Rais Kikwete amteua Bibi Mwanahamisi Omari Kitogo kuwa msaidizi wa Rais katika Huduma za Jamii

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua BIBI MWANAHAMISI OMARI KITOGO kuwa MSAIDIZI WA RAIS, HUDUMA ZA JAMII.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue leo, Jumanne, Mei 8, 2012, mjini Dar es Salaam inasema kuwa uteuzi huo umeanza Mei Mosi, mwaka huu, 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Bibi Mwanahamisi Omari Kitogo alikuwa Mkadiriaji Ujenzi Msaidizi (Assistant Quantity Surveyor) katika Kampuni ya COWI, Tanzania.

Imetolewa na
:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu
.Dar es Salaam.
8 Mei, 2012
 
Hii nayo ni kati ya kali za mwaka; kutoka mkadiriaji majengo msaidizi tena wa kampuni binafsi hadi msaidizi wa rais! Ndiyo mapigo ya JK hayo.
 
Tumpe ushirikiano

ushirikiano upi? naona jamaa kaamua kugawa vyeo kama njugu sasa , kila siku mtu anateuliwa, kesho uatasikia ndugu MS ateuliwa kuwa Msaidizi wa ......kuhusu mambo yanayojadiliwa JF
 
Katika wale walioapishwa juzi huyu bibi alikua amesahaulika nini?
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua BIBI MWANAHAMISI OMARI KITOGO kuwa MSAIDIZI WA RAIS, HUDUMA ZA JAMII.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue leo, Jumanne, Mei 8, 2012, mjini Dar es Salaam inasema kuwa uteuzi huo umeanza Mei Mosi, mwaka huu, 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Bibi Mwanahamisi Omari Kitogo alikuwa Mkadiriaji Ujenzi Msaidizi (Assistant Quantity Surveyor) katika Kampuni ya COWI, Tanzania.

Imetolewa na
:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu
.Dar es Salaam.
8 Mei, 2012

KUTOKA MKADIRIAJI KAMPUNI BINAFSI KUWA MSAIDIZI WA RAISI AISEEEE JK BABALAo
 
Naona akina mwanahamisi, mwanahawa, mwajuma, mwadawa, siajabu, sikujua......ndo wakati wao huu.
hahaha haya ndo majina yetu ya asili, ila ndo hivyo yanapotea watoto wa siku hizi hawataki kuitwa hivyo!
 
Tunavyoendelea tusishangae kusikia "Rais Kikwete amemteua so and so kuwa House Girl Mkuu. Uteuzi huo unaanza mara moja."

Kweli ujinga ni sawa na ukimwi, ukiupata ujue maisha yako kwishney! House girl katoka wapi kwenye mada hii?
 
ushirikiano upi? naona jamaa kaamua kugawa vyeo kama njugu sasa , kila siku mtu anateuliwa, kesho uatasikia ndugu MS ateuliwa kuwa Msaidizi wa ......kuhusu mambo yanayojadiliwa JF

Tunazungumzia kumpa ushirkiano katika majukumu mapya ya BIBI MWANAHAMISI OMARI KITOGO
 
hii nayo ni kati ya kali za mwaka; kutoka mkadiriaji majengo msaidizi tena wa kampuni binafsi hadi msaidizi wa rais! Ndiyo mapigo ya jk hayo.

tatizo nini? Fani aliyotambulishwa nayo au elimu yake kwenye fani nyingine na uelewa wake.
Usikalili majibu mkiwa wengi necta mtamekana mmdesa majibu feki
 
Back
Top Bottom