Rais J. Kikwete na siri nzito ya taifa hili kujulikana 2014

Wenye akili wanaona na kuthamini kazi ya JK kama mwanzilishi wa hii post hii alivyoona,lakini wengine wamekalia chuki binafsi tu dhidi ya mh. Rais na wako tayari kumkwamisha ili aonekane hafai bila kujali gharama yake kwa watanzania.Lakini pamoja na yote Kikwete atabakia kiongozi bora TZ.
Kama huyu unamuona ni kiongozi bora, basi ni bora kwa familia yako na ndugu zako. Wengine sisi tunamuona ni mkosi na janga kwa taifa.
 
Najiuliza wewe uliyeleta hii thread ndo jk mwenyewe, au ni hisia zako tu ama umetumwa na jk mwenyewe?
 
Hakuna lolote huyo rais wenu, amalize tu muda wake ajiendee kwao 'akapumzike kwa amani'. Kama ni suala la katiba hilo wala siyo suala la kutuburudisha, hiyo ni haki yetu wala siyo hisani. Rais gani anakuwa madarakani miaka 10 lakini nchi inakuwa Kama haina kiongozi!? Aende zake huko.

Mimi na niwe Tomaso, sintaamini mpaka nimeona kwani I do not see any light at the end of the tunnel!! Sioni ishara yeyote yakunipa matumaini ila naona hila tu ya kutaka kupoka haki ya wananchi ya kujitengenezea katiba waitakayo; kwa Rais kuvunja sheria aliyoitia saini mwenyewe kwa kuteua mbunge na mwakilishi kwenye tume ya katiba contrary to the law, hata miezi sita haijapiata; hiyo siyo ishara nzuri!
 
Rais angekataa hiyo hoja unayosema ya Chadema unadhani leo ingekuwepo? Si unajua Rais alikuwa na uwezo wa kuikataa hoja ya katiba mpya kama angetaka, lakini hakufanya hivyo na ata baadhi ya mambo alipishana na chama chake ambacho ni Majority. Ndio maana mleta mada anamsifia Rais na kweli kwa hili Rais anastahili sifa tele. Unafikiri ni nani aliyemteua Prof. Baregu (CDM) kwenye Tume ya Katiba? Jibu ni Rais, sasa kwanini usimpe sifa yake anayostahili? acha unazi pori.
Kibara usiyejitambua wewe.WEKA UTAIFA MBELE.
 
Kama huyu unamuona ni kiongozi bora, basi ni bora kwa familia yako na ndugu zako. Wengine sisi tunamuona ni mkosi na janga kwa taifa.
Unajua hata mirembe kuna viongozi wa machizi yaani machizi wenye nafuu.usikute na huyo prez wao wa taipu ile.
 
Nyota njema hutambulika tangu alfajiri. Tangu aingie mamlakani Kikwete amekuwa ni janga la taifa. Tutamkumbuka kwa kuuza utu wetu na raslimali zetu, huku yeye na familia yake wakitajirika kupita kiasi.
 
take frome nimesema uwenda wanajuwa ama hawajuw kabisa, pia nilazima ujuwe ikiwa katiba haimpi mtanzania fursa ktk rasilimal zake bas nitatizo. Kikwete anaenda kupiga lami watanzania tupite kwakujidai.
Hakuna cha lami hakuna cha kujidai. Ni masononeko tu kama vile tumeuzwa utumwani.
 
Rais lazima asifiwe kwa swala la katiba maana wabunge wa upinzani bungeni ni wachache sana wasingeweza kushinikiza swala la katika. Na CCM wangetaka wangekataa katiba mpya, bila ya intervention ya rais kusingekuwa na katiba mpya. Kikwete anapata upinzani ndani ya chama sana kwa mambo kama haya.
Kilichomshinikiza Kikwete katika katiba si uoga wa wabunge wa upinzani. Aliogopa people's power. Kikwete anajua kuwa hakushinda uchaguzi wa 2010. Chadema kinaweza kuwa na wabunge wachache lakini kina ushawishi mkubwa nchini. Hilo analijua Kikwete. Tuendelee.
 
Namtakia rais wetu mafanikio katika hili la katiba ila wengi hawatapenda/hawapendi maendeleo na mabadiliko anayoyafanya kwa manufaa ya nchi yetu. Mola mbariki rais wetu na tanzania kwa ujumla,

Kiakili wewe fanana matonya,
 
Rais angekataa hiyo hoja unayosema ya Chadema unadhani leo ingekuwepo? Si unajua Rais alikuwa na uwezo wa kuikataa hoja ya katiba mpya kama angetaka, lakini hakufanya hivyo na ata baadhi ya mambo alipishana na chama chake ambacho ni Majority. Ndio maana mleta mada anamsifia Rais na kweli kwa hili Rais anastahili sifa tele. Unafikiri ni nani aliyemteua Prof. Baregu (CDM) kwenye Tume ya Katiba? Jibu ni Rais, sasa kwanini usimpe sifa yake anayostahili? acha unazi pori.
Ndiyo, Kikwete angeweza kukataa hoja ya katiba. Lakini yangemtokea puani. Na yeye analitambua hilo.
 
