Rais kikwete ana nia njema lakini anaangushwa na watendaji wake - hii imekaaje?

Kidudu Mtu

Member
Nov 7, 2009
64
0
Kila wakati nasoma maoni ya baadhi ya watu wakidai eti Rais Kikwete ni kiongozi mzuri mwenye nia njema ya kuwaletea maendeleo wananchi wake lakini "anaangushwa tu na watendaji wake ambao hawatekelezi yake anayoyataka Rais huyo".

Je ni sahihi kuelekeza lawama kwa watendaji walio chini ya Rais Kikwete au lawama zote zinapaswa kubebwa na Rais Kikwete kama mtendaji mkuu?
 
Hii mbona imeshaletwa na kujadiliwa hapa?

For the sake of the records.

Mtu yeyote anayesema rais ana nia njema ila anaangushwa na watendaji wake inabidi ajue.

1. Rais ndiye mwenye dhamana na wajibu wa mwisho katika nchi, rejea hotuba ya Nyerere aliyosema kila akitembea akiona umasikini, wananchi wanakwendas nusu uchi, ni kazi yake, urais si mchezo, ikulu si pa kukimbilia.

2. Katika system ya top down kama ya Tanzania, rais ni kama demi god fulani hivi.

3. Rais ana nguvu ya kujua jinsi watendaji wake wanavyofanya kazi.

4. Kama rais hajui watendaji wake wanavyofanya kazi basi ni makosa ya rais mwenyewe kutokujua hili na hana wa kumlaumu.

5. Harry Truman said it best, "The buck stops at my desk". Vimbwanga vyote vitakavyotokea kwa jina la Tanzania rais ana dhamana ya mwisho.


Hizi habari za "rais ana nia nzuri lakini anaangushwa na watendaji wake" zinaletwa na watu wa aina mbili tatu hivi.

1.Mainly wazee ambao wanajua rais bichwabuyu, lakini kwa mujibu wa propriety system ya kitanzania rais ni kama mungu-mtu fulani na huwezi kumchamba wazi wazi.

2. Vijana na wazee wanaowa parrot wazee hao wa hapo juu bila kuelewa kwamba hii ni euphemism, na kwamba kwa kweli kusema "Rais ana nia njema ila anaangushwa na wateule wake" ni kusema rais hajui kuteua watu safi, na by induction rais mwenyewe either si msafi au si makini.

3. Watu wa serikali na wanaotegemea kuwa wa serikali wanaoogopa vibarua kuota majani au kutopata largesse na patronage ya rais.
 
Nafikiri Rais kwa nafasi yake anayo mamlaka ya kumwambia fulani toka na wewe ingia. anao hata uwezo wa kuamuru kijiji fulani kiteketezwe kipotee kabisa. sasa kama ana watendaji wabovu na hawezi kuwawajibisha, unasemaje yeye ni mzuri? Angekuwa na nia nzuri na nchi hii angewatimuatimua hao wote wanaoitwa watendaji wake wabovu. Kikwete hana ni nzuri na nchi yetu. Tatizo anacheka hata na wale wezi wa Rasilimali za nchi yetu na hiyo ndiyo sababu watu wanasema asigombee tena. maana tunatarajia Rais aweze kumwajibisha yeyote, popote.
 
Kama anania ya dhati angewafukuza hao watendaji na aweke wengine.
Kwa maana hiyo watendaji wake wamemsaliti? Au hana mamlaka ya kuwafukuza?
 
Kwani aliyewaweka hao watendaji alishakufa na haiwezekani kuwaondoa? JK hana nia ya kuwatumikia waTZ aliwaweka hao watendaji akijua hawawezi ila ni marafiki zake tu. Au he undermined the presidency or hajui analotakiwa kufanya as a president
 
Tulishasema kwamba maneno kama hayo huwa ni tabia ya kujikomba inayotokana na mfumo mbaya wa utawala.

Mfalme yuko uchi lakini anaambiwa kavaa.

Inabidi aambiwe hivyo kwa sababu ana madaraka makubwa kuliko na ili nibaki ktk nafasi yangu, namuondolea makosa yake.

Kwa akili timamu za binadamu unawezaje kusema ni mzuri lakini anashindwa kuwachagua mawaziri wazuri, wakurugenzi wazuri, majkatibu wazuri, n.k.

NI MZEMBE
 
Watendaji wake wanamwangusha? nani aliwachagua? na wanariport kwa nani? kama hawafai mbona anawakumbatia?
 
Rais anapokumbatia wanomwangusha, huyo naye si mwangukaji? Hivi unaweza kuweka kaa la moto kiganjani, na bado ukasema tatizo ni kaa la moto lililopo kiganjani ndiyo tatizo, hali ukizidi kuungua. Lazima uwe ni mwendawazimu nambaki -1.
 
Kila wakati nasoma maoni ya baadhi ya watu wakidai eti Rais Kikwete ni kiongozi mzuri mwenye nia njema ya kuwaletea maendeleo wananchi wake lakini "anaangushwa tu na watendaji wake ambao hawatekelezi yake anayoyataka Rais huyo".

