Rais J.K: Anapolala kwenye msiba Malawi wakati Dodoma si shwari!

Yale Yale ya wivu wa kike aisee, yeye ni rais wa nchi kwenda msibani kwa rais mwenzake ni haki yake. Cdm JK anawasumbua sana aisee mtakoma


Eti kwenda msibani kwa rais mwenzie ni haki yake! Hivi hilo bichwa lako linatope au? Mbona unaonekana kutetea ujuha unaofanywa na mtu mzima mwenye akili timamu! Hivi kuna jana gani ya kuzunguka huku na huko ili hali nchi iko kwenye critical point kiasi hiki,,mwambie rais wako safari hazitatui changamoto zinazomkabili! Na wewe tumia kichwa chako kufikiri sawia,,,
 
Brazil amekaa siku tano tu kutoka tarehe 15 hadi 21 aliporejea nchini jaribu kuwa mkweli.

uongo si moja ya sifa ya jukwaa hili
 
si ndiye mlie mchagua wacha hamalizie mda wake bwana ameshatuchosha sana

kura yako pia ilikuwa ya ndiyo vipi unakataa hapa Jf.

kura ni siri yako tutajuaje kama hukutoa kura ya ndiyo..... kutuambia tukuamini kwamba ulipiga kura ya hapana wakati ulikuwa peke yako wakati wa kuweka alama ya ndiyo na hapana ni kutupotezea muda hapa.
 
Nchi haendeshwi kwa maoni binafsi, Kama Rais anamajukumu ya ndani na nje ya nchi. Badala ya kuongea ya busara na maana tunafanya mambo ya ushoga. Tuongee point kimsingi. Rais ninaimani analishughulikia jambo labunge kwa makini sana. Zitto anatafuta umaarufu wa kugombea Urais tu.

Taarifa kwa umma kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu iliyotolewa jana hukuiosoma? Ilisisitiza kuwa Mhe Dkt Col (Mstaafu) Rais JK hakuwasiliana wala kuonana na Waziri Mkuu kabla ya kuelekea Lilongwe na anasubiri taarifa rasmi kutoka bungeni. Tukuamini wewe au Rweyemamu?
Pili, sidhani nyie walamba viatu vya mafisadi kama mtaweza kuwakatisha tamaa wapambanaji dhidi ya ufisadi kwa kauli za kuwabeza eti wanatafuta umaarufu wa kugombea urais! Hata hivyo katika siasa huwezi kufanikiwa bila kutafuta umaarufu. Hata Dkt col JK alipo anatafuta umaarufu ili aendelee kukaa Ikulu. Ni bora kutafuta umaarufu kwa kuwakemea Mafisadi kuliko kuutafuta kwa kuwakumbatia mafisadi.
:A S angry:
 
Huyu Baba nadhani hata mwenyewe hajielewi! Hivi lile pepo lilokuwa linamtupaga liliishia wapi? Labda kwa upande mwingine ndilo lililokuwa linamsaidia.

liliondoka na Yahya wa Magomeni
 
Dodoma si shwari kwa nini? kuna tatizo lipi Dodoma wakati magwanda hawana ubavu tena wa kuanzisha maandamano yasiyo na mpango!
 
unajua mtu mjinga hutamfahamu akiwa kimya na akava nguo safi ila matendo tu yanaweza kukujulisha humu hakuna kitu ndio kilicho kwa baadhi ya wachangiaji humu ndani tusifikirie sana msiba bali tuwaze nini cha weza tokea ndani ya nchi kwa ujinga wa group watu au mtu mmoja (rais). hii haihitaji kwenda chuo kikuu hata ingekuwa ni wewe matamushi anayotoa "huu ni upepo utapita" is really huyu mtu ana akili timamu au anatakiwa akapimwe IQ yake? tutumie akili kutoa maelezo hili ni jukwaa la kupashana na kuelimishana
 
Hakika Mhe. Rais Kikwete ametuangusha sisi tuliokuwa wapambe wake! Ni Rais asiyeweza kufanya maamuzi na kwa kweli hajali hali ya wananchi wake........Yeye ni safariiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii hadi lini jamani? Hizo gharama zote ni juu ya sisi wanyonge!

Mpaka inafika October 2015, kazi tunayo kwa aina hii ya Rais wetu!

Mwenyezi Mungu, tusaidie watanzania!
 
Ndugu wanaJF

1. Inashangaza sana, Rais J.K amekuwa huko Brazil kwa takribani siku 10
2. Mhe. Rais amerudi na kuelekea kwenda kulala msibani Malawi.....wapi na wapi Rais mzima kulala msibani?
3. Malawi juzi juzi wametuma ndege zao kuvinjari mpaka wetu katika Ziwa Nyasa (Hoja ya Mhe. Komba)
4. Nchi imegubikwa na wimbi zito la tuhuma za ufisadi, mawaziri wake wanarumbana!
5. Waziri Mkuu kawekwa kitanzi shingoni
6. CCM yake inasambaratika kwa kasi.....!

Huyu Mhe. Rais Kikwete yukoje jamani????

hv asingeweza kutuma mwakilishi?
 
hivi mbona sijawahi kusikia raisi mwingine yeyote kaja hapa kufanya ziara kwa siku 10, na wanaokuja msibani huwa wanatoa mkono wanaondoka, sasa yeye anataka mpaka aweke udongona taji kaburini ???
 
Mumsamehe huyu mtu kwani halijui alitendalo. Umeshawahi kuona Mkuu wa nchi anashabikia misiba ya nje ya nchi yake na msiba ulioko nyumbani kwake hauoni? Huyo ndiye mtu wa watu Bwana! haoni msiba wa baraza la mawaziri na haoni nchi ilipofika...sina rais!
 
Mara nyingi nchi ikiwa kwenye mapito magumu yeye anakuwa nje ya nchi na akirudi anakaa kimya nafiri umefika wakati wa yeye kukabidhi madraka kwa wasaidizi wake ili wajue nchi haina kiongozi.
 
Back
Top Bottom