Rais Jakaya Kikwete apigwa picha upya kwa matumizi ya kiserikali

samahanini kama nitamkosea yoyote, lakini picha ya sasa rasmi ya rais inamuonyesha kama ni lunatic hivi flani. the eyes and the smile......he appears high!

wandugu picha itazameni uzuri ikiwa kubwa, .....kisha muongee
 
Jamani, mie naona picha ya kwanza ilikuwa nzuri zaidi maana ilionekana yuko makini kiasi fulani. Likini hii uso wake unaonyesha kabisa tabia yake ya kutokuwa makini, unafiki na uswahili!
 
Hawa mafisadi wajanja sana wameanaza kukusanya za campaign 2010 wameona hakuna tena mahali pa kuzoa kama EPA wameamua waanze kukusanya kidogo kidogo leo vitambulisho vya uraia, kesho picha ya JK na watahakikisha kila mtu ananunua hizo picha tena kwa lazima.

Walikuwa wapi siku zote wasione picha ni mbaya kama wameweza kukaa miaka mitatu why not wait for 2 more years
 
Reserve your coment till the new picture is released, ndo tucoment kwa kuzilinganisha the tuombe cost ya hizo picha kwa taifa.
 
Jamani tunazidi kuchoka kifkra na kila kitu.....
Kila sector lazima ibadili hizi picha nasikia zinauzwa 15000/= sasa sijui hii tenda nani kapewa....
 
Jamani tunazidi kuchoka kifkra na kila kitu.....
Kila sector lazima ibadili hizi picha nasikia zinauzwa 15000/= sasa sijui hii tenda nani kapewa....

Tatizo si nani kapewa ila Je TEnder ilitwangazwa?Mie sijawahi kuiona hata Gazetini..

Nimeiona Picah Mpya ya Rais kwa michuzi,hii kaonesha smile na kavaa tai nyekundu..
 
wapige tu nyengine .. maana hiyo picha ya zamani ngozi yake imepauka si kidogo lakini sasa navimafutamafuta ... uso unangara vizuri ... hata vishavu vimenona .... nitachangia shilingi 50 ....eeeeh maana apendeze hata kwenye noti awekwe tu .... tumechoka jamani eeeh .. wafanye wanavyotaka
 
Vikao Vingapi Vilifanyika Kujadili Hiyo Picha?
Per Diem Kiasi Gani Ya Vikao?

Kila Picha Itauzwa Sh 15,000 ???? Kampuni Gani Inatengeneza Hizo Picha?

Summary: Kuna Mtu Katafutiwa Ulaji.
 
Serikali imebadilisha picha rasmi ya Rais Jakaya Kikwete kutokana na kubainishwa kuwa kwa kiwango kikubwa inaonyesha dalili za msongo wa mawazo ya kampeni za uchaguzi mkuu 2005.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Bw. Kassim Mpenda alitoa taarifa hiyo jana jijini Dar es Salaam.

Alisema uamuzi wa kubadili picha hiyo umefikiwa kufuatia ushauri wa wataalam kwamba picha ya sasa haifai kuendelea kutumika kwa sababu hizo.

Alisema picha inayotumika hivi sasa ilipigwa baada ya Tume ya Taifa ya uchaguzi kumtangaza Rais Kikwete mshindi wa uchaguzi huo.

Aliongeza kuwa makatibu wakuu na maofisa wafawidhi wengine wote wa ofisi za serikali kuu, serikali za mitaa, wakala na asasi nyingine zote za serikali wameshauriwa kuanza kutumia picha mpya ya Rais.

``Kila nakala ya picha hiyo itauzwa sh. 15,000 na zitapatikana mwanzoni mwa Julai katika Idara ya Habari.

Wakati huo huo, serikali kupitia wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, imekamilisha uchapishaji wa bango la baraza jipya la mawaziri.

Alisema nakala zake haziuzwi zinatolewa bure na ofisi ya Idara ya Habari (MAELEZO) kuanzia jana.


I wonder when was the new picture taken. Kama kweli sababu ya kubadilisha picha ni msongo wa pilika za Uchaguzi ambao JK alikuwa na uhakika wa asilimia 99 kushinda, inawezekana hali tete ya taifa na serikali kwa sasa iliyosababishwa na kashfa baada ya kashfa inaweza ikafanya picha hiyo mpya iwe mbaya zaidi. Pia huyo mtaalamu wa picha inawezekana ni laziest person ever. Ameacha hiyo picha iwepo all this time ndio anagundua leo. Hii ni kama bollocks.
 
Haja ya kubadilisha picha yuko nayo, anatuonyesha ana ama amepata matatizo ya macho,ndiyo maana hali ya nchi haioni.
 
haikuwa na haja ya picha mpya......ukizingatia picha mpya rais is not looking serious at all.
mie namuona kakaa kama yupo high....au sijui walimpa avute kidogo kabla ya picha!
 
wapige tu nyengine .. maana hiyo picha ya zamani ngozi yake imepauka si kidogo lakini sasa navimafutamafuta ... uso unangara vizuri ... hata vishavu vimenona .... nitachangia shilingi 50 ....eeeeh maana apendeze hata kwenye noti awekwe tu .... tumechoka jamani eeeh .. wafanye wanavyotaka

Siku zote hiyo sura yake imepauka na kukakamaa kama nini hamna cha uhandsome wala mashavu kazi kula intercontinental cuisines huku watu wanakufa njaa halafu shavu.Shavu twampa sisi yet anajifanya mjanja we ngoja tu yatamtokea puani one day.
 
Mambo mengine huwa ni ya kujitakia!

Kwa nini hawakutoa Picha na tamko fupi kuwa "Serikali imetoa picha mpya ya Rais" bila kuanza kutoa sababu miatano?

Tunajua watu huzeeka, rangi hubadilika na kadhalika, sasa wanafungulia nyuki wanapoanza mambo ya alikuwa kachoka wakati wa Uchaguzi, je sasa katulia na kuna sekeseke za Ufisadi?
 
Mimi naona nikitu cha kushangaza kutumia mahela mengi ya wafuta jasho kubadili picha tu.Sisi hatutaki uzuri wa face tunataka vitendo na maendeleo.Who looks at that face anyway.Jk is growing old tutakuwa tunabadili kila akipata ka wrinkle au grey hair???
 
Ninashauri tubadilishe utaratibu huu. Mahakama kama bunge ni mhimili mwingine wa serikali unaotakiwa kujitegemea. Ni muhimu vyombo vya mahakama na bunge viwe vinatumia coat of arms (ngao ya adam na eva) na bendera ya taifa tu, siyo sura ya rais; Vile vile kila kimoja kinatakiwa kuwa na nembo yake. Picha ya raisi iwe inatumika katika ofisi za serikali zinazonfaya kazi chini ya executive branch tu.

Kichuguu,
Nakubaliana na usemi wako na ningependa kuongezea kuwa, picha ya raisi kuwepo maofisini kunaleta hali ya kuwa kama tunamtukuza au hata kumuabudu mhusika (pledge alegiance kwake), badala ya sisi wote pamoja na yeye kuwajibika kwa taifa letu.

Potrait ya raisi ilitumika kwenye nchi za mashariki kwa nia ya kuwafanya watu wamuogope kiongozi wao, sijui kwetu iliingiaje. Wakati sasa umefika wa kuondolewa huu utaratibu kabisaa. Nafikiri nchi kama za US wao hutengeneza potrait ya raisi akiwa anaondoka madarakani. We can immitate that, why not.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom