Rais Kikwete amteua Bi. Juliet Rugeiyamu Kairuki kuwa mkurugenzi mtendaji wa TIC

Dawa ni kubadili mfumo wa siasa Kila kitu kitabadilika hata wewe utafikiwa zamu yako Mkiwa.
 
Last edited by a moderator:
Inashangaza sana wanapokua wa kwanza kuwaita wenzao wadini wakati wao ndo wamebobea haswaa.
 
Matamko ya Mabaraza la Maaskofu yamekuathiri sanaaa.... Anyway ukipita pale kurasini waulizie ile nembo ( NGAO YA TAIFA ) getini ni ya nini ?
mimi sijawahi kuona nchi humu duniani yenye matamko ya maaskofu mengi kama hapa bongo.wanaizidi hata vatican bana...na kila wanapotoa matamko hata hawajui kuwa wana create more religious hardliner kwa pande zote.
 
Wako wapi wapiga kelele za udini? Naona toka apigwe mkwara na maaskofu kaamua kuwateua "wao" tu sometimes hizi blackmailing na mikwara mbuzi vinasaidia ku maintain "status quo".

Walau tutapumua kutoka kwenye "matamko"......


Kweli mkuu hata mimi hili huwa linanikwaza sana, yaani kuna wapu.mbavu wa kifikra kwao hawataki kuona muislam anateuliwa kuongoza organization yeyote au kupata nafasi kubwa katika kitengo fulani, Angalia UDOM na NSSF zinavyoshambuliwa wakati kimoyomoyo kila mtu anatoa pongezi kwa NSSF kwa utendaji wake. Hili linatokana na mazoea, ni vigumu sana kwa fikra ya binadamu kukubali mabadiliko. Jamani karne hii hakuna ambaye hasomi hebu tuhangaike kuijenga nchi kuliko kuendekeza mambo yasiyo na msingi.
 
...Since independence mna lipi la kujivunia hadi sasa? Keshokutwa tunasherehekea miaka 50 ya kuzaliwa kwa taifa la Tanzania ila maendeleo yake hayaonekani hadi leo.
Huo umaskini ni kutokana na UCCM wao, na wala sio Ukristu wao. Maendeleo ya nchi hayasukumwi kwa sera za dini, bali kwa sera za serikali iliyopo madarakani wakati huo (ambayo muda wote imekuwa ya CCM). Ndio maana tunatoa wito kwa wazalendo wa nchi hii, wakristu kwa waisilamu na wenye dini nyingine, wanawake kwa wanaume, vijana kwa wazee, kuunganisha nguvu zao ili kuiondoa CCM madarakani na kukiweka chama ambacho walau kimeshajijenga kiasi fulani (CHADEMA), badala ya kuanzisha chama kitakachoanza moja, au kitakachotumia nguvu kubwa na muda mrefu kuibomoa CCM. Haya mambo ya kuunganisha CUF na CCM ni mbinu tu za CCM kugawanya kura za wazalendo ili kiendelee kubaki madarakani kuendeleza umaskini huo tunaolia nao. Haya mambo ya kuwatumia BAADHI ya waisilamu wailaani CHADEMA ni mbinu nyingine ya CCM kuzigawanya kura za wazalendo. Kama unalalamika na umaskini wa nchi hii, basi jiunge na kundi linaloelekea kuiondoa CCM madarakani, na wala usiwe mmoja wa hao wanaotumiwa na CCM kuzigawa kura, wala usiwe mmoja wa hao wanaosema CHADEMA ni cha wakristu, wala usiwe mmoja wa hao wanaosema CHADEMA ni cha wachaga, tutafika
 
MONDAY, APRIL 22, 2013


viewer+(1).png

MICHUZI

Hongera Bi Julieth kwa kuteuliwa kushika wadhifa huu muhimu. Hata hivyo taarifa ya Ikulu ni fupi mno kuhusu sifa na uzoefu wako uliofanya ukateuliwa. Website ya SADC Banking Association bado inaonyesha kuwa wewe ni Meneja Mradi (Project Manager) wa PPP project. Majukumu yako hayakuainishwa na hicho cheo cha Meneja Mkuu wa Fedha na Huduma za Kibenki hakikutajwa humo. Ikulu, au wewe ikiwezekana, wangesaidia zaidi kama wangeonyesha ni vigezo gani wametumia kukuteua, la sivyo uteuzi huu hautofautiani na teuzi tulizozizoea ambapo watu wanateuliwa tu kwa sababu walikutana na Bwana Mkubwa huko nje ya nchi katika ziara zake za kikazi.
 
huyu ndiye mama yake na waziri yule anayehusika na sheria pia Angela Kairuki??

mwendo wa kujuana juana tu!!
Hapana huyu siyo mama yake Angela Kairuki. Angela Kairuki Hilo jina analotumia ni la ndoa(Mumewe).
Ndugu zangu wana JF tuwe tuna mazoea ya kufanya utafiti kidogo kabla ya kutoa lawama na malalamiko.
 
huyu sio ndugu na kairuki yule naibu waziri wa nini sijui? Au kaolewa na akina kairuki maana naona kuna Rugeiyamu na Kairuki hapohapo hebu nijuzeni

Mkweree ana mapenzi na majina ya wakina KAIRUKI!!! Mama ya Angela Kairuki ni mjumbe wa tume ya katiba na pia mjumbe wa bodi ya BOT, Angela kairuki ni Naibu waziri, Mbelwa kairuki ni Balozi na mkurugenzi wizara ya mambo ya nje na sas Huyu Kairuki mwingine hapo TIC!!! Kazi unayo na wakina kairuki baba MwanaAsha!!
 
Mbelwa Kairuki=Angela Jasmine Kairuki= Shemeji mume wa Juliet=Juliet R. Kairuki!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Ni nani ana influence hapa? Angela Jasmine Kairuki= Esther Mkwizu=Serikali mmmmmmmmmmmmmmmmmmmm!!! Hapa hakuna nepotism hata kidogo!! Maadili ya uteuzi yamezingatiwa kwa kuangali sifa za TIC Director aliyekuwa anatakiwa. Kwa hiyo Mbilinyi hakuwa nazo!! Anafaa TNBC!!
 
Hivi ikiwa kila uteuzi utaangaliwa kwa lensi ya ukristo au uislamu wale ambao siyo wafuasi wa hizo dini mbili ina maana hawana haki nchi hii? Kuna mamilioni ya watanzania ambao hawafungamani na hizo dini mbili na wana haki sawa ndani ya nchi yao hii. Jambo jingine ambalo wengi hamlizingatii ni kuwa nchi hii siyo kila mwenye jina la John ni mkristo na siyo kila Juma ni mwislamu.
u

Mkuu hilo limekuwa ni tatizo kubwa kwa Watanzania kwa kuangalia majina wakafikiri yanareflect kilichomo ndani. Mungu ahabudiwi kwa majina yetu bali katika kweli na roho na matendo mazuri ya mtu ndiyo dini na ukristu tafsiri yake ni matendo maana imani bila matendo imekufa. Pengine Yesu anakumbusha kuwa watawatambueni kwa matendo yenu. Hivyo bila matendo ya huruma, unyenyekevu, ucha Mungu, moyo wa kusamehe na maridhiano, upendo na amengine hakuna ukristu. Watu wasipotezwe na majina.
 
Mkweree ana mapenzi na majina ya wakina KAIRUKI!!! Mama ya Angela Kairuki ni mjumbe wa tume ya katiba na pia mjumbe wa bodi ya BOT, Angela kairuki ni Naibu waziri, Mbelwa kairuki ni Balozi na mkurugenzi wizara ya mambo ya nje na sas Huyu Kairuki mwingine hapo TIC!!! Kazi unayo na wakina kairuki baba MwanaAsha!!

Kagera technology inamchanganya mkuu wa kaya
 
huyu ndiye mama yake na waziri yule anayehusika na sheria pia Angela Kairuki??

mwendo wa kujuana juana tu!!

Ni mke mwenza wake!! Ameolewa na kakaye aliyemuoa Angela Jasmine (Kairuki)!!! I.e Angela na Julieth wameolewa nyumba moja kwa marehumu Dr. Kairuki. Do you want to connect the dotizz.??????????////////
 
Mimi Ng'wanamalundi Jidulamabambasi ni dini gani? Nyie mnaoangalia majina ya watu na kutambua dini zao??. Uwezo wenu wa kufikiri ni finyu sana. Lakini hakuna la kustaajabisha. Hakuna umaskini mbaya sana duniani kama umaskini wa kufikiri. Endeleeni kukumbatia tamaduni za wazungu na waarabu. Nyie endeleeni tu.
 
Back
Top Bottom