Rais Karume aepushwe na mgogoro wa kiwanja

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Rais Karume aepushwe na mgogoro wa kiwanja
Tuesday, 04 January 2011 20:55

karumeznz.jpg
Habari zilizopatikana mwishoni mwa wiki zinasema kuwa waumini wa Kanisa la Anglikana Tanzania wameingia katika mgogoro wa ardhi na mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Fatma Karume. Kanisa hilo limemtaka asitishe ujenzi katika kiwanja kilichoko Mbweni, ambacho linadai ni chake tangu wakati wa biashara ya utumwa mwaka 1871.

Waumini wapatao 100 walifanya ibada maalumu katika kanisa lililopo Mbweni, karibu na makazi ya Rais mstaafu Karume, kuomba Fatma aiachie ardhi hiyo kwa ajili ya matumizi ya kanisa.

Eneo hilo pia lina makaburi ya kanisa hilo. Lakini katika hali ya kushangaza, baada ya kukamilika kwa ibada hiyo, waumini hao wanadaiwa walikwenda eneo la kiwanja na kufanya maombi na baadaye walipandwa jazba na kuanza kubomoa mbao zilizotumika katika ujenzi.

Msaidizi wa Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Mathew Mhagama alisema walifanya maombi kwa ajili ya kiwanja cha kanisa hilo ambacho alidai kilivamiwa, na kuongeza kuwa waumini walikerwa na ujenzi uliokuwa unaendelea na ndio maana waliamua kuvunja mbao na vifaa vya ujenzi huo. Alidai kuwa baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964, hati miliki za eneo hilo zilifutwa na waliomba hati za kumiliki eneo hilo tangu mwaka 1980 bila mafanikio na ndipo hivi karibuni walipomuona Fatma akianza kujenga katika eneo lao.

Lakini mara baada ya waumini hao kuvunja mbao za ujenzi huo wa nyumba ya Fatma, Rais huyo mstaafu akifuatana na Fatma, alihutubia mkutano wa waandishi wa habari nyumbani kwake Mbweni na kueleza kuwa madai ya waumini hao hayakuwa ya kweli kwani kiwanja hicho kinamilikiwa rasmi na binti yake huyo, ambaye alidai anazo hati zote. Rais huyo mstaafu alisema maneno mengi makali dhidi ya viongozi wa kanisa hilo ambayo tunadhani sio vyema kuyasema katika tahariri hii.

Wakati tunatambua fika kwamba hatuna mamlaka wala uwezo wa kutamka ni upande gani katika mgogoro huo ndio mmiliki halali wa kiwanja hicho, tunadhani kwamba mgogoro huo kati ya kanisa hilo na familia ya Rais huyo mstaafu haukusimamiwa kwa umakini na pande mbili hizo husika. Kwa kuacha mgogoro huo upambe moto kiasi cha wahusika kutupiana maneno na kupeleka tofauti zao katika vyombo vya habari, pande zote mbili zimeonyesha udhaifu fulani kwa kutotambua kuwa jamii yetu inaenzi pande zote mbili zilizo katika mgogoro, hivyo haiwezi kufurahia wakati tofauti zao zinapotolewa hadharani.

Tunasema hivyo kwa sababu mbili: Kwanza, masuala yanayohusu hisia za kidini, mbali na zile za kisiasa na kikabila, ni masuala nyeti mno kiasi kwamba yasipotatuliwa kwa umakini na busara huweza kusambaratisha jamii.

Historia inatufundisha kuwa nchi nyingi ambazo hazikuwa makini katika masuala hayo zimeingia katika migogoro na kusababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe. Ni bahati nzuri kwamba waasisi wa sehemu zote mbili katika Muungano wetu walitambua jambo hilo na ndio maana walifanya kila lililowezekana kuweka misingi ambayo mpaka leo inatufanya tuwe wamoja.

Pili, Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abedi Karume ni kiongozi ambaye alionyesha uongozi uliotukuka, hivyo jamii inamuenzi kwa mambo mengi, ikiwamo kuleta maridhiano Zanzibar, baada ya miaka mingi ya siasa za chuki na utengano baina ya wafuasi wa vyama vya Cuf na CCM.

Wazanzibari wanamuenzi kwa kuanzisha mchakato uliozaa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Hivyo, hadhi ya Rais huyo mstaafu ni kubwa mno, na kumuacha aingie katika malumbano ya kugombea ardhi kilikuwa ni kitendo cha kumshusha hadhi na ambacho hakikuwa cha lazima, kwa maana kwamba mtoto wake, Fatma Karume ndiye anayehusika na mgogoro huo na anao uwezo kama wakili wa kujisimamia mwenyewe.

Kwa kuwa mgogoro huo sasa upo mezani mwa Makamu wa Rais, Balozi Seif Ali Idd, tunayo imani kuwa haki itatendeka pasipo kupindisha sheria. Tunashauri kuwa Rais mstaafu Karume aachwe apumzike, kwani mgogoro huo sio wake.
 
Kumbe Wikileaks walisema ukweli kuwa serikali ya karume ilikuwa ikiendesha ufisadi mkubwa wa ardhi kwa kuwapora wananchi wanyonge bila kuwajibishwa na chombo cho chote kile..................
 
kanisa linasema liliomba hati ya eneo hilo tangu 1980 bila mafanikio baada ya zile za awali kufutwa mwaka 1964, je huyu binti rais mstaafu alipewa hati yake lini? Hao watu wa kanisa hawajatambua kwa nini hawakupewa hiyo hati kama walivyo omba badala yake wakabaki kushuhudia ujenzi wa binti mtukufu? Nway, this is africa where being in power warrants one and his/her (family members and relatives), plus his/her cronies to benefit without huddles!
 
aepushwe kivipi ikiwa anahusika? yaani unataka tuamini kuwa binti yake angeweza kuamka asubuhi na kuamua kupora ardhi bila baba yake (ambaye ni rais) kujua? huyo binti alipata wapi ujasiri huo?
 
nawasiliana na jamaa wa wikleaks kupata nakala ya jambo hili na taarifa sahihi
 
Back
Top Bottom