Rais Kikwete: Ama uamue Kusuka au Kunyoa

Ingekuwa ni amri yangu, ningewashauri wafadhili waache kabisa ku-supplement bajeti yetu ili tujifunze namna ya kujitegemea. Haiwezekani nchi yenye umri wa miaka takribani 46 ishindwe kujitegemea mpaka kesho ilhali tuna rasilimali za kutufanya tujitegemee!
Hovyo kabisa!
 
Self sufficiency siyo lazima uwe Ujamaa but yes Ujamaa ni one option. Self sufficient to me means kuji tosheleza au kuishi ndani ya uwezo wetu. Tuna shindwa nini kuadjust budget yetu iendane na hiyo 60% wakati kila leo wabunge wana jiongezea mishahara na marupurupu, magari ya kifahari yana agizwa na raisi kusafiri kila siku. To me I just want to see a Tanzania which can live within it's means. Tupange budget bila kupigia mahesabu hizo 40% za wahisani.

Asante mkuu kwa hayo niliyopigia nyekundi. wanakiri kwamba wabunge na viongozi wa serikali ya india wanatumia magari ya kawaida kuliko wao. kwamba pesa za chai na semina/workshop zinatoka kwenye kodi ya ndani (yaani ni ya uhakika) lakini pesa za MAENDELEO zinatoka kwa wafadhili eti wakina zito nao wanabariki hilo. Yaani ni uwendawazimu kudhani kwamba wafadhili wanayo excess na kwamba wanawakilisha nchi zao hapa sio kutafuta opportunities bali KUTOA PESA kwa MAENDELEO YA WATANZANIA.MIMI sijui ni kwa nini vingozi hawaoni tunadhalilika.
 
We acha tu, yaani hawa viongozi watia hasira sana wakati mwingine unafikiria huwa wanatumia
ubongo gani, kwani hata mambo ambayo yako wazi wanashindwa kuyasimamia,
fikiria waziri mkuu analalamikia matumizi makubwa serikalini wakati yeye alipaswa kuchukua hatua,
kwa kifupi viongozi wetu hawapo kwa ajili ya wananchi bali kama manyapara wakitekeleza matakwa ya mabwana.
 
Rais Kikwete.

Wafadhili wameamua kupunguza fungu lao la pesa linalokuja kwenye bajeti yetu. Wameteoa masharti na vitisho ambavyo vyaonekeana wazi kuwa wanachotaka kutoka kwa Tanzania pamoja na kuonekana kuwa ni nia nzuri kama vile kupiga vita ufisadi, lakini wanataka mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo tafsiri yake rahisi sana ni kuwa Tanzania iruhusu Wawekezaji waendeleze unyonyaji na kuivuna Tanzania kwa utashi na manufaa yao na si kwa manufaa ya Watanzania na Tafa letu.

Je unajiandaa vipi kukabiliana na upungufu huo? Je utakimbilia kutafuta Wafadhili wengine, utalegeza masharti yetu kwa ajili ya manufaa na maslahi ya Taifa letu ili kukidhi masharti ya Wafadhili ili watuongezee huko tujisenti au utasimama kidete na kuing'oa Tanzania kutoka mfumo tegemezi?

Bajeti ya Serikali yetu inategemea asilimia 40 ya fedha za Matumizi na Maendeleo kutoka kwa misaada ya Wafadhili na mashirika ya fedha ya kimataifa.

Tafsiri nyepesi sana ni kuwa sisi ni nchi huru kwa asilimia 60, asilimia 40 iliyobakia bado iko mikononi mwa wakoloni.

Ningependa sana ulisome tena Azimio la Arusha na ujiulize ni kipi wewe binafsi an CCM mmeendelea kukosea na hivyo kupoteza asilimia 40 ya Uhuru wetu?

Labda nikupe dokezo la kukupa faraja ili ufanye maamuzi kwa manufaa na maslahi ya Watanzania na si kukimbilia matakwa ya Mkoloni na vyombo vyake vya fedha.

Serikali ya Australia, ambayo ni nchi mmoja inayotupa misaada sana, imeongeza viwango vya mapato kwa makampuni yanayofanya uchimbaji wa madini na nishati na kuweka kiwango cha mapato na kodi kwa ni asilimia 40 ya mapato ya uchimbaji wa Madini, Mafuta, Gesi na aina zote za nishati.

Hugo Chavez, Lous Lula na hata Kabila na Kagame na viongozi wengi wa Dunia ya Pili na ya Tatu, wameamua kulinda maslahi ya nchi zao kwa kuongeza viwango vya kodi na mapato kwa Wawekezaji wa nje ili nchi hizi iachane na tabia ya mazoea ya kutegemea misaada na mikopo kujiendesha.

Kinachonishangaza mimi ni kuwa huu ni mwaka 2010, Tanzania hatujawa na ulazima wa kutumia Rasilimali zetu kwa lengo mmoja la kukamua Hazina yetu kama tulivyofanya mwaka 1978 tulipoingia vita na Uganda.

Ni mwaka 2010, Afrika Kusini iko huru na kila nchi inayotuzunguka iko huru pamoja na kuwa kuna chokochoko za ndani lakini ukweli ni kuwa ndoto za Tanzania kuvamiwa ni ndogo mno.

Sasa kama kwa miaka 25 tumeishi kwa Amani, Utulivu na Mshikamano, iweje tushindwe kujijenga kikamilifu na kuachana na Utegemezi wa misaada na hata kuendelea kuunadi uhuru wetu kwa hiyo asilimia 40 tunayowapa Benki ya Dunia, Nchi wafadhili na Wawekezaji?

Kwa nini chama chako CCM na Serikali yake vina kigugumizi cha kuleta mapinduzi ya uzalishaji mali ambao utalenga kumnufaisha Mtanzania na si mwekezaji?

Je ushajiuliza kama tungefuata mkondo na mfano wa Australia na kuongeza pato la Taifa kutoka wka Wawekezaji kutoka asilimia 4 hadi asilimia 40 ni mapato ya kiasi gani tungepata na ni miradi mingapi ya maendeleo tungeweza kuigharamia wenyewe?

Ikiwa ulikiri kuwa Asilimia 30 ya Bajeti yetu inapotea katika Rushwa, je huoni kama ukiziba kabisa mianya ya Rushwa na Ufisadi na hata kuongeza pato la Taifa kwa asilimia hata 25, Tanzania inaweza kuwa nchi inayojitegemea kabisa miaka 10 kutoka leo?

Ulipochaguliwa 2005, wengi walitegemea ungekuwa Gorbachev wetu ambye utaleta mapinduzi ya fikra na uzalishaji mali, mapinduzi ambayo yangeiondoa Tanzania kutoka utegemezi.

Lakini kinachoonekana ni kuwa umeendeleza demokrasia ya kujieleza kwa watu, lakini wanachokuambia, wanacholalamikia hata kukutukana kinaingia sikio moja na kutokea lingine na kasi yako ni kuiingiza Tanzania katika uchumi tegemezi na si ajabu kuongeza wigo wa utegemezi kwa kuuza asilimia zaidi za uhuru wetu kwa kisingizio chako cha kutuingiza katika soko huria au kama aliyekutangulia Rais Mkapa aliyekuwa akituhubiria Utandawazi na kutupumbaza na vijideni tulivyofutiwa huku akiruhusu misahama ya kodi na mapato na kuuza kila rasilimali kwa bei chee!

Uamuzi wa Wafadhili kupunguza misaada kwenye bajeti yetu isikupe kizunguzungu au shinikizo. Ningekuwa mimi wewe, ningeita timu ifanye kazi ya kuziba mwanya huo wa mapato kwa kuongeza pato la Taifa na kuiga walichofanya Australia!

Mara nyingine Ukarimu wako unafadhaisha, majuzi kwenye mkutano wa WEF ulikaririwa ukiwaita WB, IMF na nchi wafadhili eti wao ni Wakubwa, je unyonge wako na kujisalimisha kwa wanaotunyonya utakoma lini?

Tunajua wazi kuwa Takrima, Rushwa na Ufisadi ni vitu vigumu sana kwako kuvishinda, wewe CCM na Serikali yako mmenogewa sana na Takrima na Rushwa. Basi tunakupa Ruksa, kaa na hiyo Takrima yako, ipunguze kutoka asilimia 30 hadi 15, lakini ongeza pato la Taifa kwa kila sekta ambayo mwekezaji kaweka mguu kutoka asilimia 3 hadi asilimia 40. Zaidi ya hilo toa sharti la kutaka Wawekezaji watumie malighafi, nguvukazi na kila aina ya nyenzo kwa kutumia kinachopatikana Tanzania. Ama futa misamaha yote kwa Wawekezaji wote kutoka nje ya nchi na hata wa ndani ya nchi walio na ubia.

Uamuzi ni wako Mheshimiwa Rais, kusuka au kunyoa!

REV Heko kwako kwa uzalendo! Lakini huu mzigo tulionao sasa isingefaa kuutwisha kwa Kikwete peke yake bali kwetu sote Watanzania!

Nitowe mfano wa Grecce sasa ilivyo kuwa unafanana na yanayotaka kutokea Tanzania. Watanzania tayari tumeshajizoesha maisha ya hali ya juu na hakuna hata mmoja anaeuliza msingi wa maisha haya unatoka wapi. Watanzania wa kawaida hawawezi kulaumiwa kwa hili kwani kwa vile viongozui wao wamekuwa wakichekelea misaada na vijizawadi tunavyopewa. Viongozi hao ndio wanaofaidi na vijizawadi hivyo aidha kwa kuchukuwa sehemu kubwa kwa nafsi zao au kuhongwa ili kukubali matakwa ya wanaotupa vjisenti. Mtanzania wa kawaida anahisi kuwa maisha wanayoishi viongozi wao ndio maisha halisi yanayomfaa binaadamu yeyote na ndio maana wakaidai Serikali iwalipe zaidi ya uwezo wa kuzalisha na kutishia mgomo.

Wakati wa utawala wa Nyerere viongozi walifanya wanavyofanya sasa yaani kujilimbikizia mali na ndio maana waliporuhusiwa tu kuonyesha walichonacho hakuna aliyekuwa nyuma kimapato. Lakini wakati ule utawala haukuwa wa Kidemokrasia na wananchi wakitishwa na kuzuiwa kujieleza hisia zao. Nyerere alifikishwa alipofikishwa Kikwete sasa na akaamuwa kubwaga manyanga na kukubali kubadilika kwa mujibu wa matakwa ya Wakubwa. Sasa tunaishi katika demokrasia na wananchi wamekuwa waelewa wa mambo. Tatizo letu Watanzania tunapenda kutumia na tunafanyakazi kwa wale tu ambao wasipofanyakazi (kulima) watazidi kufa njaa. Tunatakiwa tubadilike na tuamuwe kufanya kazi ili tujiepushe na utegemezi lakini tabia yenu ya uvivu inatuzuia kufanya hivyo.

Sasa REV unafikiri Kikwete kama Rais afanye nini huku wabunge walipoingia madarakani tu wamedai mamilioni kama mishahara, hata wale wananaijinasibu kuwa wapiganaji wanafanya kufuru katika matumizi na huku wakijilabu kuwa wanastahiki kufuru hizo. Wapi! Hili ni jukumum letu sote katika huko kusuka au kunyowa kwani tukijidai tunajali uhuru wetu na huku hatuwezi kufanya kazi tuakuwa tunajidanganya na iwapo tutasarenda kwa matakwa ya Mabwana haitusaidii bali tunaahirisha tu matokeo ya miaka ya mwisho ya utawala wa Nyerere.
 
Miaka 50 hamsini ni umri mkubwa kwa binadamu na anapofika hapo huwa anakuwa anajitegemea. Sasa sisi kama nchi tunashindwa nini na resources tunazo za kutufanya tujitegemee nafikiri itakuwa vizuri sana maan serikali itaamka na kuanza kujitegemea vinginevyo kama hawatweza sio lazima wabaki madarakani kuna vyama mbadala vya kufanya hayo ambayo wao hawawezi.
 
Back
Top Bottom