Rais Jakaya Kikwete Kwenye Kazi ya Upatanishi Huko Ivory Coast

Jan 16, 2007
721
176
WAKUTANAPO MARAFIKI WANAOFANA KWA VITENDO VYAO
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokelewa na Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo muda mfupi baada ya kuwasili jijini Abidjan kwa mazungumzo ya kutafuta suluhu na mpinzani wa Gbagbo Bwana Allasane Ouatarra. Rais Kikwete yupo katika jopo la kamati maalumu ya Viongozi wa Afrika walioteuliwa na Umoja wa Afrika(AU) kutafuta suluhu ya kisiasa nchini Ivory Coast.Viongozi wengine walio katika kamati hiyo ni pamoja na Rais Jackob Zuma wa Afrika Kusini,Rais Idriss Deby wa Chad,Rais Blaise Compaore wa Burkina Fasso na Mwenyekiti wa kamati hiyo Rais Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania.
 

Attachments

  • 3.jpg
    3.jpg
    91 KB · Views: 40
Tabasamu lake labda litaleta suluhu kwa hawa jamaa. Jamaa huwa anababaisha sana wasiomjua na haiba yake hiyo.
 
Anakaribihwa kwa kuamboiwa aisee wewe ulifanikiwa vipi kuchakachua nasikia uliambulia asilimia 34 kihalali? JK anajibu Mitanzania imelala doro so haiwezi kushtuka hivi sasa tuna mpango wa kujilipa dowans
 
Hapo ni kama anasema Dr. Slaa nae angekomaa kama Allasane ndie (Dr. Slaa) angekuwa hapa anasuluhisha!
 
ya kwake yamemshinda hapa nyumbani huko atasuluhisha nini kama sio unafiki mtupu. tatizo la dowans tu hata kulizungumzia anaogopa
 
Back
Top Bottom