Rais anapokosea kuushika mwenge!

Msendekwa

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
442
168
Natazama sherehe za kuuzima mwenge hapa TBC1 kule Shinyanga.
Rais alipokabidhiwa mwenge na Capt. Honest Erenest Mwanosa, aliushika huku mkono wa kulia ukiwa chini, wa kushoto juu, wakati kinyume chake ndo utaratibu.
Je, ni kuwa hajui utaratibu au kasahau?
Najua mwenge kwa wengi wetu kwa sasa ni jambo la kipuuzi, ila nimeguswa na Rais kukiuka utaratibu.
 
Honestly to the majority of us, it does not matter, kwangu ingebidi hata autupe ni sawa tu, acha hilo la kuushika vibaya. Unatumia hela zetu bure na kuongeza maambukizi tu ya ukimwi!
 
Kingine wakati akipokea Risala toka kwa Capt Mwanosa alikuwa amevaa kofia sijui ilikuwa ya nini akavua na kuwapa wasaidizi.....Je Kuna jua au Usharabaro?
 
Angeushika mwenge huku mkono wa kulia uko juu na kushoto chini, halafu kumpa mkono wa pongezi kapteni Ernest kwa kutumia mkono wa kulia, ina maana angekuwa amebakiwa kuushika mwenge upande wa chini kwa mkono mmoja wa kushoto usio na nguvu, na mwenge ungekosa balance na kuanguka au kumuangukia rais kabisa! Nadhani JK alikuwa sahihi, hata kama ni kinyume na taratibu za gwaride la mwenge.
 
Kingine sasa watu wa Haki za watoto waishauri serikali kuwatesa watoto angalia walivyojaa majukwaani wakichomwa na jua watu wazima ni wale waliovaa nguo za kijani yaani CCM. Mi nasema kitendo hichi ni cha kuwatesa watoto.
 
mwenzenu anawaza safar yake ya muscat,yupo hapo kimwil tu mawazo yote yapo muskat weeeh!
 
Ningepata mtu aniondolee hao watoto walioanikwa juani kama dagaa au nguru,kisa mwenge its shame.......
 
Yaani kwanza hilo limwenge na lenyewe ni lifisadi,ingewezekana likatupwe baharini kabisa maana duu,bajeti yake simchezo.
 
JK Anasema sasa hivi kuwa'' UKIMWI NI UGONJWA WA KUJITAKIA"......LIVE TBC Je anafikiri wote wanaoumwa ukimwi wamejitakia?
 
Pesa za kuzunguka na limwenge zipo za kutosha,ila za kuwalipa walimu na madaktari,hizo kasungura kadogo.purumbashi kasorobo gov.
 
Angeushika mwenge huku mkono wa kulia uko juu na kushoto chini, halafu kumpa mkono wa pongezi kapteni Ernest kwa kutumia mkono wa kulia, ina maana angekuwa amebakiwa kuushika mwenge upande wa chini kwa mkono mmoja wa kushoto usio na nguvu, na mwenge ungekosa balance na kuanguka au kumuangukia rais kabisa! Nadhani JK alikuwa sahihi, hata kama ni kinyume na taratibu za gwaride la mwenge.

Hv umeshawahi kuubeba mwenge?
Ni mzito, kiasi kwamba huwezi ubeba kwa mkono mmoja.
 
JK Anasema sasa hivi kuwa'' UKIMWI NI UGONJWA WA KUJITAKIA"......LIVE TBC Je anafikiri wote wanaoumwa ukimwi wamejitakia?
Njia za maambukizi ni pamoja na yale ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na matumizi ya vifaa vyenye ncha kali vilivyotumiwa au kuambukizwa na yule mwenye virusi kisha kutumiwa na mwingine asiye na virusi.
Je haya maambukizo katika mazingira haya ni ya kujitakia?
Raisi hana taarifa kamili.
Je anajua wenye virusi wananyweshwa ARV 'fake'?
 
hata angeuacha ukadondoka sawa tu huo utaratibu unaousema umeandikwa wapi?
Tanzania ni nchi pekee duniani maskini inayotumia mwenge kwa garama kubwa kuzindua miradi yenye thamani isiolingana na garama za ukimbizaji wa huo mwenge sijui uchawi. HII kitu ni ya kuchoma moto hautufai kwa kizazi hiki cha science na teknlojia
 
Nani aliyeanzisha iyo sheria ya kushika?? Muda jangeani au tume tu iliyokula kodi yako?!
 
Mwenge jamani si kitu kibaya, tatizo ni siasa ndani ya mwenge, mpaka leo si tunaona olimpic unavyohawasisha? Sisi wazalendo wa kweli tulipata mafunzo ya kupokea mwenge nikiwa primary miaka ya themanini.
 
Labda ungetusaidia kwa mujibu wa katiba ya nchi , kikanuni mwenge watakiwa ubebejwe !
Au kama iko sheria ndogo iliyotungwa kuhusu hilo. Ndiyo tutachangia vizuri.
 
Natazama sherehe za kuuzima mwenge hapa TBC1 kule Shinyanga.
Rais alipokabidhiwa mwenge na Capt. Honest Erenest Mwanosa, aliushika huku mkono wa kulia ukiwa chini, wa kushoto juu, wakati kinyume chake ndo utaratibu.
Je, ni kuwa hajui utaratibu au kasahau?
Najua mwenge kwa wengi wetu kwa sasa ni jambo la kipuuzi, ila nimeguswa na Rais kukiuka utaratibu.

manajeshi feki.lini mjeshi akashindwa kushika mwenge!!
 
Acha uongo.
Kafafanua na njia zingine za maambukizi.
Ndo nyie mnaosoma robo ya mstari wa baibo na ku-draw concludion.
Hata kama kataja njia zote, tunachozungumzia hapa ni kauli ya UKIMWI NI UGONJWA WA KUJITAKIA ni kauli stahili kutolewa na kiongozi wa nchi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom