Rais Joyce Banda amfukuza kazi Mkuu wa Polisi Malawi!

jk safari inayofuata aende malawi akapate uzoefu wa kuendesha serikali.
 
sawa sawa kumtimua kazi...........unadhani hata mi niwe rais leo..lazima mwema alambe mchanga tu.
umeooona eeh
msiogope hi ni sytem kila uongozi anaekuwa kwenye cheo cha juu lazima aive na wewe kuhakikisha usalama wako na ndicho mama alichofanya
 
Sawa sawa kumtimua kazi...........Unadhani hata mi niwe Rais leo..lazima Mwema alambe mchanga tu.

Duh. Noma sana. Kimsingi utendaji wa polisi inatakiwa usiegemee upande wowote, tofauti na hapa kwetu
 
She iz iron lady,Kumfukuza tu haitoshi mtumieni salam kuwa amfungulie mashtaka kabisa uone vile ambavyo wangeanza kukimbia nchi yao.....Yaaani huyu Mama Banda ananipa mzuka sanaa, Hivi hana mtoto wa kike jamani nkaanza kujisogeza ? Namfananisha na Amanda wa division kwenye season ya NIKITA !
 
Kazi bado anayo mama rais Joyce Banda.

Baada ya kuona Bingu wa Mutharika amefariki tena akiwa nje ya nchi mafisadi wakaanza kuangalia "loopholes" kwenye katiba ili kumweka mdogo wa marehemu Peter Wa Mutharika ili arithi kiti cha urais.

Peter Mutharika ni waziri wa mambo ya nje wizara nyeti sana na inayodhibiti sera ya nje ya nchi hiyo, kwahio ili kuendeleza usafi mama Banda ni lazima atamtimue bwana Peter Wa Mutharika maana ni kama bado yupo.
 
Kazi bado anayo mama rais Joyce Banda.

Baada ya kuona Bingu wa Mutharika amefariki tena akiwa nje ya nchi mafisadi wakaanza kuangalia "loopholes" kwenye katiba ili kumweka mdogo wa marehemu Peter Wa Mutharika ili arithi kiti cha urais.

Peter Mutharika ni waziri wa mambo ya nje wizara nyeti sana na inayodhibiti sera ya nje ya nchi hiyo, kwahio ili kuendeleza usafi mama Banda ni lazima atamtimue bwana Peter Wa Mutharika maana ni kama bado yupo.

Achana na mafisadi, wanaweza wakakuua huku wanakuona au ukifa wanashangilia kwamba sasa tupange namna ya kuweka mambo sawa.

Ukweli ni kwamba Bingu wa Mutharika alifia Malawi. Mafisadi walichofanya ilikuwa ni kusafirisha mwili wa marehemu ili wapate nafasi ya kurekebisha mambo. Ndio maana ndege ya ambulance ambayo iliitwa toka Sauzi kuja kuchukua mgonjwa, rubani alipogundua kwamba ni mwili wa marehemu, aligoma kuondoka mpaka walipoomba vibari vya kumsafirisha kama mzigo na sio mgonjwa. Ndege ilikuwa iondoke saa moja usiku kwa saa za Malawi, lakini ilikuja kuondoka saa tano za usiku.

Kilichonisikitisha kuliko vyote Prof. Peter Mutharika anajua kabisa kaka yake amefariki na bado anakaa kwenye kikao kusuka mipango ya kumrithishwa kiti. Halafu mkewe, Callista nae alishiriki hiyo dhambi. Hapo ndipo unapoanza kujiuliza hivi huyu Callista alimpenda Bingu wa Mutharika au alipenda title ya Urais?

Mama bado ana kibarua kigumu maana baraza la mawaziri wengi wao walitaka kubaka Katika ili Peter awe Rais, so inabidi awashughulikie. Uzuri mwingine ni kwamba ana support ya baadhi ya wanachama wa DPP (walioanzisha Hope Alliance kimya kimya) na pia kuna vyama vingine vinamuunga mkono, tunaweza kuona serikali ya mchanyato kama sio mseto. Wapambe wa Bingu wa Mutharika (akina Kaliati na wenzake) that is the end, wajiandae kukalia mabenchi Bungeni, zama zao zimekatishwa bila kujiandaa!
 
Ofcourse anatakiwa pia amtimue mkuu wa majeshi!
UKitaka uraia wa Malawi wee nenda Kyela jifunze kinyaki polepole unajisogeza Karonga bidae ukiiva kwenye kilugha chao unasogea Mzuzu then LIlongwe!
Wakikuuliza kabila unasema wewe Nkonde

Umenikumbusha mbali sana ... kuna kipindi vijana kutoka Tanzania walikuwa wanazama sana kwenda kufanya vibiashara lakini bila documents zozote. Ili kuwakamata hao wazamiaji, kulikuwa na random search kwenye baadhi ya siku ambapo askari walikuwa wanaweka barriers.

Askari wengi wanaoishi maeneo ya kuanzia Kasumulu - Kasyova mpaka Karonga wanaongea kiswahili kama kawa. Basi siku wakiamua kukamata wazamiaji walikuwa wanasimamisha vi-Hiace then washusha abiria wote. Wakishamshitukia abiria hasa vijana, Polisi anamsalimia, MAMBO? Kijana akiingia tu mkenge akajibu POA, basi ndo inakuwa imekula kwake wanamdaka hapo hapo kuuliza documents. Suluhisho ni ama awahonge au wanamrudisha Kasumulu.

Ushauri wako unaweza kumsaidia kuishi kwa muda kimachale, si unajua tena itafika mahali atahitaji huduma kubwa kama passport na mengineyo, lazima watataka ma-documents. Halafu jamaa wa huko wanathamini uongozi wa ki-chief. Kama huna nondo/utambulisho wa kutoka kwa Chief wa local area unayotokea then unaweza kupata ugumu fulani. Sina hakika na wale wakazi wa Lilongwe au Blantyre kama na wao huwa wanaulizwa hizo documents za kutoka kwa ma-chief wao.
 
Kutokana na polisi na vyombo vya habari nchini Malawi kukitumikia chama tawala cha nchi hiyo wakati wa utawala wa rais aliyefariki siku chache zilizopita badala ya majukumu sahihi ya kiserikali ktk utawala uliopita,utawala mpya wa Rais Joyce Banda umemfuta kazi mkuu wa jeshi la polisi (IGP) wa nchi hiyo pamoja na kuwafuta kazi viongozi wa vyombo vya habari vya serikali ya Malawi kwa kosa hilohilo.

Hapa kuna funzo kubwa kwa vyombo vyetu vya usalama na vyombo vya habari vya serikali ya Tanzania (mfano TBC )ambavyo kwa makusudi kabisa vimekuwa vikifanya kazi bila kufata maadili ya kazi yao na kujikuta vikifanya kazi kwa matakwa ya CCM na mafisadi wa nchi hii na kuwakandamiza wanyonge na kuwanyima haki yao ya kikatiba.
Rai yangu kwa polisi,Mahakama na vyombo vya habari vya serikali ya Tanzania ni kusoma alama za nyakati na kubadilika kwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni za kuundwa kwa vyombo hivyo,vinginevyo watakumbana na dhahama ya kufukuzwa na kupambana na mkono wa sheria kwa kutumia madaraka waliyopewa vibaya pale ambapo Nchi itarejeshwa kwa utawala wa haki unaojali masilahi ya nchi na wananchi wake kwa ujumla.Hili lipo njiani na si muda mrefu litatimia kazi kwenu vibaraka wa kusigina haki za wanyonge na kuwanyang’anya kesho yao kwa niaba ya watawala.
:nono:


 
Lazima afanye hivyo kwa nia njema tu ili aweze kuongoza.
 
Kwetu haiwezekani maana ameowa sehemu moja na mkuu na jemedari wa majeshi
 
inakera vyombo vya dola kukitumikia chama tawala. hata hivyo rais mpya wa Malawi amekuwa na papara mno ya kuwatumia kabla hata hajafikisha masaa 48 ya utawala wake.
 
Hebu amua mwenye maamuzi ya huyo bosi mpya wa Malawi kama siyo malipizi.....................

[h=1]Malawi's new president sacks police chief[/h]
na jana kamfuta kazi gavana wa benki.........na kumpachika makamu wa gavana ambaye ni mwanamke...........sorority power now in full gear in Malawi?......aliahidi kuwa hatalipiza visasi lakini hivi ni nini ?
 
Back
Top Bottom