Rais aweza kuwa mwizi?

Ndugu, wewe unanufaika na wizi nini?? Hivyo vya kijinga ni vipi hivyo- huu uzi ni wakijinga? Au elimu waliokupatia hawa hawa wezi ndio inalikuelimisha? Na huyo mtoto wako wa kufikirika unajua kinachomliza ni nini?

Wengine wamekusaidia hapo chini tumia JF kujifunza sio kuleta mawazo mgando.


Raisi wa nchi anapokuwa Mwizi. Swali zuri sana, na jibu lake ni kuwa Wezi katika nchi hiyo watakuwa ni watu wanaoheshimika na kuonekana mfano wa kuigwa.

mkuu usipate taabu kwa jinsi alivyoandika huyu buku 7 inaonyesha ni mshirika na mnufaika. siku zao zinahesabika na zaidi rais wao mwiz anazidi kuwafumbua macho raia wa kawaida kubwa tusikate tamaa vita ya ukombozi iendelee mwaka jana wameonja joto la jiwe lilikuwa kubwa kweny serikal za mitaa UKAWA wamefanya uharibif mkubwa kwa ccm.
 
Niambieni watanzania wenzangu maana inawezekana mkawa na ushahidi wa kutosha tangu JK hajaingia madarakani na hadi anaingia madarakani! kila kona sasa ni DOWANS! hata mtoto mdogo! ikiongezewa na majeraha ya nyuma kama vile RICHMOND, EPA/KAGODA, IMPORT SUPPORT COMMODITIES, MEREMETA, IPTL, RADA, na nyingine nyingi mnazozijua, inakifanya Chama Cha Mapinduzi Kionekane kama chama cha majambazi tena wenye roho mbaya ambao wakiwaingilia watawabaka, kulawiti na kuwaua na kuchukua kila kitu! Duh! mimi nimeogopa maana sasa watu wana hasira kwelikweli! Hebu niambieni, nipeni ushahidi wa kutosha huyu raisi wetu ni sehemu ya maovu haya niliyoyataja? lakini;
1. Mbona anaonekana mtu mwema?
2. Mbona anaonekana mpole na mwenye maadili?
3. Mbona anazungumza kwa upole na sauti nyororo?
4. Mbona hana makuu, watoto wake kusoma shule za kifisadi na majumba ya kifahari?

Mhh! jamani hasingiziwi??! Lakini;
1. Mbona Hazungumzii, DOWANS?
2.Mbona aliwapa muda EPAS kurudisha pesa baada ya kuwakamata mara moja na kuwafungulia mashitaka? na muda ulipofika alikaa kimya?
3. Mbona hazungumzii KAGODA na nyinginezo?
4.Mbona hawaongozi watanzania kuwapatia majibu kwa maswali magumu?
5. Mbona anapotezea mada kwa kuingiza topic ya udini baada ya uchaguzi wakati issues zilizopo ni wizi wa kura na DOWANS, EPA na nyinginezo?

Mhh! Jamani!!
1. Huyu JK si ndiye aliye kula kiapo cha kuilinda katiba ya nchi?! naambiwa pia alishika QUARAN?! Kwani humo kwenye quaran kunapindisha mambo?


NIPENI MAJIBU! USALAMA WA NCHI UPO MASHAKANI? CCM HAITASIMAMA KAMWE KAMA HAKUNA MAJIBU YA KINACHOULIZWA!

HAIWEZEKANI RAIS AKAONGOZA MAJAMBAZI KUIBIA NCHI! NAONA KAMA ANASINGIZIWA!!??

Asingiziwe mara ngapi? Kalagha bao.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom