Rais Banda auza ndege ya rais

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Rais wa Malawi, Joyce Banda, ameamua kuuza ndege ya rais pamoja na magari 60 ya fakhari.
120408080057_malawi_304x171_afp.jpg

Ndege hiyo ilinunuliwa kwa dola milioni-13 na rais aliyemtangulia, Bingu wa Mutharika, aliyefariki mwezi wa Aprili.
Rais Banda amenukuliwa kusema kwamba anatosheka kusafiri kwenye ndege za abiria kama watu wengine, kwa sababu ameshazowea kutembea kwa miguu na kusaidiwa na wasafiri njiani.
Fedha zitazopatikana katika mauzo ya ndege na magari hayo, zitatumiwa kuwasaidia maskini wa Malawi.
Serikali ya Uingereza, ambayo ndio mfadhili mkubwa wa koloni yake hiyo ya zamani, imepokea vema uamuzi huo kuwa ni ishara inayotia moyo.
source BBC
 
nchi zingine zinabahati sijui kwa nini isiwe sisi.!
 
Hivi Tanzania tutaweza kuiga huo mfano kweli?au ndio kwanza Jk ataagiza nyingine kwa ajili ya kuzururia ktk anga la nchi hii!!!maswali ni mengi,hongera Banda umethubutu umeweza.
 
Nasi tungeiga jamani pesa tuzielekeze kwenye madawati na madawa hospitali zetu...
 
haitakaa ije itokee tanzania,na ukiona hivyo ujue wajukuu wetu wananeema yawangoja
 
Hongera sana rais Banda kwa kuonyesha mfano wa kuigwa Afrika. Viongozi wengi Afrika wanajipenda mno na kuwasahau waliowaweka madarakani. Hilo lidege na magari ya kifahari uzilia mbali na hela hizo uvute bomba za maji safi ya kunywa.

Eee Mungu Baba, kwanini usiwapulizie viongozi wetu hapa Tz upepo huu wa busara?
 
Back
Top Bottom