Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
Aliyekuwa mkuu wa itifaki Bwana Abdul Sisco amekuwa balozi mpya wa Tanzania Malyasia.
Rais pia ameteua mkuu mwingine wa itifaki.
Source: Ikulu, na habari zaidi tusubiri magazeti ya kesho!
Hongera sana Sisco. Mimi nakupongeza sana.
Lakini labda naomba kuuliza kidogo je kuna vigezo vyovyote vinavyotumika katika kuchagua mtu kuwa balozi?
Je mtu yeyote Tanzania anaweza kuwa Balozi?
Je kila mtu akipiga Mkwara akapewa madaraka, itakuwaje kama nafasi zitakuwa zimeisha? Si ndiyo mwanzo wa kushikana mashati?
A well deserved appointment for a Civil servant of his calibre!
Mwanadiplomasia!
But what are the motives for bringing this to Jukwaa la siasa?
Curious?
Rais Kikwete ateua Cisco, Biswaro mabalozi Malaysia, Brazil Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete amewateua mabalozi wapya kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Brazil na Malaysia.
Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imesema kuwa rais amemteua Balozi Joram Biswaro kuwa balozi wa Tanzania nchini Brazil na Balozi Abdul Cisco Mtiro kuwa balozi wa Tanzania nchini Malaysia. Uteuzi huo utaanza mara moja.
Kabla ya uteuzi huo, Balozi Biswaro alikuwa Mkurugenzi Idara ya Asia na Australia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Mtiro alikuwa Mkuu wa Itifaki katika wizara hiyo.
Pia Rais Kikwete amemteua Anthony Itatiro kuwa Balozi na Mkuu wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Itatiro alikuwa Mnikulu katika ofisi ya Rais.
Ningependa kusahihisha tu kuwa Cisco Mtiro tayari alishateuliwa kuwa Balozi tangu enzi za Mkapa wakati alipokuwa anaiwakilisha Tanzania katika nchi zinazozungumza kifaransa kule West Africa na kituo chake cha kazi kilikuwa Nigeria
labda waandishi wetu wangeuliza hili wangeambiwa lakini ndio hivyo tena
Vile vile ningependa kuchukua fursa hii kuwaweka wazi kuwa HALISI si credible pamoja na sources zake kwani mwezi wa pili alikuja humu na thread iliyodai kuwa JK AMFUKUZA KAZI CISCO lakini nilipombana hakuweza kuja na jibu linaloeleweka