Mimi sijakuelewa, una maana ndani ya hiyo katiba mpya ndo kuna siri nzito? Kama ndivyo basi hamnazo maana katiba mpya ilikuwa ndani ya ilani ya chadema wala siyo ccm. Sikuelewi kivipi katiba mpya ndo ibebe siri nzito wakati ni shinikizo la wapinzani wala hawakuwaza kitu hiki wakati wanachakachua ushindi?

Logically kama binadamu, hakuna kitu kikubwa unachoweza kukifanya Ndani ya miaka mitatu kikizidi yale uliyofanya ndani ya miaka saba?

Kwa hiyo kama kunakitu kikubwa kinakuja basi hakiwezi kuzidi yale Ya miaka saba iliyopita.

Katiba mpya haiwezi kuwafunga mafisadi kama ccm ikiendelea kuwa madararkani.

Mkuu siri nzito ambayo mimi naweza kuifikiri ni kuKiua chama chake na kuwakabidhi nchi chadema.

Kama anaenda kuhakikisha ccm inakufa basi ni wazi kila mtu atampongeza maana shida zote za nchi hii ni kwa sababu ya Ccm. Hili ndo pekee ambalo tutampa hongera kwa kuupigania upinzani akiwa mwenyekiti wa ccm. Ila kwa swala la maisha bora hilo tusahau hata tukimwongezea miaka mingine mitano


Mungu ibariki Nchi yetu na Mungu nipe maisha marefu tukashuhudie ukuu wako .
 
aargh kachelewa mno, kwa nini kawaachia wamekula weee mpaka wamesaza halafu eti aje na mpya mh siamini kwa kweli, jamaa DHAIFU MNOOO!
 
hii post ya tumainiel is simply a satanic deception kama sio mwelevu unanasa. Revisit your mind game 101 classes pana kipande umeruka kwenye huu uongo wako.
 
Tumaini,

1) Ni nini faida ya kuchagua (kuchakachua) kiongozi kwa muhula fulani halafu useme atafanya vizuri mwishoni wakati mwanzo na katikati ya uongozi wake hakuna viashiria bayana vya mwisho kuwa mwema?

2) Nakumbuka vema toka wakati anaingia ikulu wengi wa wapenzi wake walikuwa wanasema usemayo kuwa anaijua vema nchi, anajua kila kona, ni mjanja, ni handsome nk lakini nikuulize swali; Kwa nini hakufanya hayo "mazuri" mwisho mwa muhula wa kwanza? Kwani ktk demokrasia ya vyama vingi angehatarisha kupoteza urais 2010 then "kazi na mpango wake" usingehitimishwa.

3) "Ni heri chuki ya wazi kuliko upendo uliiofichika". Hiyo siri aliyonayo ambayo inawafanya wenye kutumaini mwisho wake utakuwa mzuri ni ipi ikiwa hajaonesha wazi upendo wake kwa nchi? Amejaza na kukumbatia washkaji kibao. Angalia ishu za Nyalandu, Malima, Ngeleja, Jairo, Richmond, EPA Part II, Udini nk kutaja machache.

4) Sio kwenye mada hii wala kwingineko nimewahi kusoma hoja zenye mashiko na mtiririko wa kimantiki kuhitimisha usemayo. Zaidi huona hisia na itikadi zaidi.

5) Huoni ingawa ulikusudia kuonesha +ves kuwa pia kuna element za -ves kwani kama mpango na siri ni kufanya vizuri 2013/14 then kwa nini alipoteza muda na rasilimali za taifa muda huu wote, si angesubiri muda huo ndio agombee?
 
msifananishe huyu mtu na baba wa taifa, huyu hakuna kitu, kwa nini asuburi kufanya mwishoni wakati nchi inaibiwa? ina maana anataka aache mifupa ndo mfurahi? hicho ni kichwa cha nazi!!

Mjomba unafikiri kila atakaye fanana na baba wa Taifa lazima atoke butiama tu? kwenye white tuseme kama ilivyo na ikiwa black tuseme black, mchakato wa katiba utaleta majibu mengi ambayo maswali yake tangu uhuru hayana majibu! maswali hayo wana JF wanayajua mi siyataji.... kazi nzuri tumpe support JK.
 
Hakuna lolote huyo rais wenu, amalize tu muda wake ajiendee kwao 'akapumzike kwa amani'. Kama ni suala la katiba hilo wala siyo suala la kutuburudisha, hiyo ni haki yetu wala siyo hisani. Rais gani anakuwa madarakani miaka 10 lakini nchi inakuwa Kama haina kiongozi!? Aende zake huko.

Tutajie mema waliofanya marais wa kabla yake ambayo yeye hajafanya zaidi yao. Nakuhakikishia utatafuta sana hulipati hata moja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom