Rais anapodanganya Umma na kulialia eti Umasikini...

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Rais Kikwete akiwa safarini kwenda Davos, alisimama LIbya na kukutana na Ghaddafi na kumpa shukrani kwa msaada uliotolewa na Libya kujenga nyumba kwa familia zilizoathirika kwa mafuriko.

Katika hotuba yake, Rais Kikwete alisema yafuatayo ambayo nayanukuu na kuyajengea hoja ya yeye kuudanganya umma!

Nanukuu gazeti

"Rais alisema mafuriko hayo yaliyotokana na mito miwili, ukiwamo Mto Mkondoa kuacha njia za asili na kubomoa kingo, yameharibu mno miundombinu ya barabara na reli kiasi kwamba Serikali ya Tanzania inahitaji kiasi cha dola za Marekani milioni 15 (zaidi ya Sh bilioni 15) kukarabati miundombinu hiyo.

Ni hasara kubwa kwetu. Kiasi cha dola za Marekani milioni 15 ni nyingi kwa nchi masikini kama Tanzania lakini tumeamua kuwa ukarabati huo utakuwa umekamilika katika muda mfupi.

Rais anadai Taifa letu ni masikini sana na dola milioni 15 ni nyingi sana!"

Kweli dola Milioni 15 ni nyingi hasa zikitumika kwa matumizi yasiyo ya msingi au kipaumbele mbayo ni jambo la kawaida sana kwa Serikali ya Tanzania kutumia fedha kwa mambo yasiyo ya msingi au kipaumbele kwa Taifa zima.

Hata kama fedha hizi zingekuwa ni za mtu, shirika au Taasisi binafsi, inapofikia kuwa fedha zinatumika kwa minajili ya kuwa zipo zitumike, swali linakuja, iweje kama Taifa tuendelee kudai sisi ni masikini?

Kwa nini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaendeleza ulaghai, udanganyifu na kutukuza umasikini na unyonge kwa kudai eti nchi ni masikini hatuwezi kuwa na Dola milioni 15 na kuzitumia kwa vitu vya muhimu?

Labda nitumie Jedwali hili kuonyesha ni vipi kauli ya Rais ni ya kizandiki na kinafiki!

1. Benki Kuu imejenga na kukarabati nyumba nne kwa ajili ya Gavana na manaibu wake. Jumla ya gharama zote ni karibu Shilingi Billioni 6 ambazo ni sawa na Dola Millioni 5 ambayo ni asilimia 30 ya Dola Milioni 15.

2. Nyumba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, shirika la umma linalokabiliwa na matatizo ya kifedha kuipatia Tanzania umeme wa kutosha, imegharimu si chini ya Shilingi Bilioni 1.5 ambazo ni sawa na Dola Milioni 1 na ni asilimia 7 ya Dola Milioni 15 zinazohitajika kujenga hii barabara iliyoharibiwa na mafuriko.

3. Chama Cha Mapinduzi, kimetumia takribani kati ya Shilingi Billioni 9 na Bilioni 14 kununua magari 200 kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Taifa wa mwaka huu 2010. Magari haya kutoka Japani ambayo nayapa makadirio kutokana na bei za International Motor Mart au Toyota Motors of Tanzania ambazo kwa magari ya Toyota kati ya Rav4 na Land Cruiser VX yana bei ya chini bila kodi na ushuru kati ya Dola 35000 na Dola 55000. Hivyo iwe kwa kadirio la chini la Shilingi Bilioni 9 ambayo ni sawa na Dola Milioni 7 ambayo ni asilimia 47 ya dola milioni 15.

Kwa mifano hiyo mitatu ya matumizi ya Taasisi na Mashirika yanayohusiana na Serikali ya Tanzania, ni dhati kuwa Tanzania ina uwezo wa kujitegemea na hizo dola milioni 15 si nyingi sana kiasi cha kutangazia umma na dunia kuwa eti sisi ni masikini! Ukichukua matumizo yote ya hizi taasisi tatu tuu, unakuta kuwa tayari Tanzania dola Milioni 13 ambazo ni asilimia 86 ya dola Milioni 15 zinazohitajika kujenga upya barabara na reli huko Morogoro!

Jana katika hotuba yake kwa Bunge la Marekani, Rais Barack Obama aligusia suala la matumizi ya lazima na umuhimu wa Serikali ya Marekani kufunga mkanda na kuachana matumizi yasiyo ya busara na ya holela.

Je Rais Kikwete baada ya miaka yako minne ya kuwa madarakani:

a. umefanya nini kupunguza deni la Taifa?
b. umeanya nini kupunguza matumizi ya Serikali?
c. umefanya nini kuondokana na umasikini?

Nasubiri majibu kutoka kwa Rais mwenyewe au Wapambe wake!
 
You nailed it mkuu, inatia hasira mpaka basi. Suppose we put an educated guess on how much is spent for him and his delegates to do this globe troting............... Unaweza kukuta hiyo $15mn is just for 3 trips!!!!!!
 
Rais Kikwete akiwa safarini kwenda Davos, alisimama LIbya na kukutana na Ghaddafi na kumpa shukrani kwa msaada uliotolewa na Libya kujenga nyumba kwa familia zilizoathirika kwa mafuriko.

Katika hotuba yake, Rais Kikwete alisema yafuatayo ambayo nayanukuu na kuyajengea hoja ya yeye kuudanganya umma!

Nanukuu gazeti

Rais anadai Taifa letu ni masikini sana na dola milioni 15 ni nyingi sana!

Kweli dola Milioni 15 ni nyingi hasa zikitumika kwa matumizi yasiyo ya msingi au kipaumbele mbayo ni jambo la kawaida sana kwa Serikali ya Tanzania kutumia fedha kwa mambo yasiyo ya msingi au kipaumbele kwa Taifa zima.

Hata kama fedha hizi zingekuwa ni za mtu, shirika au Taasisi binafsi, inapofikia kuwa fedha zinatumika kwa minajili ya kuwa zipo zitumike, swali linakuja, iweje kama Taifa tuendelee kudai sisi ni masikini?

Kwa nini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaendeleza ulaghai, udanganyifu na kutukuza umasikini na unyonge kwa kudai eti nchi ni masikini hatuwezi kuwa na Dola milioni 15 na kuzitumia kwa vitu vya muhimu?

Labda nitumie Jedwali hili kuonyesha ni vipi kauli ya Rais ni ya kizandiki na kinafiki!

1. Benki Kuu imejenga na kukarabati nyumba nne kwa ajili ya Gavana na manaibu wake. Jumla ya gharama zote ni karibu Shilingi Billioni 6 ambazo ni sawa na Dola Millioni 5 ambayo ni asilimia 30 ya Dola Milioni 15.

2. Nyumba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, shirika la umma linalokabiliwa na matatizo ya kifedha kuipatia Tanzania umeme wa kutosha, imegharimu si chini ya Shilingi Bilioni 1.5 ambazo ni sawa na Dola Milioni 1 na ni asilimia 7 ya Dola Milioni 15 zinazohitajika kujenga hii barabara iliyoharibiwa na mafuriko.

3. Chama Cha Mapinduzi, kimetumia takribani kati ya Shilingi Billioni 9 na Bilioni 14 kununua magari 200 kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Taifa wa mwaka huu 2010. Magari haya kutoka Japani ambayo nayapa makadirio kutokana na bei za International Motor Mart au Toyota Motors of Tanzania ambazo kwa magari ya Toyota kati ya Rav4 na Land Cruiser VX yana bei ya chini bila kodi na ushuru kati ya Dola 35000 na Dola 55000. Hivyo iwe kwa kadirio la chini la Shilingi Bilioni 9 ambayo ni sawa na Dola Milioni 7 ambayo ni asilimia 47 ya dola milioni 15.

Kwa mifano hiyo mitatu ya matumizi ya Taasisi na Mashirika yanayohusiana na Serikali ya Tanzania, ni dhati kuwa Tanzania ina uwezo wa kujitegemea na hizo dola milioni 15 si nyingi sana kiasi cha kutangazia umma na dunia kuwa eti sisi ni masikini! Ukichukua matumizo yote ya hizi taasisi tatu tuu, unakuta kuwa tayari Tanzania dola Milioni 13 ambazo ni asilimia 86 ya dola Milioni 15 zinazohitajika kujenga upya barabara na reli huko Morogoro!

Jana katika hotuba yake kwa Bunge la Marekani, Rais Barack Obama aligusia suala la matumizi ya lazima na umuhimu wa Serikali ya Marekani kufunga mkanda na kuachana matumizi yasiyo ya busara na ya holela.

Je Rais Kikwete baada ya miaka yako minne ya kuwa madarakani:

a. umefanya nini kupunguza deni la Taifa?
b. umeanya nini kupunguza matumizi ya Serikali?
c. umefanya nini kuondokana na umasikini?

Nasubiri majibu kutoka kwa Rais mwenyewe au Wapambe wake!

Mkuu, rent ya nyumba ya gavana ili USD7800 kwa mwezi,ambayo kwa mwaka ni USD93,600.Sijui kama huyu Rahisi wetu anajua kuwa hata nchi Tajiri haziwezi kufanya upuuzi kama huu.
 
Rev Kishoka, na wachangiaji wengine wenye mapenzi mema kwa nchi yetu ya Tanzania, ninakupongezeni sana kwa brief analysis inayoonyesha jinsi Rais wetu anavyodanganya na haoni aibu kulia lila. Kwa mifano michache tu uliyoorodhesha, mtu mwenye akili ataelewa huo umaskini ambao Rais Kikwete anapigia filimbi ni upi. Ningemuelewa kama angesema, "Umakini Tanzania unatokana na chama tawala kuwa na uongozi ulioigawa nchi sio katika misingi ya ukabila tena kama ilivyodhaniwa, bali maskini na matajiri, mostly mafisadi."

Na hawa matajiri wanatumia kodi ya mwananchi kwa mfano kujinenepea na sio kwa lengo la kuwakomboa wananchi kutoka katika umaskini. Mimi ninasema hata MKUKUTA ni propaganda! JK anapowaambia wananchi kuwa kukarabati sehemu zilizo za maafa ni hela nyingi, lakini yeye anakuwa na convoy kuzunguka dunia...how much they spend each day on his trips? Ni akinamama wangapi wanakufa Mawenzi Hospital kila siku tu kwa kukosa vitu vidogo na vya gharama ndogo ambavyo serikali ingeweza walau kuhakikisha vipo? Morogoro Hospital ni mfano; mama mjamzito anatakiwa kwenda kujifungua atakuwa anabeba ndoo (kwa ajili ya kujisaidia), nguo nyembe, nk. Hadi lini, wakati huo huo mkubwa anayetakiwa kushughulikia tatizo hilo anapimwa afya Marekani, Ufaransa, Uswisi, nk.? Hizi dola za safari hizo kwa mwaka ni takriban 200% ya dola milioni 15 kwa ajili ya kukabiliana na maafa.

Lingine ni kuwa, Watanzania tutadanganywa hadi lini? Serikali badala ya kuangalia matatizo ya wananchi, inaweka nguvu kuhakikisha inashinda uchaguzi unaofuata hata kama ni miaka 5 baadaye. Maendeleo yatatoka wapi?

Ndugu zangu, tuamke. Mwaka 2005 marafiki zangu walipokuwa wanamsherehekea JK kupitishwa kugombea uraisi, nilipatwa na homa ya ghafla kwa sababu za kuhofia kuwa "hawakuwa naejua nini kiko mbele yao," yaani umaskini. Leo hii nikiwauliza walichokuwa wanasherehekea, hakuna hata mmoja anayethubutu kuniangalia usoni. Tunakokwenda ni wapi?

Umakini Tanzania ni wa kujitakia, haswa kwa kiwango kikubwa ikiwa ni sera isiyoeleweka ya serikali. Watu wakiendelea kuwa maskini, ukiwapa kanga wakati wa uchaguzi, basi watakuchagua maana watona wewe ni mfalme. Burundi, Rwanda, na Angola, ambazo zimekuwa na vita siku nyingi, leo ziko wapi? Tanzania iko nyuma sana.

Asante sana Rev Kishoka!
 
Mchungaji,

Sijawahi kuona mkuu wa nchi kama rais wetu; huwa najisikia vibaya sana nikimsikiliza akiongea mambo muhimu ya taifa letu. Utakumbuka wakati wa mktikisiko wa uchumi wa dunia, aliwahi kusema maneno haya baada ya kuulizwa nchi itaathirika vipi na janga hili: "hili haliwezi kutukumba sisi, ni kwa ajili ya mataifa makubwa na mabenki yao, sisi tuna benki ndogo ndogo hivyo hilo si letu."

Nilishangaa sana na kauli hiyo, yaani yeye alijua kuwa tatizo la uchumi ni kwa ajili ya mabenki tu? Sasa sijui tatizo ni uwelewa wake mdogo au wa wasaidizi wake.

Mie mpaka sasa sijaelewa, ila kwa kuwa alisema huwa hawasikilizi wasaidizi wake, nina wasiwasi sana na uwezo wake wa kung'amua mambo. Haiwezekani kuongea bilioni 15 ni nyingi kwa nchi kama hii, ambayo ina motorcade za BMW na posho nyingi. Pesa zipo na azitumie vizuri, zilitoka wapi za RDC? Huku ni kututia aibu tu.
 
Gembe.. siku chache zilizopita alipokuwa akizungumza na mabalozi kwenye sherry party alizungumzia gharama ya ujenzi wa hiyo miundo mbinu... alisema ni bilioni 10! juzi Engineer Chambo akasema sijui bilioni 13.. leo wamefikia bilioni 17, by the end of next week itakuwa bilioni 20.

I got a pendekezo.. why not go to bilioni 50 yaishe. It looks we have a thing for 50!!
 
Mkuu,rent ya nyumba ya gavana ili USD7800 kwa mwezi,ambayo kwa mwaka ni USD93,600.Sijui kama huyu Rahisi wetu anajua kuwa hata nchi Tajiri haziwezi kufanya upuuzi kama huu.
Na ya Speaker Sitta kule Dodoma ni dola elfu nane kwa mwezi. Tunahitaji jasiri mmoja wa kufanya mabadiliko ya uongozi wa Nchi yetu kwa amani.
 
Mchungaji,

sijawahi kuona Mkuu wa nchi kama rais wetu;huwa najisikia vibaya sana nikimsikiliza akionglea mambo muhimu ya taifa letu.utakumbuka wakati wa mktikisiko wa uchumi wa dunia aliwahi kusema maneno haya baada ya kuulizwa nchii itaathirika vp na janga hili; "hili haliwezi kutukumbuka sisi,ni kwa ajili ya mataifa makubwa na mabenki yao,sisi tuna benki ndogo ndogo hivyo hilo si letu".

Nilishangaa sana na kauli hiyo,yaani yeye alijua kuwa tatizo na Economic recesion ni kwa ajili ya mabenki tu?sasa sijui tatizo ni uwelewa wake mdogo au wa wasaidizi wake?

Mie mpaka sasa sijaelewa ila kwa kuwa alisema huwa hawasikilizi wasaidizi wake nina wasiwasi sana na uwezo wake wa kung'amua mambo.Haiwezekani kuongea bilion 15 ni nyingi kwsa nchi kama hii ambayo ina motorcade za BMW na posho nyingi..pesa zipo na azitumie vizuri,zilitoka wapi za RDC?huku ni kututia aibu tu

Mkuu wetu wa nchi, anasikitisha sana. Kwa kweli nakumbuka jinsi alivjojibu kuhusu economic recession, ni aibu tupu!!

Mi nahisi inawezekana ni mbishi, hawasikilizi washauri wake au washauri hawamuandai vizuri. Kuna tatizo sehemu!!
 
Ina maana hata wataalamu wa kujumlisha hasara iliyotokea katika hiyoo miundombinu bado ni TATIZOOO??

Hakuna cordination mpaka kwenye assesment inavyoonekana wizara wana yao na IKULU wana yao.!!! capacity limitation in thinking!!!!!!!!!!!!!!
 
Gembe.. siku chache zilizopita alipokuwa akizungumza na mabalozi kwenye sherry party alizungumzia gharama ya ujenzi wa hiyo miundo mbinu... alisema ni bilioni 10! juzi Engineer Chambo akasema sijui bilioni 13,leo wamefikia bilioni 17, by the end of next week itakuwa bilioni 20.

I got a pendekezo.. why not go to bilioni 50 yaishe. It looks we have a thing for 50!!

Tatizo la Muungwana hajui nini kinaendelea;tabia yake ya kupenda sifa ndiyo tatizo na najua mwanzoni inawezekana alimpigia chambo coz ni swahiba wake na kumuuliza "hivi ni shilingi ngapi itatosha kurekebisha barabara zilizoharibu?",chambo akamwambi kama bilioni 10 hivi.Navyomfahamu jamaa lazima akaidandia hiyo bilioni kumi na kuwaambia wafadhili.

Baadaye TANROADS walipohakiki na kufana tathmini ikafikia bilion 13 na hii ni wiki iliyopita kwenye cabinet sasa leo huko Libra anasema bilion 15;hivi kweli tuna shida ya pesa ndogo ndogo kama hizi?na bado mkulu na Shein wanasafiri safiri kwenda nje?inaingia akilini?

Kila siku anang'ang'amia kukutana na Marais wa marekani Je anajifunza nini kutoka kwao?au ndiyo kupiga picha tu na kusema kuwa mie ni rais wa kwanza kuonana na Obama?inaongeza nini kwa wananchi?Obama majuzi alisema kuna haja ya viongozi kuwatumikia wananchi zaidi ya kujihudumia nafsi zao.

Miaka minne amenekana ameshindwa ila anatakiwa ajipange na kuangalia njia ya nzuri za kubadilisha uchumi wa nchi hii;Rejea mwelekeo wa sera ya chama cha mapinduzi kwa miaka kumi ambao lengo lilikuwa ni kujenga taifa leny uchumi unajitegemea ;kuondoa utegemezi wa wafadhili katika shughuli za kimaendeleo ,mkapa aliweza kuanzisha mfumo huu kwa kujenga mfumo mzuri wa ukusanyaji mapato.

kuanzia mwaka 2005 kumekuwa na kusuasua kwa mafanikio wa kiuchumi na kushuka kwa hazina ya pesa za kigeni na hili linachangiwa na wizara ya fedha na uchumi kuongozwa na mawaziri wasio na uwezo;mawaziri wanaopenda safari za nje kila siku bila kufanya kazi za kujenga na kusimamia uchumi(October -Dec TRA hawakufkia lengo laukusanyaji mapato)

Kama unakuwa na kiongozi mkuu(Muungwana) ambaye anaenda nje kuombamsaada wa kifedha;kuna haja gani ya kila waziri naye kusafiri kwenda nje?kufanya nini?kwanini serikali isiwe inapelekea wataalamu vijana(watendaji) nje ili wakajifunze na kuja kufanya kazi kwa ufanisi?ila kila siku utasikia mawaziri wako canada..wtf?Hata Memeb hana haja ya kusafiri coz kuna mabalozi kule.nchi haina maendeleo yoyote kwanini tunakuwa na gharama kubwa za kupeleka mawaziri safari za nje?ulimbukeni?

Taifa lilipo hivi sasa,mpaka tunaanza kulilia bilioni 15 ni wakati sasa ambapo linahitaji kiongozi ambaye atakuwa anajua taifa linaendaje?priority zetu ni zipi?tunakiwa tufanye jambo gani ili kufanikisha mipango yetu?pesa zitatoka wapi?usimamizi ukoje?.

Kimsingi tunahitaji kubadilika sana;tena sana!Mzee mwanakijiji naomba umtumie Muungwana hotuba ya state of union ya juzi ili asome na aone jinsi wengine wanavyojua kueleza mambo .

Na kwa kuwa atakaye mpinga Jk atakufa basi ajifunze na tunahitaji mabadiliko na haya ni mawazo yangu kwake na wapambe wake.

Gembe
 
Mkuu Bullet ;

Ndiyo kasomea uchumi ila siyo mtaalam wa mambo ya uchumi!
 
Tatizo la viongozi wa nchi yetu ni kukosa priorities, ni mara nyingi sana tumeshuhudia mambo yasiyo na tija kwa taifa hili ndiyo yanayotiliwa mkazo sana na serikali yetu na ndiyo hayo yanayotugharimu mabilioni ya pesa, ni ulimbukeni, roho za ulafi na ubinafsi wa viongozi wetu unaowafanya wasahau kabisa dhamana tuliyowapa ya kutusaidia kuongoza taifa hili.

Nakumbuka kipindi fulani rais alisema eti "anasikitishwa sana na umaskini wa watanzania", kwangu nie kauli hii niliiona kuwa ni ya kizandiki isiyo na ukweli hata kidogo zaidi ya kujikomba kwa wananchi, kama kweli umaskini wa watanzania unamnyima usingizi mbona hatuoni lolote la maana analofanya kuwakwamua watanzania na umaskini huo, kazi imekuwa kupiga misele tu huko ughaibuni kuomba misaada, kweli Tanzania tumeshindwa kumanage resources tulizonazo hadi leo hii tumekuwa ombaomba..,ni aibu sana kwa kweli.

Marehemu Baba wa Taifa [RIP] aliwahi kusema kuwa nchi hii haiwezi kuendelea kwa misaada, kwani ni uongo.., si haya tunayaona sasa, kama misaada tunayopewa ingeweza kutuendeleza sasa hivi tusingekuwa na unyonge huu tulionao, tungekuwa moja kati ya African Superpowers lakini misaada yote ya wazungu inaishia mifukoni mwa viongozi wetu kwa matumizi yasiyo na msingi hata kidogo..,inauma sana eti leo hii miaka 49 baada ya Uhuru Tanzania bado ina maeneo yasiyofikika kwa barabara, hayana umeme wala huduma za afya na maji safi na kila siku tunasikia misaada ya kuendeleza miundiombinu ya nini sijui.,mbona hawa wenzetu hawafaidiki nayo.,yote inaishia mikoa fulani fulani ambayo baadhi ya viongozi wanatoka na mikoa mingine inaendelea kukandamizwa.

Ni aibu kubwa sana kwa Rais mzima kwenda huko ughibuni na kulia eti Tanzania haina dola nilioni 15, huu ni uongo wa hali ya juu, kama angejali kweli si serikali yake ingepunguza matumizi ya kipumbavu, hiyo bilioni 15 si ingepatikana fasta tu, ni picha gani ambay hawa viongozi wetu wanatujengea huko nje?, kwa mtaji huu tutaachaje kudharaulika huko duniani?.,wanapambana na ombaomba njiani wakati bwana mkubwa mwenyewe ndiyo ombaomba namba 1.,viongozi wetu lazima wabadilike kwa kweli, wamejisahau sana inawezekana ni kutokana na huu ukondoo tuliojivika sie wananchi..,lazima tupaze sauti zetu kukemea ujinga huu.,watatusikia tu kwani sisi si ndio waajiri wao jamani......?

Naomba kuwasilisha.
 
Wanafikiri sisi sote ni wajinga....!

La hasha.

Wanajua sio wote ni wajinga. Ila wanajua wengi kupindukia ni wajinga hivyo wanatumia hiyo fursa kujinufaisha.

Wanajua werevu wachache hawawezi kuwawajibisha. Sio sasa wala hivi karibuni.
 
Nadhani Mkuu alienda bila kujitayarisha au wsaidizi wake walimwandalia hotuba kyk ndege na kuprint walipotua Airport Libya

Inashangaza sana serikali ilishindwa kufanya tathmini ya hasara, any way amwombe Gadhafi

Vipi ha kwenda na mama Salma.
 
Inashangaza sana serikali ilishindwa kufanya tathmini ya hasara [/FONT]
Hapana; Wanajua sana. Ila sema tu kwamba huu ni utaratibu wetu wa kawaida hapa Tz kubadirisha badilisha makadilio ya ghalama za ujenzi ili mwishoni mwa siku kile cha juu kiweze kutunufaisha wachache. Kazi na dawa - Ufisadi kwa kenda mbele. (Yale ma-Twin Towers ya BOT) Watanzania tuna kazi ya ziada katika kuidhiti / kukomesha tabia hii miongoni mwa watendaji wetu.
 
Je Rais Kikwete baada ya miaka yako minne ya kuwa madarakani:

a. umefanya nini kupunguza deni la Taifa?
b. umefanya nini kupunguza matumizi ya Serikali?
c. umefanya nini kuondokana na umasikini?

!

Maisha Bora kwa Mtanzania yanawezekana kweli?
Matumizi ya serikali yako juu, kila siku wakuu ni ngonjera tu za kupunguza matumizi, Pinda alisema uongo kuwa serikali itasitisha matumzi ya Mashangingi, lakini mpaka sasa kitendawili,

Umasikini unaongezeka, Sasa hivi Gap ya tajiri na masikini iko juu. Je kikwete unasemaje juu ya Hili? Embu punguza safari za nje walau kidogo tu ili pesa unazotumia kwenye safari ziweze kutumika sehemu nyingine, Au safari nyingine tuma mwakilishi au balozi akuwakilishe ili upunguze gharama.
 
Kishoka

Naongezea tu kwenye analysis yako fupi kuwa Tanzania inazo pesa

Tazama hivi kuna kesi ngapi mahakamani ambazo serikali inawashtaki watendaji wake na wafanyabiashara kwa kuchota pesa za umma

  • EPA 133b
  • BOT majengo pacha a.kak Liyumba scam 221b
  • BOT utangenezaji noti >100b
  • Mramba na mambo yake >13b
  • Ongeza nyingine
Sasa unaweza kuibiwa kama huna? Maskini anaibiwa nini sasa wakati hana

Zipo ndo maana zinaibiwa
 
Back
Top Bottom