Rais JK mwenyewe awakana gazeti kwenye facebook yake

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,033
23,873
Jakaya Kikwete
Gazeti la Mwananchi la leo, Jumanne, Januari 31, 2012 limeandika habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge: Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku.
Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka kutoa ufafanuzi ufuatao:
Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi.
Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo:
Kwanza, Mheshimiwa RaisKikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakarisuala hili.
Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya sualahilo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasilianoya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Januari, 2012
 
unajua raisi siyo mtu bali ofisi?

Mbona hajajibu hata comment moja hapo ktk Facebook huwezi kujiuliza?
 
Childish government! unaweza ukaugua degedege bure kwa kufuatilia blunders za serikali hii ya NEC, TISS na POLISI!
 
HIVI kweli watu wazima mnaamini kuwa PM kasema asichojua.MPs, Posho Tsh.200,000/- wanakula tangu Bungela lililopita Spika mwenyewe kathibitisha hilo. Watu wazima wameamua kufool WaTz,wakati huu msg inapoandikwa wajamaa tayari washalamba chao. Wataalam sio wamuhimu sana kwa nchi hii kwa sasa mpakA HAPO BAADAE, wao wasubiri bajeti. Kipaumbeleni wanasiasa kwanza. MUNGU TUSAIDIE NA HILI TATIZO
 
Account hii haioperate yeye JK, inakua operated na dogo mmoja yuko hapo jengo la CCM lumumba. Habari zote za hii account ni copy and pasted kutoka source nyinginezo hasahasa kurugenzi ya habari!
 
namaanisha yoyote anaweza kuandika hilo bandiko uliloliona facebook. Kwanza bandiko lenyewe limeshindwa kututhibitishia kuwa JK hajasaini.

SOBIBOR uko sahihi kuhoji kama ni yeye aliyandika kwenye hiyo page ya Facebook. Ukweli ni kwamba ile account wala hana habari nayo, kuna mtu anayeiendesha, wengi huwa wanadhani wanawasiliana naye moja kwa moja lakini ni choo cha kike tu.
Siyo kama Paul Kagame ambaye ana account ya Twitter na huwa anachat na watu mara nyingi tu. Kikwete is not as techno-savvy as people would make you believe.
 
Back
Top Bottom