Rais J.K hateui wakuu wa Mikoa na Wilaya, kulikoni?

Yakuza

Senior Member
May 22, 2011
114
43
WanaJF

Mbona Rais J.K ana kigugumizi cha kuwateua wakuu wa Mikoa na Wilaya? Je, pengine amekubali kuwa wakuu hawa ni mzigo kwa taifa? Au ni nani awemo na asiwemo nalo ni tatizo? Au ni tatizo la kifedha?

Ni takribani mwaka mmoja sasa, mikoa na wilaya nyingi hazina viongozi hawa......kulikoni? Hakika haijawahitokea Uhuru NCHI ikawa hivi.

Mwenye habari za uhakika......tafadhari tujuzeni.
 
.....................Anajua kuwa tuta-mgadafi muda si mrefu sasa aangaike na maendeleo ya taifa ya nini? sasa hivi anakula na Mama Salma na Ridhiwani....
 
WanaJF

Mbona Rais J.K ana kigugumizi cha kuwateua wakuu wa Mikoa na Wilaya? Je, pengine amekubali kuwa wakuu hawa ni mzigo kwa taifa? Au ni nani awemo na asiwemo nalo ni tatizo? Au ni tatizo la kifedha?

Ni takribani mwaka mmoja sasa, mikoa na wilaya nyingi hazina viongozi hawa......kulikoni? Hakika haijawahitokea Uhuru NCHI ikawa hivi.

Mwenye habari za uhakika......tafadhari tujuzeni.
Kwa kutokuwepo kwao kume-athiri nini?
 
Sitamani hata awachague, ila linalonikera zaid ni hawa wanao kaimu wanakula mshahara mara mbili. Kikwete amechoka, ameichosha ccm, hajielewi anachopaswa kufanya. Tunaongozwa na mtu asiyejua kwann anatuongoza, asiyejua shida zetu. Tusitegemee mambo mazur, tutegemee maafa zaid.
 
Habari za ndani zinasema kila kukicha anabadilisha list..........

Pengine baada ya Eid anaweza kuwatangaza wakuu wa Mikoa!
 
Zitto alisema Serikali imefirisika - wengine wakabisha. sasa huu ndiyo uthibitisho kwamba CHADEMA huwa hawakurupukagi.
 
jamani hili swali mbona mnalirudiarudia kuuliza?

mh. pinda alishajibu kuwa uteuzi wa wakuu wa wilaya na mikoa unangoja kukamilika uundwaji wa mikoa mipya

hilo ndili linalokwamisha wapendwa

mbarikiwe
 
Nampongea sana Rais Mkwerre kwa hili, na ninamsihi aendelee na msimamo huu mpaka mwisho wa muhula wake ( kama tutaendelea kuivumilia serikali yake dhaifu. )
Wakuu wa mikoa na wa wilaya hawana tija kwa Taifa na mzigo wa kujitakia.
 
Bado kidogo jamani wenzenu bado TUNABANA MATUMIZI YA SERIKALI kutuzibia walau hata kwa kiasi kidogo tu; si mnajua tena UCHAKACHUAJI wa hapo mwaka jana ulivyotugharimu si kidogo.

Kwani wakuu wa mikoa na wilaya mnawahitaji wa kazi gani wakati wanamtandao wapo na wanatosha kabisa kutoa jibu ya kero zenu. CCM na serikali si ni KITU KIMOJA kilekile jamani???????????????

Kitakachowashinda hao viongozi wetu wa CCM Mikoa, Wilaya na Kata basi katuleteeni huku Magogoni tutashughulikaa!!!!!!!!
WanaJF

Mbona Rais J.K ana kigugumizi cha kuwateua wakuu wa Mikoa na Wilaya? Je, pengine amekubali kuwa wakuu hawa ni mzigo kwa taifa? Au ni nani awemo na asiwemo nalo ni tatizo? Au ni tatizo la kifedha?

Ni takribani mwaka mmoja sasa, mikoa na wilaya nyingi hazina viongozi hawa......kulikoni? Hakika haijawahitokea Uhuru NCHI ikawa hivi.

Mwenye habari za uhakika......tafadhari tujuzeni.
 
jamani hili swali mbona mnalirudiarudia kuuliza?

mh. pinda alishajibu kuwa uteuzi wa wakuu wa wilaya na mikoa unangoja kukamilika uundwaji wa mikoa mipya

hilo ndili linalokwamisha wapendwa

mbarikiwe

Miss Judith, uundwaji wa mikoa mipya uko tayari kwa maana uliishatoka kwenye government gazet. Labda kama kuna jingine.
 
Anataka waliopo watajirike ipasavyo

Angalia Mkaimu wa Mkoa wa Dar ana Dar and Lindi alikuwa ni mkuu wa Mkoa wa Lindi, hakutaka wa Pwani akaimu akachagua wa Mbali Lindi

Yeye na Familia wanaishi Hotelini Dar? Sababu kwao ni Lindi... ULaji huo

JK Nyerere Yuko Wapi?
 
Hapo umenena Mkuu. Nadhani J.K anaogopa kugomnanisha friends atakapochagua wachache na kuwamwaga wengine.
 
Mbona maisha yanakwenda vizuri bila hao wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya!ILI KUBANA MATUMIZI KTK KIPINDI HIKI KIGUMU NI VYEMA ANGEWAPUNGUZA KABISAA,kwani kuna WAKURUGENZI,MAAFISA TAWALA na WABUNGE wanatosha kuhamasisha maendeleo ktk mikoa na wilaya,ktk kipindi kama hiki serikali inakabiliwa na uhaba fedha ni vyema matumizi ya fedha ya kabanwa kwani hawa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanagharimu mishahara minono,marupurupu na maghari na hata nyumba.nchi ina hali ngumu kwasasa.
 
Tatizo letu watanzania hatuoni kuwa hiyo ni serious ommission on the part of the president. Nafasi ya RC ni nafasi iliyoundwa chini ya Ibara ya 61 ya Katiba na kazi zake zipo bayana chini ya Ibara 61(4) ya katiba, Kutoteua watu kuziba nafasi hizo kunasababisha ombwe la uongozi kitu ambacho sio vizuri katika utawala bora.

Anavunja katiba aliyoapa kuilinda na kuiheshimu.

Ni hatari Mkuu wa Nchi akianza kuvunja katiba, kesho hatujua atafanya uvunjifu gani wa katiba na kwa uzito upi.
 
[1] Hivi wakuu wa Mkoa na Wilaya wanafanyakazi gani ?.

[2] Mkoa wa Dar na Kilimanjaro haina wakuu wa mkoa je mikoa hiyo imekosa maendeleo,ulinzi na usalama ?. Jibu ni hapana wakuu wa mikoa na wilaya hawana kazi nafasi zao ni zakikoloni zaidi.
 
jamani hili swali mbona mnalirudiarudia kuuliza?

mh. pinda alishajibu kuwa uteuzi wa wakuu wa wilaya na mikoa unangoja kukamilika uundwaji wa mikoa mipya

hilo ndili linalokwamisha wapendwa

mbarikiwe

Mikoa mipya inahusiana vipi na wakuu wa mikoa iliyopo, Pinda ameishazoe kujibu ushuzi. Watanzania wenye uwezo wa kujaza nafasi wako kibao na hata kesho akitaka anawapata na hiyo mikoa mipya ikija anawapata wengine no need to wait kwa hiyo mikoa ya kichina.
 
[1] Hivi wakuu wa Mkoa na Wilaya wanafanyakazi gani ?.

[2] Mkoa wa Dar na Kilimanjaro haina wakuu wa mkoa je mikoa hiyo imekosa maendeleo,ulinzi na usalama ?. Jibu ni hapana wakuu wa mikoa na wilaya hawana kazi nafasi zao ni zakikoloni zaidi.
Mkuu wa mkoa kazi yake ni kutoa taarifa za kiintelijensia Chadema wakiitisha maandamano na pia kwenda kuwapokea Mama Salma na Riziwani wakitembelea mkoa wake. Na kazi nyingine kuchangisha fedha na vifaa vya ujenzi kwa wahindi akisingizia za kifanyia kazi za maendeleo kumbe anaenda kujengea nyumba yake kwao
 
Back
Top Bottom