Rais anapokuwa kibaka, Mutharika na maburungutu ya pesa uvunguni mwa kitanda!

Mutharikas-ndata-house.jpg

Lioneni hekalu la mfalme Mutharika la huko kwao Ndata.


Mjumba mkubwa hivi aligeuka kuwa tembo au ndo hivi vimwili vyetu vya kawaida tu,, binadamu ni wabnafsi sana
.
 
Huyu kafundishwa ni kina Mkapa ambao hadi Ardhi zenye madini wamejimilikishia kama kule muheza na Kiwira,
 
Kinachosikitisha sana ni upofu na kujuana hata kwa hawa waliomrithi mfalme Mutharika. Maana wameishasema eti mazishi yake yatamkamua Mmalawi maskini si chini ya kwacha 150,000,000. Alipaswa azikwe kwa pesa yake mwenyewe. Hilo hekalu hakuna shaka litaanza kuhudumiwa kwa pesa ya walipa kodi hao hao aliowaibia. Wizi ndani ya wizi alijisemea Remmy Ongala. Hamuoni Lowassa anavyolipwa pesa ya kustaafu wakati hakustaafu ukiachia mbali kutuachia balaa la mgao na ulanguzi wa umeme? Nani atamwajibisha nani iwapo samaki wote wana masharubu huku ngedere wote wakiwa wezi wa mahindi? Ama kweli kesi ya nyani mpelekee ngedere haki itatendeka kwa mahindi.
 
Huyu kafundishwa ni kina Mkapa ambao hadi Ardhi zenye madini wamejimilikishia kama kule muheza na Kiwira,

Mkuu STEIN, tafadhari usinikumbushe juu ya kumbakumba huyo!!! katiba ya Tz inampa kiburi sana, kama angeishi milele, mimi ningejinyonga hadi nife.
 
Hilo Ndata farm lenyewe lilikuwa na eneo kubwa balaa - japo miaka ya mwishoni alikata sehemu akatoa eti "zawadi" kwa Malawi na hapo kinajengwa chuo kikuu cha sayansi na teknilojia.
 
Haya bhana ila sijui bongo tukianza kuwasachi itakuaje maana waziri anakutwa na four milioni za matembezi

wametofautiana kidogo tu, mmoja anaficha chini ya kitanda na kutaka ziwe nyingi, mwingine anaenda nazo night club kuringishia mademu..
 
Bora mkulu wetu anazipeleka kila wiki kwenye zile nyumba mbvofu mbofu mpaka ufikirie kuzifwata hata uwe poliisi unahisi roho yako itakuwa halali yao
 
Mutharika, kurithishana na maburungutu ya dola

Chanzo: www.mpayukaji.blogspot.com


UROHO NA UNAFIKI WA MARAIS WETU


thumbnail.aspx
suitcase_468x269_to_468x312.jpg



Habari zilizoripotiwa na gazeti la Nyasa Times ni kwamba mabegi na masanduku yaliyojaa pesa yalikutwa kwenye chumba cha rais wa zamani wa nchi hiyo marehemu Bingu wa Mutharika. Habari zinaendelea kusema kuwa pesa hiyo ilikamatwa na polisi baada ya kugundua kuwa ndugu wa marehemu walikuwa wakipanga kuihamisha pamoja na mali nyingine za serikali. Ni aibu kiasi gani. kwanza kwa rais kuficha pesa uvunguni mwa kitanda tena kwenye karne ya 21?

Ni aibu kiasi gani kitendo hiki kinapotendwa na rais tena msomi aliyebobea katika uchumi? Je huyu rais alikuwa ameelimika kweli? Je ni watawala wangapi wa kiafrika ni aina ya Mutharika? Je wanajifunza nini ingawa uwezo wao wa kujifunza siku zote ni mdogo? Muhimu ni kuwaambia wazi kuwa kila mficha maradhi kilio kitamfichua kama ilivyotokea kwa Mutharika. Ajabu wakati rais akilalia mamilioni ya dola na kwacha, mamilioni ya watu wasio na hatia wanakufa kwa magonjwa yanayotibika! Je namna hii kuna haja ya kuwa na rais ambaye kimsingi ni mwizi anayeitwa mheshimiwa? Kama rais wa nchi maskini kama Malawi isiyo na raslimali za kutosha anakutwa na mamilioni ya dola uvunguni mwa kitanda hao marais wa nchi zenye raslimali nyingi kama DRC na Tanzania wanalilia mabilioni kiasi gani? Kwa habari zaidiBONYEZA HAPA.

Hawa wtu wengine hawa hakukuwa na sababu hata ya kufanya state funeral. Wangeenda zao taratibu tu. Imagine he wanted his young brother to take over after ending up his official terms. Alikuwa anafikiria yeye ni nani?
 
Hakuwa transparent, ndio maana watu walikuwa wanampinga kwa ufisadi lakini ni mchumi aliyebobea ndio maana alificha hela kwenye begi!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom