Rais Kikwete ahutubia taifa mwisho wa mwezi Februari

Kama anaruhusu maswali kwa njia ya simu nitamuuliza alikuwa wapi muda wote tangu mgomo wa madaktari leo ndo analiongelea! au alikuwa anasubiru mwisho wa mwezi (no emergency because he doesnt care)
 
mwakiluma utakuwa una katabia ka kuinamishwa;punguza umbea hata sisi tunaiona ana hutubia vizuri.
 
Jamani baba mwanaasha madaktari walisharudi kazini mgomo uliisha. Songea napo pametulia. Naona kama vile unatutonesha vidonda
 
Kamaliza-naona hotuba yake imekuwa fupi
kamalizia na staili ya obama,nampongeza kwa hii staili
 
...Gamba kuu limemaliza kutoa kinachoitwa hotuba ya mwisho wa mwezi....
Hakuna mvuto katika hotuba hii...hajazungumzia hali ya nchi kiuchumi, hajasema atawachukulia hatua gani wale ambao pinda alisema anamwachia rais...huenda huyu jamaa hayajui matatizo ya nchi hii...
 
Idadi itakayotakiwa ni 32 tu wakiwemo Rais wa JMT na Rais wa Zanzibar.

Sifa:

1.Wawe na uzoefu katika masuala ya uchumi, sheria nk.
2.Wawe wanakidhi mahitaji ya kijiografia.

Makundi yatakayohusika kutoa mapendekezo ya majina ya wajumbe ni
vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu,makundi mbalimbali yenye
mahitaji maalum na wadau mbalimbali wa masuala ya katiba. Pia
yeye mwenyewe anaruhusiwa kikatiba kuteua wajumbe wake.

Pamoja na kwamba nafasi ni 30 tu ukimuondoa yeye (Rais wa JMT) na Rais wa
Zanzibar makundi hayo yataruhusiwa kupendekeza wajumbe watatu kwa kila
kundi japo wanaweza wasichukuliwe wote kutokana na idadi inayohitajika
kuwa ndogo.

Source: Hotuba yake ya mwezi Februari, 2012.

Nawasilisha.
 
Kweli tunamsanii. JK hatutendei haki Watanzania. Hii nchi inamatatizo mengi ambayo ilibidi walau hatupe moyo. Kweli tuliliwa hapa. Walaaniwe wote waliompa kura na waliosaidia kuiba kura
 
Back
Top Bottom