Rais Kikwete aenda Brazil kukagua kilimo cha nyanya

Ngoiva

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
235
44
Rais wetu mtukufu, mhe. Dk. J. M. Kikwete afanya ziara ya kikazi nchini Brazil kukagua kilimo cha nyanya ili kuenzi sera ya kilimo kwanza.

Hiyo ndio safari ya kikazi ya mhe. Mkubwa. Watanzania sasa tujiandae kwa kilimo cha nyanya kwa maendeleo na ustawi wa jamii yetu na uchumi madhubuti.
 
Hiyo ni pamoja na wapambe zaidi ya 100. Ukitaka kujua Bongo ilivyop bongo sidhani kama alikuwemo afisa wa kilimo katika kundi hilo, ambaye angaa wanaweza kudai kuwa walikuwa SERIOUS ili achukue rekodi ya kurudi nayo wizarini kwa ajili ya utekelezaji!!!:thinking:
 
Angeenda pale kwenye chuo chetu cha kilimo wana mradi mzuri tu wa kilimo cha nyanya na mboga na matunda mengineyo.
 
Angeenda pale kwenye chuo chetu cha kilimo wana mradi mzuri tu wa kilimo cha nyanya na mboga na matunda mengineyo.

mkuu huyu rais wetu hathamini mambo yanayofanywa na wenyeji. Anawaabu na kuwasujudu wazungu sana, na ndo maana safi zake nyingi ni nje ya Afrika.
 
Atamaliza term mbili za urahisi (miaka 10) akiwa anajifunza na kushangaa. Hataacha chochote cha kukumbukwa na Watanzania zaidi ya kudidimiza uchumi na kupaisha bei za bidhaa na mahitaji mengine muhimu kwa watanzania. Bei ya mchele kwa sasa imefikia shilingi 2,800 hadi 3,000 kwa kilo ilhal sembe imegota shilingi 1,000 kwa kilo. Jaribu kulinganisha bei ya bidhaa hizo wakati anaingia madarakani mwaka 2005; mchele ulikuwa shilingi 500 hadi 600 kwa kilo wakati sembe ilikuwa shilingi 200 hadi 250 kwa kilo.

Ponda maisha JK Watanzania wanakuangalia na kuendelea kuvumilia maumivu na mateso ya ugumu wa maisha!!!!!!
 
Rais wetu mtukufu, mhe. Dk. J. M. Kikwete afanya ziara ya kikazi nchini brazil kukagua kilimo cha nyanya ili kuenzi sera ya kilimo kwanza. Hiyo ndo safari ya kikazi ya mhe. Mkubwa. Watanzania sasa tujiandae kwa kilimo cha nyanya kwa maendeleo na ustawi wa jamii yetu na uchumi madhubuti.

Nilikuwa sijajua kwamba tanzania tuna uhaba wa nyanya. Hii ni kali na si kidogo. kwanza tukishazilima tutanunulia nini kama hela zote wamegawana kule hazina. Au mwenye kitunguu atabadilishana na mwenye nyanya?
Muuza nyanya hapokei hela zilizoko mtaani. wao wamehamisha zile original wakatusambazia feki na kutufungulia kesi kwa kuzipokea.

'Nyonge mnyonge na haki usimpe' ndo sera ya serikali
 
Rais wetu mtukufu, mhe. Dk. J. M. Kikwete afanya ziara ya kikazi nchini brazil kukagua kilimo cha nyanya...
Hivi anatakiwa kukagua au kujifunza? Maana nijuavyo mimi, mtu anakagua kitu chake, sasa akikagua nyanya za Wabrazil inakuwa kama anataka kujua progress ya nyanya ambazo hakuzilima
 
Rais wetu mtukufu, mhe. Dk. J. M. Kikwete afanya ziara ya kikazi nchini brazil kukagua kilimo cha nyanya ili kuenzi sera ya kilimo kwanza. Hiyo ndo safari ya kikazi ya mhe. Mkubwa. Watanzania sasa tujiandae kwa kilimo cha nyanya kwa maendeleo na ustawi wa jamii yetu na uchumi madhubuti.

afadhali.......pengine itatusaidia na si ile ya kwenda Jamaica kwenye ile pembea ambayo ilitakiwa iwepo sehemu kama Ngorongoro Crater tangu miaka hamsini iliyopita.

my worry..asije akakutwa Copa Cabana beach akiogelea kisha tukaambiwa aliunganisha na likizo.
 
Rais wetu mtukufu, mhe. Dk. J. M. Kikwete afanya ziara ya kikazi nchini brazil kukagua kilimo cha nyanya ili kuenzi sera ya kilimo kwanza. Hiyo ndo safari ya kikazi ya mhe. Mkubwa. Watanzania sasa tujiandae kwa kilimo cha nyanya kwa maendeleo na ustawi wa jamii yetu na uchumi madhubuti.

Ziara hiyo ni muhimu kwa serikali?....zaidi ya milioni mia tatu zimetumika kwa ajili ya safari hiyo then tunakagua kilimo cha nyanya...what a shame...............
 
Naomba magreat thinkers anayejua idadi ya safari za huyu vasco daggama wetu na cost kwa kila safari atuwekee hapa. Mimi nadhani labda wanayemwita wanamlipia garama za safari.
 
Prezdent gb ndogo jamani mmusamehe tu. Mlikosea wenyewe kumpa mzigo asioewza kuukabili.
 
Back
Top Bottom