Je ni sahihi kuelekeza lawama kwa watendaji walio chini ya Rais Kikwete au lawama zote zinapaswa kubebwa na Rais Kikwete kama mtendaji mkuu?
MIMI naona anajiangusha mwenyewe!hao watendaji ALICHAGULIWA?au alijichagulia.kila kukicha NAPANGUA BARAZA,KILA KUKICHA NAPANGUA BARAZA!upuzi mtupu....
 
Ni kweli the buck may stop at JK. Kwa mazingira ya Tanzania kuna tatizo la kisheria na utaratibu. Hebu nitoe mfano. Mfumo wa nchi yetu wa the public service delivery system unategemea umahiri na uweledi wa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya/Mji/Jiji/Manispaa. Ideally rasilmali pesa, rasilimali watu na kadhalika vinapelekwa kwenye Halmashauri kutoka Serikali Kuu (Central Government) kupitia bajeti ya kila mwaka wa fedha. Hizi ndizo zinatumiwa na sekta mbalimbali kama vile afya, maji,barabara n.k. Afisa Mtendaji Mkuu ni Mkurugenzi ambaye ndiye msimamizi wa matumizi ya mafedha na rasilimali za halmashauri. Kama utendaji wake hauridhishi anayepaswa kuwa jicho la Rais katika ngazi hiyo ni Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa. Huyu DC ndiye anaetakiwa kumkabili huyo Mkurugenzi kwa kumwajibisha na kama anakuwa mbishi na mkaidi basi anapeleka taarifa kwa Mkuu wa Mkoa kuwa mambo pale kwenye Halmashauri yake hayaendi iapsavyo. Nae RC atambana Mkurugenzi. Akikaidi basi anamripoti Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambayo iko ofisi ya Waziri Mkuu. Sasa pale ndipo watamchukulia hatua za kinidhamu dhidi ya huyo Mkurugenzi. Jamani hiyo ndiyo ideally yaani kinadharia.

Hatua atakazochukua TAMISEMI dhidi ya Mkurugenzi zimewekewa taratibu na kanuni za kisheria ambazo Waziri wa TAMISEMI akisaidiwa na Katibu Mkuu wake anapaswa kuzizingatia. La sivyo asipozizingatia Mkurugenzi akienda Mhakamani Waziri anaweza kujikuta anashindwa. Utaratibu huu umeigharimu sana taifa hili kwa sababu imebidi tubakie na watendaji wabovu. Sana sana kuwafukuza ni ngumu kwa sababu wanalindwa na hizi kanuni kwa hiyo anaweza akapewa kazi nyingine. Maana huo uoza unaendelea kuathiri sekta nyingine ya serikali.

Sasa nije kwenye mada. Hapo Rais anaweza kufanya nini. In theory, kwa sababu anavyo vyanzo vingine vya kumpatia taarifa kama vile Usalama wa Taifa, wananchi wa kawaida, magazeti anaweza kuchukua hatua. Lakini kumbuka huyu Rais anayo miaka mitano ya kutekeleza Ilani yake. Kwa hiyo anayo monitoring system ambayo inaangalia utekelezaji. Je reality ikoje?

1. Asilimia kubwa ya bajeti inategemea wafadhili. Mpaka pesa ije na haiji yote unakuta na miezi nayo inayoyoma. Hii inaathiri performance ya serikali.
2. Asilimia kubwa ya watendaji wetu ni mediocre. Why? Wengi wao elimu zao zinatokana na mfumo wa elimu mbovu wa kipindi cha awamu ya kwanza hadi ya tatu. What we sowed in our education system is what we reaping now in what we see as mediocre performance ya serikali.
3. Watendaji wengi wana mahusiano ya kindugu tena ya karibu na wakubwa wa sasa na wawaliopita awamu zilizotangulia ambao ni watoto wao wa kuzaa au wa ndugu zao au mashemeji zao. Na hawa wamo katika idara nyingi tu za serikali kama vile polisi, magereza, idara ya usalama wa taifa, TRA, BOT, Wizarani ndiyo usiseme. Namjua Mkurugenzi mmoja ambaye anaye girlfriend ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara mojawapo serikalini. Sasa katika hali hii unafikiri wabovu hawa hata ukiwachukulia hatua kali wakati system nzima imejaa hao hao unafikiri it can work.

Mimi nasema hata JK na CCM watoeni kwenye madaraka waje CHADEMA hakuna lolote watakalofanya. Kwa sababu we will just have a change of the political leadership and not the Civil (Public) Service System. Sawa CHADEMA itabadilisha Makatibu Wakuu, Wakurugenzi wa Wizara na kadhalika. Lakini unafikiri itawatoa kutoka wapi kama siyo kwenye kundi hili hili bovu. Na watakapokuwa wanatawala wakiona mambo hayaendi kama ilivyokuwa kwa CCM wataanza na wao visingizio unajua hii ni kutokana na miaka mingi ya ukiritimba wa CCM tupeni muda wannchi. Awamu ya Tano ya Sita mpaka milele. Hali ni hiyo hiyo. Tujifunze kutoka Zambia, Malawi. Kwa hiyo wao CHADEMA wachukue serikali halafu tutakuwa na CCM ile ile in style and rhetoric but different attire.
 
Back
Top Bottom