Rais Jakaya Kikwete kuongea na Waandishi wa habari leo !

Wadau,

Leo majira ya saa 9 Alasiri, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Kikwete leo atakuwa na mkutano na waandishi wa habari Ikulu- Magogoni !

Tusubiri tuone atakuja na lipi !

Nawakilisha !

Anakutana na waandishi kuzungumzia nini?? Maana kila jambo ukiulizia jibu ni" HILO LIKO MAHAKAMANI; TUSIINGILIE MAHAKAMA".....Hakutakuwa na jipya huko leo..
 
leo halongi na wazee wa dar???
Hata hao Wazee walishamuona ni kilaza hivyo wameamua kumchunia! Siku zote amezoea kuwapiga blaaa blaa + usanii halafu hata mafao yao ya EAC au matibabu hawayapati, hivyo WAZEE WAMETUMIA AKILI ZA KUAMBIWA WAKACHANGANYA NA ZAO! Safari hii M.K.W.E.R.E hana audience, ndio maana kaita Waandishi wa habari maana hao lazima waende kupata habari kesho wauze magazetini! Hata ile hotuba yake ya mwisho wa mwezi hata Walalahoi wa Vijijini walishaona ni usanii mtupu! M.k.w.e.r.e bwana? Ama kweli jamaa ni JANGA LA TAFA!
 
Nafikiri anataka kujiuzulu rasmi hakuna jingine, kama siyo hivyo basi ni mambo ya mbayuwayu.
 
Kwani Bagamoyo ameenda lini mara ya mwisho? maana suprising kama hivi lazima 'wataalamu' wake kutoka Msoga wamshauri kwanza, zamani kidogo ilikuwa rahisi maana 'mlinzi' wake maalum Shekh Yahaya Hussein alikuwa anamtonya kwanza,

yote kwa yote tunaomba Source ya hizi taarifa.
Alikuwa huko weekend iliyopita, hukuona magazeti mengi kesho yake yalitoa picha akiwa amejilaza kwenye mkeka wa Bi. Kizee (85) mmoja pale Msoga? Hako kabibi ndio kakuu ka benchi lake la ufundi! Huyu M.K.W.E.R.E kwa ndumba? Ndio maana anaendesha nchi kwa mazingaombwe!
 
hana jipya ataenda kuchekacheka kama kawaida yake. huku wananchi tunashida tele
 
Source tafadhali: Jambo la walimu lipo mahakamani kama kuna luninga au redio itakwenda live.
 
Nategemea atazungumzia masuala yafuatayo

[1] Mgomo wa waalimu

[2] Matatizo ya TANESCO

[3] Mgogoro wa mpaka baina ya Tanzania na Malawi.

[4] Ikulu kuhusishwa na mateso ya Dr Ulimboka

[5] Sensa na kizungumkuti cha waIslam.

Hapo patachimbika !
 
Alikuwa huko weekend iliyopita, hukuona magazeti mengi kesho yake yalitoa picha akiwa amejilaza kwenye mkeka wa Bi. Kizee (85) mmoja pale Msoga? Hako kabibi ndio kakuu ka benchi lake la ufundi! Huyu M.K.W.E.R.E kwa ndumba? Ndio maana anaendesha nchi kwa mazingaombwe!

JF is never boring .... nimecheka ! watu mna midomo !
 
Atasema walimu wagome tu kwani serikali ya China imejitolea msaada wa walimu wa kutosha kwa shule zetu
 
Nategemea atazungumzia masuala yafuatayo

[1] Mgomo wa waalimu

[2] Matatizo ya TANESCO

[3] Mgogoro wa mpaka baina ya Tanzania na Malawi.

[4] Ikulu kuhusishwa na mateso ya Dr Ulimboka

[5] Sensa na kizungumkuti cha waIslam.

Namba 1 na 4 viko mahakamani mkuu
 
Ni hotuba ya kawaida ya mwisho wa mwezi, safari atatumia staili ya kuongea na waadishi wa habari. Msitegemee aongelee lolote kuhusu hii migomo kwani serikalini wanasema ni upepo tu utapita.
 
Alikuwa huko weekend iliyopita, hukuona magazeti mengi kesho yake yalitoa picha akiwa amejilaza kwenye mkeka wa Bi. Kizee (85) mmoja pale Msoga? Hako kabibi ndio kakuu ka benchi lake la ufundi! Huyu M.K.W.E.R.E kwa ndumba? Ndio maana anaendesha nchi kwa mazingaombwe!

nyani haoni kundule! wewe umeyajuaje hayo! kama si mshiki wa hayo.
 
Back
Top Bottom