Rais jk uko wapi?

mtetemo

New Member
Nov 3, 2011
4
0
Barua ya wazi kwa rais
Sisi wafanyakazi 12 wa Bodi ya TumbakuTanzania (TTB) kada ya udereva na wahudumu, tunapenda kuwasilisha kwako kero yauchakachuliwaji wa mishahara yetu uliofanya kati ya Bodi na Hazina.
Kwa mujibu wa taratibu hazina hutulipa misharaya kila mwezi kupitia akaunti ya bodi na kisha bodi hutupatia hati ya malipo.Tumebaini kuwa toka mwezi Novemba 2010 mpaka mwezi Julai 2011, Hazina ilikuwaikitulipa mishara mipya, lakini cha ajabu Bodi ilikata ongezeko jipya la mishara yetu nakuendelea kutulipa mishara ya zamani.
Katika kipindi hicho Bodi imekata Sh 15,232,500kutoka katika mishahara bila ridhaa yetu, takwimu hizi zinatokana na hati zamalipo zilizotolewa na hazina ambazo hata hivyo bodi ilizificha na badala yakeilitupatia hati zingine.
Zaidi ya hapo tumebaini kuwepo kwamawasiliano kati ya bodi na hazima. Katika barua yenye kumb nambaTTB/C/FA/26/VOL.VII/28 ya Desemba 27, 2010 yenye kichwa cha habari ongezeko lamishahara ya kada ya udereva na wahudumu, bodi iliiandikia Hazina ikieleza kuwa‘Salary Slips’ ilizozipokea mwezi Novemba 2010 imeonekana kuwepo kwa ongezekola mishara kwa kada za udereva na wahudumu. Kwa mujibu wa barua hiyo bodiilikuwa ikiomba hazina kutoa ufafanuzi wa ongezeko hilo.
Ikijibu barua hiyo, hazina katika baruayake yenye kumbu namba C/BA.54/13/03/10 ya januari 7, 2011 ilijibu kuwa kwamujibu wa taarifa za zake hakuna marekebisho ya mishahara yaliyofanyika kwawatumishi wa bodi kwa mwaka 2010 na kusisitiza kuwa inawezekana mabadiliko hayoimesababishwa na mapungufu kwenye komputa za mfumo wa malipo. Hata hivyo hazinailidai kuwa barua ya TTB inafanyiwa kazi na kwamba matokeo ya uchunguzi huoyatatolewa kwa Bodi.
Bodi ya Tumbaku Februari 7, 2011 ilitoabarua kwa wafanyakazi wote yenye kumbukumbu TTB/C/FA/26/VOL.VII/35 ikiwajulishajuu ya majibu yaliyotolewa na hazina kuhusiana na mabadiliko ya mishahara kwakada ya udereva na wahudumu.
Aidha Machi 2, 2011, bodi iliiandikia tenaHazina barua yenye kumbu namba TTB/C/FA/26/VOL.VII/41 ikieleza kuwa ni takribanmiezi minne sasa toka marekebisho hayo kufanyika pasipo hazina kutoa ufumbuziwa suala hilo hali ambayo ilidaiwa kusababisha manung’uniko makubwa kutoka kwawafanyakazi husika na chama cha wafanyakazi dhidi ya menejimenti.
Kutokana na barua hiyo bodi iliendeleakuomba maelekezo zaidi ili kuruhusu malipo hayo kufanyika kama ilivyotolewa nakusisitiza kuwa kama si stahili yao kwa maana kuwa inalipwa kimakosa irudishwehazina. Kwa upande wake hazina ikijibu barua hiyo kwa barua yenye kumbu nambaTYC/T/200/809/34 ya Machi 8,2011 ikieleza kuwa maombi ya TTB yanafanyiwa kazina kwamba bodi itafahamishwa pundu ufumbuzi utakapo kamilika.
Hatimaye Julai 20, 2011 Hazina iliiandikiabarua bodi yenye kumbukumbu namba C/CA.251/548/02/8 ikiifahamisha bodi kuwaimefanya uchunguzi na kubaini kuwa mambo manne ni pamoja na mifumo ya mishaharaya bodi ya tumbaku kwa waendeshaji (TTBOS) inafanana na ile ya Bodi ya UtaliiTanzania kwa waendeshaji (TTBOS).
Mengine ni marekebisho ya nyongeza zamishahara hufanywa kwa kuingiza waraka husika kwenye komputa ya malipo na siyojina moja moja na kwamba marekebisho ya mwisho ya Bodi ya Tumbaku yalifanyikamwaka 2009 yale ya bodi ya utalii yalifanyika mwaka 2010. Pia barua hiyoimesema kuwa wakati wa kurekebisha mishahara ya Bodi ya utalii mwaka 2010 kwabahati mbaya komputa ilikokotoa mishahara ya TTBO kwa bodi ya tumbaku wakatihaikupaswa kufanya hivyo.
Kwa barua hiyo bodi iliagizwa kutolipa mishahara hiyo na kuijulisha Hazinaharaka kiasi kilichozidi ili kirudishwe kwenye mfuko mkuu wa serikalivinginevyo fedha hizo zitakatwa kwenye mishahara ya wafanyakazi hao kwa mweziwa agosti.
Barua hiyo ilisisitiza kuwa iko haja yakufanya mazungumzo kati ya TTB idara ya bajeti, idara ya Komputa na msajiri waHazina ili kukubaliana jinsi ya kubadilisha vifupisho vya viwango vya mishaharaya bodi ya Tumbaku (TTBO), ili kuondoa utata uliopo na vile vya bodi ya utaliiTanzania (TTBO)
Kutokana na barua hiyo ya hazina bodi yatumbaku iliwaandikia barua wafanyakazi wake wote wa kada ya udereva nawatumishi yenye kumbukumbu namba TTB/C/FA/26/VOL.VII/37 ya Julai 22, 2011ikiwafahamisha juu ya agizo la Hazina na kudai kuwa mishara tunayopata sasandiyo iliyo halali.
Pamoja na ufafanuzi huo, tunaulizaiwezekanaje toka mwezi Novemba 2010 mpaka kufikia mwezi Julai 2011 makosayanayodaiwa kusababishwa na komputa yaendelee? Mheshimiwa rais sisi tunaaminikuwa wafanyakazi waliohusika na mchezo huo ambao unaashilia dalili ya wizi wafedha za umma wawajibishwe.
Sambamba na hilo tumebaini pia kuwa wakobaadhi ya wafanyakazi katika bodi yetu ambao wameajiliwa kinyemela pasipokufuta taratibu za ajira za kutangaza nafasi na kuwafanyia usaili waombaji.Tunafahamu kuwa baadhi ya wafanyakazi hao walikuwa wakiitwa mmoja mmoja nakupewa ajira .
Kama hilo halitoshi tunatambua pia ya kuwawako baadhi ya wafanyakazi wanaokaribia 10 ambao wameajiriwa hapa lakinihawalipwi mishahara na hazina badala yake kupata misharaha kutoka OC jamboambalo si utaratibu wa serikali hivyo kuzifanya shughuli zingine za bodikushindwa kufanyika kutokana na kutokuwa na fedha.
Kutokana na hilo tunaomba tume yakuchunguza malalamiko haya, sisi tuko tayari kutoa ushirikiano ili kuthibitishataarifa hizo.
Sisi wafanyakazi wa TTB.


 
Back
Top Bottom