Rais Kikwete akutana na wahariri; asema madai ya walimu hayatekelezeki!

Mh.Rais tunaomba tusikie kwa mara ya kwanza kama AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YETU Ukimkoromea ya mama wa nchi jirani anayedai ziwa nyasa mali ya Malawi.

Tukumbushe hasira zetu enzi za wimbo HUU: bandaaa wa Malawi atuvalia ngozi ya simba, hatujali hatujali. Tunataka tukusikie leo kuitesa kwenye anga zako kama amiri jeshi mkuu.

Vinginevyo hatutakuelewa, huyu mama sasa amekuwa kama mpiga filimbi wa hamerini. Come on JK
 
Asizungumze leo juu ya mgomo wa walimu, kwani kufanya hivyo ni ukiukaji wa Katiba na kuingilia uhuru wa Mahakama (hata hivyo huyu jamaa (JK) huwa anavunja Katiba mara nyingi, thus haina mbaya kama ataendelea kuivunja).
 
Mnategeme jipya toka kwa JK? Hawezi kuwa na ishu yoyote ambayo haijadiskasiwa kwa kirefu hapa JF.
Kama ataongea mbele ya waandishi wa habari basi aruhusu maswali, na swali la 1 liwe ana kauli gani kufuatia kufungiwa kwa gazeti la Mwana Halisi.
 
Wana JF

Rais Kikwete leo saa kumi kamili jioni anazungumza na taifa kupitia kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar. Agenda kuu iko mfukoni mwake, lakini swala la mgomo wa walimu huenda likatawala mkutano huo.

MY Take: JK akumbuke kuna kesi maakamani na hukumu inatolewa kesho. Mkutano wake usije ukaingilia uhuru wa mahakama na kuathiri maamuzi ya kesho.

Hukumu zinazotolewa na majaji ni kupitia matakwa ya wanasiasa
 
Hili la Malawi kutukoromea limenikera sana kwani nyerere alitusadikisha kwamba wa-malawi ni adui zetu kwani walitaka sehemu ya ardhi yetu na sasa wameanza tena.Longa JK acha woga wewe dume.Wasukuma wana msemo wao IYINIYI IDI KAYA YA JISHIMBE maana yake hii siyo familia isiyo na baba, baba lazima afoke wajue majirani
 
Wahariri msikubari awhutubie tu kama watoto wadogo, muulizeni maswali magumu aumbuke
 
hana jipya usanii mtupu matasikia anawalaumu walimu kabla ya kujilaumu yeye na serikali yake kuwa wasanii juu ya maswala ya wafanyakazi
 
Mi nataka tu kujua,Saed Kubenea naye amealikwa? Kwasababu mi najua wamefungia gazeti lake but he is free to continue with his jobs, na je ataruhusu maswali? maana'ek huyu jamaa ni mwoga sana kwa maswali, huwa simsikilizi tena but kwakua ataongea na Wahariri then i think nta tune ka TV kangu ili nimsikie.
 
Wana JF

Rais Kikwete leo saa kumi kamili jioni anazungumza na taifa kupitia kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar. Agenda kuu iko mfukoni mwake, lakini swala la mgomo wa walimu huenda likatawala mkutano huo.

MY Take: JK akumbuke kuna kesi maakamani na hukumu inatolewa kesho. Mkutano wake usije ukaingilia uhuru wa mahakama na kuathiri maamuzi ya kesho.

Updates:

Jamani anayefuatilia mkutano huu kwa Radio ama TV atoe updates hapa mara utakapoanza. Mie nitajaribu kutoa updates kama bepari wangu akinipa upenyo kidogo.

Labda kama anazungumza nao (waandishi wa habari) itakuwa ni kimya kimya maana TBC wanaonesha kikao cha bunge na Clouds (wasaidizi wa TBC wasiokuwa rasmi) kipindi hewani ni JAHAZI. Au suala la kuzungumza na waandishi nalo LIMEKWENDA MAHAKAMANI=kukutana kimya kimya??
 
Ni baada au kabla ya kufuturu? Asije haribu funga yake tu kwa kudanganya

si bora awe mfungaji tujue tuna mcha mungu na siku moja anaweza kukiri makosa yake na kubadilika au kubadilisha matendo yake ambayo yatapelekea hata nchi kubadilika maana atakuwa makini na mzalendo na ukwere ataacha na ubinafsi na uongo na upendeleaji na mengine tele
 
Muda sio mrefu Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania anaanza maongezi ya moja kwa moja.

Kaa mkao wa kusikiliza.
 
thanks, naona anazungumzia issue ya kuzama kwa meli na uokoaji
 
Raisi J.K kuongea na wananchi wa Tanzania kupitia TBC1 tuwe tayari, TBC1 yahairisha kuonyesha vipindi vya bunge kwa ajili hiyo

[MENTION]JK anaongea live kupitia tbc taifa 92.3, nmechelewa kumsikiliza sasa anaongelea maswala ya gas tanzania[/MENTION]
 
Eeeh vp kuna waandishi habari makini kama kubenea hapo na kuna mda wa maswali au
 
Back
Top Bottom