Rais Jakaya Kikwete amteua Bwana Hussein A. Kattanga kuwa Mtendaji Mkuu wa Idara ya Mahakama

kabla ya kuja kinondoni alikuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mbinga, then akaletwa kinondoni kuchukua nafasi ya berege aliyepelekwa kuwa mkurugenzi songea, wakati yuko kinondoni alifanikiwa kupanyosha vilivyo na hatimaye akapandishwa cheo na kuwa RAS wa singida na baadaye akahamishiwa kuendelea kuwa RAS morogoro. Mungu jalia akapata promotion ya kuwa naibu katibu mkuu wa wizara ya ustawi wa jamii na mwishowe akaja kuwa katibu mkuu wa katibu wa tamisemi but by profession ni mhasibu.
 
Hili ni balaa, Hussein Katanga aliwahi kuwa mkurugenzi wa wilay mbinga, akachukua chake mapema na kujenga gorofa zake ale ngongo la mboto na kwa vile ni sehemu yao, akapelewkwa ofisi ya waziri mkuu. Kweli nchi inaenda kubaya
 
Ila kwa nini mchapa kazi huyu ahamishwe hamishwe? Kwa nini asikae sehemu moja kwa muda mrefu ili aweze kuboresha? Mfano amekaa kinondoni miaka 3 pekee
Mtanzania haswa,
Maximum Standart time ya Mtumishi wa Serikali kutumikia sehemu moja ni Miaka mitatu tu. Wataalamu wa Utumishi wanasema kwamba Mtumishi akikaa sehemu moja anajijengea mazoea mabaya ya kazi ambayo yanapunguza ufanisi.

Mfano mtumishi anapokaa muda mrefu sehemu moja anaanza kujenga tabia ya kuchelewa kufika kazini kwa sababu anakuwa amejenga familiarity na mazingira ya kazi (Maboss, nk). Na hata kupewa punishment inakuwa ngumu kwa sababu hizo hizo za kujenga familiarity na mazingira ya kazi. Ni jambo la kushangaza sana kuna baadhi ya watumishi wanzia kazi sehemu moja wanakaa zaidi ya miaka 7, 10, 15, 20 na hata kustaafia hapo hapo.

Pia watumishi wanahamishwa hamishwa ili kusumbaza ujuzi na uzoefu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Through uhamisho watumishi wanaweza ku emitate from each others the best way of doing things.


TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),

tumbiri@jamiiforums.com
 
Nami nimeshangaa sana kusikia Rajab Kiravu ni msabato!ule usanii wote ule na wizi ,udanganyifu kweli ukiwa sirikalini lolote lawezekana!

Mkuu Skills4Ever,
Utaumia sana kama Utaoanisha majina ya watu na Dini zao! Hivi hushangai data zinazotolewa na viongozi wako kuhusu idadi yenu na data zinazotolewa katika Operation ya Vua mkono wa Sweta ktk baadhi ya mikoa kufikia 26%? Nchi hii ina mchanganyiko wa ajabu sana! TAFAKARI
 
Siku zote ni jambo la kuondoa simanzi kuona watu wenye weledi wa maoni na uadilifu wa rai na silika miongoni mwa Watz, kama mkuu Mzalendo kweli. Juu ya dini, amesema kweli na haki, i
ngawaje yeye mwenyewe ni Mkristo kama alivyoeleza. Kuna wakati kaatika miaka ya 60,70,80 wakati Baraza lote la Mawaziri huwezi kupata zaidi ya Waislamu wawili au watatu. Waislamu walivumilia wakati huo naa hawakutoa kauli yeyeto kwa vile walijua ukosefu wao wa elimu za kisasa. Hivi sasa hali hiyo imeebadilika, kwa nini Wakristo wengine wanaona hali ya zamani izidi kuendelea na kusiwe angaalau na balance? Inasikitisha kwa hawa Wakristo wanaozua uini kwa sababu hadi leo badi Wakristo ni wengi katika nafasi za uongozi wa serikali na maidara kuliko Waislamu. Lazima wafahamu kuwa hali ya zamaani haiwezi kuendelea kama mkitaka amani ya nchi. Angalau tuanze sas kukubali fikra ya kuwa maadam Waislamu nao wamesoma, basi kigezo pekee sasa kiwe ni kiwango cha elimu na utenda kazi.
Kuhusu rais kuteuwa viongozi wa sheria, hii kwa kweli ni kasoro kubwa. Watu kama hao hawawezi kamwe kuibana serikali.
 
Acheni utoto, hakuna udini katika hili. Ukiona mtu anasema udini udini ujue yeye ndo wa kwanza kuwa mdini!
 
JK anampenda sana kattanga..alianza kama mkurugenzi manispaa ya kinondoni ..amepanda kwa kasi sana kwenye system

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Lakini hili la kutoka Katibu Mkuu TAMISEMI kwenda Mtendaji wa Idara ya Mahakama siyo demotion kweli?
 
huyu lazima atakuwa ni shemeji wa binamu yake kwa baba mwingine ambaye walisoma wote mido skuli, maana ndio criteria za bw mkubwa ktk uteuzi,
 
Teh teh inauma eh? sasa ndio na wewe ujisikie yale machungu ambayo wenzako tumekuwa tukiyasikia tokea enzi za Nyerere!
Big up Jey Key!
badala ya kumoderate kwahiyo ni jino kwa jino. hizo agenda za siri za uteuzi wa hawa watu ndizo zinazowatia shaka watu. inawezekana jk asiwateue kwa udini, yeye anawateua ili kujihakikishia ngome imara yake mwenyewe. adhawaizi this is a shortliving strategy
 
Hatuwezi kuepuka kuzungumzia UTEUZI kwa kigezo cha UDINI pia UKANDA (hususani KANDA YA KUSINI i.e LINDI&MTWARA) hususani kipindi hiki ukianza (kote kwenye CHAMA na sirikalini 1. DINI: Makamu(Mzee wa Mikasi), KAWAMBWA, GHASIA, MAJALIWA,KIGHODA,MAKAMBA, KAGAASHEKI 2. UKANDA:MEMBE,MKUUCHIKA, CHIIIKAWE,3. MAKATIBU WAKUU:................... 4. RAS........... 5. RC's ........... 6. DC's......................
****USHAURI: Ndani ya katiba mpya itamkwe UTEUZI uzingatie sifa (merit) na hata kama Mkuu ndo atakuwa anateua lazima awasiliane na mamlaka nyingine eg. Bunge kabla ya kufanya FINAL APPOINTMENT. Vinginevyo tutajenga watendaji washkaji wa Mhe. Mkuu.
 
Hussein katanga ni mwajibikaji , anastahili tu. nachohoji ni Mamlaka makubwa ya rais kuteua kila mtu, hivyo basi na mimi leo namteua mke wangu kuwa mtunza hazina mkuu wa familia, namteua mwanangu mecky kuwa mkuu wa mkoa wa chumba chake cha kulala ili mradi tu kuteue teua.
 
Huyo jamaa ni miongoni mwa watendaji waliojuu sana kwa utendaji wa kazi zao hapa Tanzania sasa hivi, jamaa anafanya mambo makubwa kwa muda mfupi popote anapopita! na kila anapoondoka wafanyakazi humlilia, alitokea Mbinga kama Mkurugenzi akaliliwa, akaenda Kinondoni manispaa akaliliwa na wafanyakazi, akaenda Singida kama RAS na alipoondoka akaliliwa pia, akaenda Morogoro kama RAS akaondoka akaliliwa, akawa naibu waziri kule Jinsia na watoto hapo hakukaa hata miezi 3 sina taarifa kama alililiwa mana sidhani hata kama ali deliver kitu. Akaenda TAMISEMI kwa muda mfupi amefanya mambo makubwa.

Kifupi ni mtu mzuri anayeweza kutuletea mabadiliko popote anapokuwa, ni mbunifu sana na mtu wa kupenda maendeleo kama sisi wana JF. Naomba kuanzia leo muanze kumfatilia then mtakuja pata majibu. Ila kama ameondoka TAMISEMI itakuwa sio nzuri mana alianza isuka TAMISEMI vizuri sana, na kurekebisha mifumo mingi ya TAMISEMI iliyokuwa inakwamisha mambo... kwa hilo uteuzi wake utakuwa umeinyima haki TAMISEMI..
 
Tatizo siyo jina lake wala anakotoka au dini yake. Tuangalie anaenda kuwa nani huko. Ninavyojua mimi mahakama, ni muhimili wenye changamoto nyingi sana, kuanzia human resource mpaka fedha. Lkn huko kuna mabosi wengi yaani CJ, JK, Jugdes wa CA, Judges wa H/C na wasajili. Muundo wa mahakama sasa ni tofauti na wizara au bunge.
yeye anakwenda kusimamia utawala wa rasilimali watu na fedha, wakati chief registrar anasimia utawala wa utoaji haki yaani admnistration of justice. Huu ni mfumo mpya ambao unamgongano wa madaraka na maslahi. Tatizo kubwa hapa ni sheria iliyoanzisha muundo huu. Kama atakwenda kuongoza mahakama kama halmashauri atakwama haraka sana, na nadhani kama kweli ni mtu makini atafanyakazi kwa muda mfupi tu na kuondoka. swali ni je atapokea maagizo ya nani kwanza ya Rais au jaji Mkuu- hii Kenya imewashinda ktk katiba mpya wamwondoa chief court administrator na kurudi kwa mfumo wetu tunaoutupa kapuni sasa, je ataweza? utendaji wake tu ndo utakao mlinda.
 
UDINI at work. Tanganyika kwa kweli kama msipoangalia hilo lazima litawamaliza na mtaangamia vibaya sana.
Hebu pitieni Katiba yenu ya Muungano ya JMTz, Sharia namba 15 Ibara ya 6 ya mwaka 1984. Kifungu cha 23
23.-(1) Kila mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote,
anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watuwote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo
kulingana na kiasi na sifa za kazi wanayoifanya.

Najiuliza kwanini mnabaguana kwa misingi ya DINI?

 
Mbinga mbona mbali alikua mkurugenzi wa halmashauriya kinondoni,alipambana sana na genge la kina londa na mdogo wake Regina lowassa,baada lowassa akapendekeza aondolewe pale,akapelekwa kuwa RAS sijui mkoa gani nimesahau
Ni kweli mbinga anafahamika zaidi kwani ndiko alikoibukia jamaa ki ukweli ni mchapakazi sana alikuja pale kama mhasibu msaidizi akapanda ngazi hadi akawa mkurugenzi wa halmashauri then akahamishiwa kinondoni baadae akateuliwa kuwa RAS singida then morogoro baadae akateuliwa kuwa naibu katibu mkuu wa wizara (nimeisahau)na baadae ndo akaenda TAMISEMI. kifupi jamaa ni jembe...bt ttz langu ni kupelekwa idara ya mahakama wakati jamaa professionally ni mhasibu
 
Back
Top Bottom