Rais Jakaya Kikwete amewataka Watanzania wote kutimiza wajibu wao wa kujitokeza

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,298
33,083
SensaJK(1).jpg

Rais Jakaya Kikwete


Rais Jakaya Kikwete amewataka Watanzania wote kutimiza wajibu wao wa kujitokeza kuhesabiwa leo kutokana na Sensa ya mwaka 2012 kuwa na umuhimu wa aina yake na tusipofanya hivyo dunia itatushangaa.

“Naomba kila mmoja wetu ahakikishe kuwa anakuwepo kuhesabiwa na kujibu maswali yote yatakayoulizwa na makarani wa sensa kwa ufasaha. ”, Rais alisisitiza hayo katika hotuba yake ya kila mwezi ambayo aliitoa jana, siku moja kabla ya kufanyika zoezi la sensa nchini leo.

Alisema taarifa zake zitatumika kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Dira za Taifa za Maendeleo za Tanzania Bara na Zanzibar; Mkakati wa Kukuza na Kupunguza Umaskini Tanzania Bara (MKUKUTA II); Mkakati wa Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA II); na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa 2011/12 – 2015/16.

Vilevile taarifa zitakazopatikana zitatumika kupima maendeleo ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia (Millenium Development Goals) yaliyowekwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2000, aliongeza.

Kuhusu madodoso amesema wapo baadhi ya watu wanaotaka liongezwe swali la dini ya mtu katika orodha ya maswali yatakayoulizwa katika Sensa ya mwaka huu.

“Wahusika wakuu hasa ni baadhi ya viongozi na wanaharakati wa Kiislamu. Wao wanasema bila ya swali hilo kuwepo, Waislamu wasikubali kuhesabiwa. Wamekuwa wanafanya juhudi kubwa ya kuwashawishi Waislamu wawaunge mkono katika msimamo wao huo, anasema Rais na kuongeza;

“Nimesoma baadhi ya nyaraka na vipeperushi vyao kuhusu madai hayo. Nilipata pia bahati ya kukutana na kuzungumza na baadhi ya wanaharakati na viongozi wa harakati hizo. Nia yangu katika kufanya hayo ilikuwa ni kutaka kuelewa kwa undani hoja na madai yao.

“Yako mambo kadhaa yanayotajwa kama sababu, lakini ukweli ni kwamba jambo linaloweza kuhusishwa moja kwa moja na Sensa, ni lile la takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani zilizotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki, Shirika la Utalii na Shirika la Utangazaji Tanzania.

Kuhusu Tume huru, Rais Kikwete amesema haoni ulazima wa kuunda Tume Huru ya Sensa yenye uwakilishi sawa wa Wakristo na Waislamu kwani tangu mwaka 1931 kazi ya Sensa imekuwa inafanywa na Ofisi Kuu ya Takwimu nchini na ndipo ujuzi na maarifa yote yapo.
Amesema hata ukiamua uiite Tume bado utawatumia watu hao hao, hivyo mabadiliko hayo hayana sababu. Vile vile, haoni haja ya kuwa na mgao wa

wafanyakazi wake kwa msingi wa dini kwa sababu Sensa siyo kwa ajili ya kujua Wakristo na Waislamu. Huduma hazitolewi kwa misingi ya dini za watu.
Rais Kikwete amese kuwa tofauti na miaka ya nyuma, Sensa ya mwaka huu imekabiliwa na changamoto ambazo hazijawahi kuwepo. Kuna baadhi ya wenzetu wamekuwa wanafanya jitihada za makusudi za kutaka kulivuruga zoezi la Sensa nchini.

Wamekuwa wanawashawishi watu wasishiriki kuhesabiwa, kwa sababu ambazo baadhi yake hazina uhusiano wo wote na Sensa. Zipo sababu nyingine ambazo hata haziingii akilini, alisema.

Kwa mfano, alisema wapo watu wanaodai kuwa hawatashiriki Sensa mpaka mjusi aliyeko kwenye Jumba la Makumbusho kule Berlin, Ujerumani atakaporudishwa. Kinachozungumzwa hapa ni mabaki ya mifupa ya mnyama wa kale aliyekuwepo hapa nchini zaidi ya miaka milioni 200 iliyopita.
Mwaka 1906 wana sayansi wa Kijerumani waliyagundua mabaki hayo kule Tendaguru, Lindi, wakayafukua na kuyapeleka Ujerumani ambako yamehifadhiwa tangu wakati huo.

Kudai mifupa hiyo irejeshwe nchini si jambo baya, watu wataona wanyama wa kale waliokuwepo wakati huo wanafananaje. Huenda pia kikawa kivutio cha utalii.

Hata hivyo, akasema kugeuza kurejeshwa kwa mabaki hayo kuwa sharti la kushiriki Sensa ni jambo ambalo mantiki yake haielewi. “Watu wakisusia Sensa kwa sababu hiyo itakuwa siyo tu haieleweki wala haielezeki, bali hata watu wengine nchini na duniani watawashangaa. Lakini, jambo ambalo

ningependa wajiulize ni kuwa hivi hasa wanamsusia nani? Mjerumani au wanajisusia wenyewe?, aliuliza na kuongeza;
“Hivi kweli mtu uko tayari kuacha manufaa yako ya maendeleo yapotee au yaathirike kwa sababu ya mjusi ambaye hata akirejeshwa huna manufaa ya moja kwa moja? Hasara anapata nani sisi au wao? Hata hivyoa aliwasihi, Watanzania wasiwasikilize watu wanaoeneza maneno yahusuyo Mjusi au mambo

mengine ya upotoshaji na uvurugaji wa mambo yenye maslahi makubwa zaidi kwetu binafsi na nchi yetu. “Tuachane nao hawatutakii mema na wala hawaitakii mema nchi yetu. Nawaomba tusitumie vibaya uhuru wa kutoa maoni”, alisisitiza Rais Kikwete.
Alisema katika mazungumzo yake na baadhi ya viongozi wa Waislamu aliwaambia kuwa anelewa sababu na hoja za wao kukasirishwa na kutokuzikubali

takwimu hizo. Vile vile, aliwaeleza kuwa takwimu hizo si za Serikali bali ni za mashirika hayo. Alisisitiza kuwa takwimu za Serikali kuhusu idadi ya watu hutolewa na Ofisi Kuu ya Takwimu na si chombo kingine chochote cha Serikali.

Bahati nzuri Ofisi Kuu ya Takwimu haijatoa takwimu hizo na wala siyo chanzo cha takwimu zilizotolewa na mashirika hayo. Walikozipata wanajua wenyewe. Taarifa hizo hazina ithibati yo yote na ndiyo maana zinatofautiana. Niliwasihi waachane nazo, wazipuuze na wakipenda watoe tamko la kuzikataa.

Kwa upande wetu, yaani Serikali, imekuwa vigumu kukubali maombi ya kuliingiza swali la dini katika Sensa hii kwa sababu za kisera na kiutekelezaji.
Wakati wa ukoloni maswali ya rangi, dini na kabila la mtu yaliulizwa katika Sensa. Baada ya uhuru, maswali hayo yaliulizwa katika Sensa ya kwanza ya mwaka 1967 kwa vile ilikuwa bado inafuata misingi ya kikoloni.

Baada ya hapo ulifanyika uamuzi wa kisera wa kutokuuliza maswali hayo kwani nia ya wakoloni kuuliza maswali yale ilikuwa ni kwa sababu ya sera yao ya wagawe uwatawale. Walitoa huduma kwa ubaguzi, sera ambayo Serikali zetu ziliachana nayo baada ya Uhuru na Mapinduzi. Huduma hazikuwa

zinatolewa kwa ubaguzi wa rangi, kabila wala dini, bali kwa msingi wa haki ya uraia na ubinadamu wake.
Sera hiyo pia ilikuwa na lengo la kudumisha umoja na mshikamano wa taifa letu na watu wake. Badala ya watu kubishana juu ya watu wa dini ipi ni wengi na hivyo kufarakana kwa kutokubaliana na takwimu zilizotolewa, sera mpya inawataka watu wajivunie uwingi wao kama Watanzania.

Kwa hili Rais akasisitiza, “lNionavyo mimi Sera hii ni nzuri na kwamba ulikuwa ni uamuzi wa busara na hekima kubwa. Tuendelee kuidumisha na kuienzi. Kufanya vinginevyo, na hasa kuingiza sera ya kutoa huduma kwa misingi ya dini zetu ni kuliingiza taifa letu ambalo lina sifa ya amani, upendo na utulivu, katika migogoro isiyokuwa ya lazima. Ni migogoro inayoweza kuepukika kwa kuenzi na kudumisha sera yetu hii nzuri na sahihi.

Sababu ya pili inayotoa ugumu kiserikali ni ya kiutekelezaji. Imechukua miaka kadhaa ya maandalizi mpaka kufikia hatua hii ya sasa ya kuwa tayari kutekeleza zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, alisema Rais JK.
Isitoshe, Sensa ya majaribio imeshafanyika kwa kutumia vifaa, madodoso na maswali yaliyopo na marekebisho kufanywa baada ya hapo. Kuingiza

mambo au jambo jipya sasa itakuwa viguku kiutekelezaji. Kutachelewesha zoezi zima na kusababisha hasara kubwa kwa taifa, alisema.
Kuhusu Tume alisema haoni ulazima wa kuunda Tume Huru ya Sensa yenye uwakilishi sawa wa Wakristo na Waislamu. Tangu mwaka 1931 kazi ya

Sensa imekuwa inafanywa na Ofisi Kuu ya Takwimu nchini na ndipo ujuzi na maarifa yote yapo.
Hata ukiamua uiite Tume bado utawatumia watu hao hao, hivyo mabadiliko hayo hayana sababu. Vile vile, sioni haja ya kuwa na mgao wa wafanyakazi wake kwa msingi wa dini kwa sababu Sensa siyo kwa ajili ya kujua Wakristo na Waislamu. Huduma hazitolewi kwa misingi ya dini za watu, alisema.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

 
Duniani kuna mambo tembea uyaone aunjoo Tanzania ujionee maajabu
 
Anatapatapa tu, ooh mara nimeongea na wanaharakati wa kiislam kumbe kina mataka, wameanza kunote kaya zisizohesabiwa ili wakadirie
 
Back
Top Bottom