe dili huko.

sina uhakika kama bado anauza mjadala.kwa maana nyingine hazungumkiki,wananchi wamesha mdelete kwenye mawazo yao.
 
Mimi nilifikiri tunaelezwa kurejea kwa V. d. G kutoka alikokwenda baada ya mkutano wa Perth, Australia. Hatujamsikia tokea mkutano uishe. Alipoondoka nchini tulihabarishwa, lakini tokea mkutano uishe hatuna habari mpendwa wetu yuko wapi!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom