RAIS awapandisha vyeo maofisa saba JWTZ

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
RAIS na Jakaya Kikwete* amewapandisha* vyeo,* makanali saba wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuwa mabrigedia Jenerali, kuanzia Septemba 2 mwaka huu.

Taarifa ya JWTZ* ilisema maofisa wanne miongoni mwa hao, walivalishwa vyeo hivyo* jana na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange katika makao makuu ya JWTZ, jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, waliopandishwa vyeo kutoka ukanali ni Brigedia Jenerali* Mangwamba, Brigedia Jenerali Kilama, Brigedia Jenerali Milinga, Brigedia Jenerali Emmanuel Maganga, Brigedia Jenerali Makere na Brigedia Jenerali Nassoro.

“Maofisa wanne kati yao wamevishwa vyei na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange katika makao makuu ya jeshi kwa niaba ya Amri Jeshi Mkuu na waliobaki watavalishwa vyeo baadaye kwa kuwa wako nje ya nchi,” ilsema taarifa.

Katika hatua nyingine, wananchi wa Kijiji cha Kiharaka, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, wamelilalamikia jeshi hilo kwa kushindwa kuwalipa fidia halali ya eneo ililolichukua.* Eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 192.10, lipo katika Mapinga wilayani humo na* lilichukuliwa na jeshi mwaka 2006 kwa shughuli za* kulenga shabaha, baada ya eneo lililokuwa la awali huko* Kunduchi,* jijini Dar es Salaam kuzingirwa na makazi ya watu. *

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti, wananchi hao walisema baada ya jeshi kusanifisha eneo hilo mwaka 2006 waliambiwa kuwa watalipwa fidia kulingana na ukubwa wa eneo la kila mtu.* Wananchi hao ambao hata hivyo hawakutaja majina yao yatajwe, walisema wanaodai fidia hawakupewa hundi ya kujua malipo yao.

Walisema hali hiyo ilisababisha malipo kutolewa kiholela na bila kujali thamani ya ardhi waliyomiliki.* “Malipo tuliolipwa awali yalikuwa* hayana risiti wala muhuri wa serikali, jambo ambalo tunahisi ni ujanja wa kutumia kofia ya* jeshi ili kutunyonya,” alisema mwanachi mmoja.

*“Kuna baadhi ya watu wameingizwa kwenye orodha ya kudai fidia ya malipo wakati hawakuwa na maeneo na hata hivyo, wamelipwa wakati wenye haki ya kulipwa hatujalipwa,” alisisitiza.* Hata hivyo, waathirika hao walidai* walishawahi kupeleka malalamiko yao kwenye ngazi mbalimbali ili lakini hadi sasa hayakushughulikiwa.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Magesa Mlongo, alipohojiwa juu ya madai ya wananchi hao alisema madai hayo si ya kweli. “Kuhusu kulipwa papo kwa papo wananchi walitaka wenyewe kwa kuwa wengi wao hawakuwa na akaunti,” alisema Mlongo.

Hata hivyo, Mthamini Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa* ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Temba, alikataa kulizunguzia suala hilo akidai kuwa yeye siyo msemaji wa jeshi.* Hata hivyo, Temba alisema jeshi linakusudia kuchukua eneo hilo watakapokamilisha malipo ya awamu ya tatu kwa wananchi na kwamba hilo litafanyika Desemba mwaka huu.*
 
Back
Top Bottom